Mungu Hafanyi Kazi na wanaokata Tamaa

Mungu Hafanyi Kazi Na Wanaokata Tamaa… Mungu Hafanyi Kazi Na Wale Ambao Wakianguka Wanaamua Kukata Tamaa Na Kuamua Kulala Hapo Na Kusubiri Kifo Kiwakute Hapo Wamelala.
Mungu Anawapenda Wale Watu Ambao Wakiangushwa Au Kuanguka Katika Safari Ya Maisha Wanainuka, Wanafuta Vumbi, Wanafunga Vidonda Vyao Na Wanaendelea Na Safari.
Hata Kama Kuna Jambo Limekuangusha; Ndoa, Biashara, Mahusiano (Umeachwa/ Umeachika), Huduma Haichanui (Idadi Ya Washirika Haiongezeki, Wengine Wamekugeuka Na Kuanza Kukusema Vibaya Na Kwa Maneno Ya Uongo), Ndugu, Wazazi Wamekutelekeza, Umefukuzwa Kazi Au Umepitiwa Na Punguza Punguza… Hapo Si Mwisho; Inuka, Simama, Jifunge Kiume, Maisha Yanaendelea… Maadamu Unao UHAI, UNA PUMZI, UNAISHI Unaweza Kuyapata Yote Uliyopoteza Na Zaidi… Unamkumbuka Ayubu? Hakuishia Kulia Wala Kumuwazia Mungu Kwa Upumbavu, Katika Mambo Yote Aliyokutana Nayo, Ayubu Hakutenda Dhambi… Bali Kwa Ujasiri Alisema Maneno Yafuatayo Ambayo Nataka Uyachukue, Yawe Kauli Mbiu Yako Ya Imani Na Yahifadhi Hadi Pale Mungu Atakapo Kutengenezea Mlango Wa Kutokea!

“Kwani Yako MATUMAINI Kwa MTI Ya Kuwa UKIKATWA (Ukidondoshwa) UTACHIPUKA TENA, Wala MACHIPUKIZI YAKE HAYATAKOMA. Ijapokuwa Mizizi Yake HUCHAKAA MCHANGANI, Na Shina Lake KUFA Katika Udongo; Lakini KWA HARUFU YA MAJI (Mpenyo Toka Kwa Bwana) UTACHIPUKA Na KUTOA MATAWI (Kuongezeka) Kama Mche” (Ayubu 14:7-9)

“Hapo WATAKAPOKUANGUSHA, Utasema KUNA KUINUKA TENA” (Ayubu 22:29a)

HUYU NI MUNGU NDANI YANGU, ANAKUSALIMIA NA KUKUPA WAZO LAKE KUHUSU CHANGAMOTO YAKO!

Nakupenda Sana, Haijalishi Changamoto Yako, Mungu Yuko Pamoja Nawe Taabuni Ili Apate Kukuokoa Na Kukutuza/ Kukufunika Kwa Utukufu (Zaburi 91:15)

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: