NIMEKUTANA NA MUNGU KWENYE MAZINGIRA YANGU; WEWE HAUJAKUTANA NAYE HAPO KWENU??

Kukutana na Mungu

Sijawahi Kuona Nyumba Isiyo Na Mjenzi… Chungu Kisicho Na Mfinyanzi… Chuma Kisicho Na Muhunzi… Mtoto Asiyekuwa Na Mama… Msiba Usio Na Marehemu… Harusi Isiyo Na Wanandoa… Lenye Mwisho Lisilo Na Mwanzo… Kubwa Lisiloanzia Udogo… Mshindi Asiye Na Aliloshinda… Mzazi Asiye Na Mwana… Hekima Bila Uwepo Wa Upumbavu… Akili Bila Uwepo Wa Ujinga Nk!

Je Kama Yote Hayo Yapo Kwa Sababu Kuna Vyanzo; Kweli Kwa Akili Yako Timamu Unadhani MPANGILIO Wa Jua Kuwaka Mchana, Mwezi Na Nyota Usiku, Umejianzisha? Dunia Kuwa Katika Mhimili wa Nyuzi 23 na Nusu Ambazo Zinafanya Maisha Yawezekane Kwenye Sayari Hii Tofauti Na Sayari Zingine… Kiwango Cha Jua Kinachotua Juu Ya Uso Wa Dunia Kuwa Kiwango Sahihi Na Maalumu Kuruhusu Maisha Tofauti Na Sayari Zingine, Unadhani Yote Haya Ni BAHATI TU? Kwa Ufahamu Wako Wote Ulionao Unafikiri Kwamba Maisha Yametokana Na Seli Moja Iliyopasuka Na Kuzaa Aina Zote Za Viumbe? Kwa Uwezo Wako Wa Kimawazo Unafikiri Nyani Alibadilika, Hatua Kwa Hatua, Miaka Kwa Miaka Hadi Kufikia Hatua Ya Kutokea Nyani-Wewe Uitwaye Binadamu? Kwa Kuangalia Viumbe Hai Wa Namna Zote, Kuanzia Tembo, Nyangumi, Hadi Kwa Viumbe Wadogo Vimelea Wasioonekana Kwa Macho, Bado Unaamini Dunia Na Kila Kiijazacho Ni Matokeo Ya “THE BIG BANG THEOREM”? Hivi Utaratibu Wa Uzazi, Unaousisha KE na ME, Hatua Za Ukuaji Kwenye Tumbo Hadi Kujifungua, Kichanga Hadi Uzee Ni Matokeo Tu Ya Asili YASIYOPANGILIWA NA KURATIBIWA KWA UFAHAMU WA JUU SANA? Hivi Kwa Namna Seli Ndogo Sana Ilivyoundwa Kwa Namna Tata Sana…Seli Tofauti Kuunda Tishu Moja… Tishu Tofauti Kuunda Kiungo… Viungo Kadhaa Kuunda Mfumo… Mifumo Kadhaa Tofauti Kuunda Kiumbe, Bado UAMINI TU Kuwa Kuna MKONO WA FUNDI STADI; Aliyeifanya MBINGU, NCHI NA KILA KIUMBE, RATIBA NA MIFUMO YOTE? Huyu Fundi Anaitwa MUNGU… ALIYE HAI, WA KWANZA NA WA MWISHO, MZEE WA SIKU, ALIYEKUWAKO, ALIYEKO NA ATAKAYEKUJA..!

Leo Hama Kutoka Kwenye Kundi La Wapumbavu… Maana “MPUMBAVU AMESEMA MOYONI MWAKE YA KWAMBA HAKUNA MUNGU”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: