UKIWEZA? YOTE YANAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE!

Kwa Mungu kila kitu kinawezekana

Mtu Mmoja Alileta Kesi Kwa Yesu Akihitaji Msaada Juu Ya Tatizo La Ugonjwa Wa Kifafa Lililokuwa Linamtesa Mwanae Tangu Utoto Wake, Na Alikuja Na Kauli Za “HURUMA HURUMA” Naye Alimwambia BWANA Yesu, “Ukiweza Neno Lolote, Utuhurumie Na Utusaidie” (Marko 9:22)
Na Yesu Hakuanza Kumwambia Maneno Yaliyojaa AKILI ZA KIBINADAMU NA THEOLOJIA Bali Alizungumza Kwa UHAKIKA, Tena Kwa Mshangao, “Ukiweza! YOTE Yawezekana Kwake Aaminiye” (Marko 9:23)
Yesu Alikuwa Anamaanisha, “HAKUNA JAMBO LOLOTE AMBALO MTU WA IMANI HAWEZI KUFANYA; YOTE YANAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE”

Miaka 2 Iliyopita, Nikiwa Semina Huko Kahama, Mama Mmoja Alinikaribisha Kwake, Akanikaribisha Chakula; Nilipomaliza Kula Aliniambia, “Mtumishi, Nina Mwanangu Hapa, Ana Umri wa Miaka 11 Sasa, Yuko Darasa La 3, Ila Hata Uko Amefika Kwa Sababu Ya Umri, Walimu Waliamua Kumsogeza tu, Maana HAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA… Hata Wadogo Zake Wenye Miaka 7, 9 Wanajua Kusoma Sana Na Kuandika, Ila Yeye Kwakweli Hawezi Chochote, NISAIDIE MTUMISHI WA MUNGU” Yule Mama Alisema Yale Maneno Kwa Huruma Sana, Halafu Akaendelea, ” Pia Tangu Utoto Wake, Huyu Mwanangu Ana Matatizo Ya Ugonjwa Wa Kubana Kifua [Asthma], Amekuwa Akiteseka Sana, Mtumishi Kwakweli Tunateseka Naye”

Nikamwambia Yeye Na Mwanae Waje Pale; Nikamwamuuliza Unataka Nini Hasa Mama? Akajibu, “Nataka Yesu Anisaidie, Amponye Mwanangu Na Aanze Kuelewa Kusoma Na Kuandika”

Nikaweka Mikono Juu Yao, Kisha Nikayalaani Yale MATESO NA ROHO YA UJINGA Inayozuia Yule Mtoto Asisome… Kisha Nikamwambia, “AMINI TU; IMEKUWA”

Kesho Yake Alinipigia Simu Akishangilia, “Mtumishi, Kifua Kimeacha, Ni Mzima Kabisa… Lakini Nashangaa Zaidi; Nimemkuta ANASOMA Kitabu Cha Hadithi Ya Simba Na Sungura, Na Amesoma Kila Kitu, Anaandika Pia…”

Tangu Wakati Huo Hadi Leo, Imekuwa Amani Na Furaha Kwao…

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: