YOTE YANAWEZEKANA KWANGU, YANAWEZEKANA KWA WATU WA IMANI, NA KWA WATU WA NYUMBANI KWA MUNGU!

Nayaweza Yote..

Wakati Fulani Unapokuwa Unapanda Ngazi Katika Kumjua Mungu, Kuna Mambo Mengine Haupati Kabisa Faida Yake Au Unapata Kwa Kiwango Kidogo Sana…. Wakati Fulani Nilkuwa Ninaitafakari Luka 1:37 Wakati Malaika Gabrieli Anamwambia Mariamu, “Kwa Mungu Mambo Yote Yanawezekana” … Nami Moyoni Mwangu Ilijengeka Fikra Kuwa “Kwa Mungu” Tu Ndiko Mambo Yote Yanapowezekana, Nikiwa Na Maana Kwamba Ni Mungu Peke Yake Awezaye Kutenda Mambo Yote Au Mwenye Uwezekano Wa Kufanya Lolote… Mimi Nilikuwa Sijihusishi Na Uwezekano Wa Kila Kitu Kwangu, Kwa Vile Mimi Si Mungu…. Kwa hiyo Ningeomba Maombi Kwa Mungu, Nikijua Kwake tu, Ndiko Yanakowezekana!

Lakini Nilipoendelea Kukua Na Kupata Nuru Ya Kweli Za Neno La Mungu, Nimegundua Kuwa, Kila Linalowezekana Kwa Mungu, Linawezekana Na Kwangu Pia… Kila Anachoweza Kutenda Mungu, Nami Naweza Kutenda, Kama Mungu Anaweza Mambo Yote, Nami Naweza Mambo Yote…. Hii Imekuja Kuwa Halisi Kwangu Kwa Sababu Nimemjua Mungu Kama BABA YANGU… Aliyenipa Neema Ya Kuwa MSHIRIKA WA TABIA ZA UUNGU… Yaani Nimepewa DARAJA Ndani Yake Ambako Naweza Kufanya Kila Kitu Awezacho Kufanya… Maana “KAMA YEYE ALIVYO, NDIVYO NA MIMI NILIVYO ULIMWENGUNI HUMU” (1 Yohana 4:17)… Pia Kitu Kikubwa Na Cha Ajabu Alichokuwa Nacho Yesu, Yaani UTUKUFU WA MUNGU, AMENIPA (Yohana 17:21-23)… Ameninunua Kwa Damu Ya Mwanakondoo Aliyechinjwa Ili Niwe Mwakilishi Wake Duniani Na NIMILKI JUU YA NCHI (Ufunuo 5:9-11)… Kubwa Zaidi, Ni Yeye Aliye Hai Ndani Yangu, Hivyo Kila Kitu Anatenda Yeye (Wagalatia 2:20)… Nina Asili Yake; Yeye Ni Mungu, Mimi Ni Mwanae, Ni Muungu Pia, Kazi Zake Kama Baba, Nami Kama Mwana Nazitenda Pasipo Shaka (Zaburi 82:6)

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: