UNAITUMIAJE HELA INAYOPITA MKONONI MWAKO? INAWEZA KUKUFANYA UWE TAJIRI AU MASIKINI

https://i1.wp.com/allwomenstalk.com/wp-content/uploads/2010/01/10-tips-for-smart-budget-planning/Write-down-ALL-expenses_tips-smart-budget-planning.jpg

Watu Wengi Hawajui Ni Namna Gani Watakuja Kuwa Na Maisha Safi Na Ya Kuridhisha Kwenye Eneo La Fedha Na Uchumi Kwa Sababu HAWAJALI NA HAWAZINGATII Namna Na Jinsi Wanavyotumia Pesa Inayopita Mkononi Mwao… Wengine Wana Mishahara Au Vitega Uchumi Vinawaingizia Zaidi Ya Milioni Moja Ya Kitanzania Kwa Mwezi Lakini Wana Miaka Zaidi Ya Mitano Wanaishi Kwenye Nyumba Ya Kupanga, Wana Madeni Usiombe… Lakini Kuna Wengine Wanapata Mshahara au Faida Ya Shilingi Laki 2 Na Ndani Ya Miaka 2 Au 3 Tayari Amejenga, Ameweka Vema Mambo Ya Nyumbani Kwake, Anasomesha nk… Swala Hapa Si Kiasi Gani Unaingiza Mwisho Wa Mwezi, Swala Ni Kwa Kiasi Gani UNAIELEWA FEDHA NA KUITHAMINI NA PIA NAMNA UNAVYOITUMIA… Kama Hauwezi Kupanga Bajeti Yako Kwa Shilingi 10,000/= Iliyo Mkononi Mwako Kwa Kigezo Kwamba Ni HELA KIDOGO TU YA SODA… Hautaweza Kufanya Makubwa Na Shilingi Milioni Moja… Kama Akili Yako Haijawa Na Akili Kwenye Eneo La Pesa, Hata Kama Mungu Angehamishia Mapesa Ya BOT Kwenye Kabati Za Chumbani Kwako, Baada Ya Miaka 5 Tu Utakuwa Masikini Mzuri Kama Ulivyo Sasa!

1.UNAJUA KIASI GANI CHA PESA UNATUMIA KWA SIKU?

Kwa Siku Moja Unatumia Kiasi Gani Kwa Ajili Ya Chakula, Na Vitu Vidogo Vya Kulakula? Watu Wengi Wanapenda KULAKULA; Siwezi Kuwalaumu Maana Hata Akina Adamu Na Mkewe Walishindwa Kwa Kuendekeza TUMBO, Na Nyie WAJUKUU ZAO Mnafeli Pia Katika Hili Eneo… Mnapenda Kula, Mnatumia Kiasi Kikubwa Cha Pesa Hapa Isivyostahili… SIWAKATAZI MSILE, LA HASHA! Nawakumbusha Kupunguza Matumizi Makubwa Mliyonayo Kwenye Eneo La Chakula… Kwanini Ule Steers Chakula Cha Sh 10,000/= Wakati Unaweza Kukipata KWINGINE Kwa Sh 4,000/=? Kwanini Ule Chakula Cha Sh 5,000/= Mgahawani Wakati Ungekipika Mwenyewe Nyumbani Kwa Gharama Ya Muda Wako Na Sh 2,000/= tena kwa Usafi, Usalama Na Ubora zaidi?

Unatumia Pesa Kiasi Gani Kwa Siku Kwa Ajili Ya Simu Yako? Wengine Mna Line 2 Ama 3, Mmewahi Kujifanyia UKAGUZI MKAONA KIASI GANI MNATUMIA KWA WIKI AU MWEZI KWENYE GHARAMA ZA SIMU YA MKONONI? Kuna Watu Wanaunga VIFURUSHI Kila Siku, Hujaweka Kupiga Ikitokea Namba Mpya Imebip, Au Kupiga Kwa Yule Anayedai ANAMPENDA SANA [Hata Mara 5 kwa Siku]… Kwa Siku Ni Hela Nyingi Sana Mnawakusanyia Voda, Tigo, Airtel, Zantel Na Wengineo… Tena Kwa Kuwafanya Msishituke Wamewawekea AKAUNTI ZENU Za M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money nk Kwenye Simu Zenu; Salio Au Kifurushi Kikiisha Haraka Sana MNAZAMA *150*XX# Haraka Sana… Tujiulize Kwa Pamoja, Je Kiasi Cha Pesa Unayotumia Kwa Siku Kwenye Simu Ni Sawa Na Kiasi Cha Pesa Unachoingiza Kwa Simu Hiyo? Wengi Wanatumia Simu Kwa Ajili Ya Kufanya Tu PUMBA PUMBA TU, Hakuna Cha Maana… Wengine Ni Wanafunzi, Wanategemea Kwa Wazazi, Wanapiga Mizinga Kwa Kaka Na Dada, Lakini Nao Utawakuta Wako Kwenye CHATI ZA JUU ZA MATUMIZI YA SIMU!

Kama Hauwezi Kuijali Shilingi 100, 200 Au 500 Inayopita Mkononi Mwako, Anza Mapema Kujitoa Kwenye LIST Ya Matajiri Na Watakaofanikiwa Kifedha!
Kwa Taarifa Yako; Milioni 1 Ni Sawa Na Hizo Mia Mia 10,000… Milioni 1 Ni Sawa Na Hizo Mia Mbili Unazobeza 5,000… Kwa Taarifa Yako, Milioni Moja Ni Sawa Na Noti 2000 tu Za Mia 5 Usiyoithamini Wewe!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: