Roho Mtakatifu ni Mtaji kwa wakristu

Roho mtakatifu

Roho Mtakatifu Ndio Ulikuwa Mtaji Wa Yesu Na Huduma Yake Ya Kihistoria Hapa Duniani… Tunasoma, “Habari Za Yesu Wa Nazareth, Jinsi Mungu Alivyompaka Mafuta Kwa ROHO Na Kwa Nguvu; Akazunguka Huku Na Huko Akitenda Kazi Njema Na Kuwaponya Wote Walioonewa Na Ibilisi, Kwa Maana Mungu Alikuwa Pamoja Naye” (Matendo 10:38)… Na Hata Alipotoka Kumtafuta Mungu Kwa Siku 40 Za Kufunga Na Kuomba, Alipoingia Hekaluni Alisema Yafuatayo, “ROHO WA BWANA Yu Juu Yangu, Maana Amenitia Mafuta Kuwahubiri Masikini Habari Njema, Kuwaweka Huru Waliofungwa, Kuwafungua Waliosetwa, Vipofu Wapate Kuona Tena… Kutangaza Mwaka Wa Bwana Uliokubalika” (Luka 4:18-19)… Na Kila Alichofanya Yesu Kilitendwa Na Mungu Mwenyewe Kupitia Roho Mtakatifu!
Wakaja Mitume, Nao Hawakufanya Jambo Lolote Mpaka Baada Ya Kumpokea Roho Mtakatifu (Matendo 2), Petro Aliyekuwa Mwoga Kiasi Cha Kumsaliti Yesu Mbele Ya Kijakazi Akahubiri Injili Yenye Uweza Watu 3000 Wakaokoka Ndani Ya Siku Moja… Sura Ya 3 Ya Matendo Ya Mitume, Petro Tena Akiwa Ameshampata Roho Mtakatifu, Akamwinua Kiwete Aliyezaliwa Hivyo Tangu Tumboni Kwa Mamaye… Sura Ya Tano Ya Matendo Ya Mitume, Roho Mtakatifu Kupitia Kwa Petro Akafichua Kila Kitu Kuhusu Anania Na Safira Na Akawaadhibu Kwa Kumdanganya… Sura Ya Sita Mtu Wa Mungu Stefano Akatenda Mambo Makubwa, Miujiza, Ishara Na Maajabu Kwa Mtaji Huo huo Roho Mtakatifu… Sura Ya Nane, Mtu Wa Mungu Filipo Naye Akafanya Mambo Makubwa Kwenye Huduma, Lakini Mtaji Wake Alikuwa Roho Mtakatifu… Sura Ya Kumi Na Moja, Mtume Paulo, Naye Baada Ya Kujazwa Na Roho Mtakatifu Akaanza Kufanya Mambo Ya Ajabu Sana Kiasi Cha Hata Leso Yake Kuponya Magonjwa Na Kutoa Pepo… Kwa Ujumla Kila Walichofanya Mitume Katika Kitabu Cha Matendo Ya Mitume Na Mwendelezo Wa Kazi Za Roho Mtakatifu… Baadaye Wamekuja Watu Kama Charles Finney, John G Lakey, Andrew Murray, Charles Huddon Spuergeon, Terry Moody, Smith Wigglesworth, A A Allen, Mariah Woodworth Etter, Kathrin Kuhluman, Kenneth Haggin, T.L Osborn, Reinhard Bonke, Billy Graham Ambao Wameleta Mapinduzi Makubwa Lakini Mtaji Wao Ukiwa Ni Roho Mtakatifu… Zama Hizi Kuna Watumishi Wengi Wa Mungu Wanafanya Mambo Ambayo Macho Hayajawahi Kuona Wala Masikio Hayajawahi Kusikia, Lakini Mtaji Ni Ule Ule Roho Mtakatifu!
Habari Njema Ni Kwamba; Hakuna Mtu Maalum Aliyetengwa Katika Siku Hizi Za Mwisho Kutembea Na Kutenda Katika Upako Wa Roho Mtakatifu… Kila Mtu Aliyeokoka, Mwenye Kiu, Njaa Ya Kuziona Na Kuziishi Nguvu Za Mungu Za Siku Za Mwisho Anayo Fursa Ya Kuingia Kwenye Orodha Ya Mapinduzi Ambayo Mungu Amekwisha Yaanzisha Kwa Ajili Ya Siku Hizi Za Mwisho Tulizomo… Kabla Ya Yesu Kurudi Kulichukua Kanisa, Akina Baba, Akina Mama, Vijana Wa Kike Na Kiume, Walio Na Roho Mtakatifu Watakwenda Kuleta Mapinduzi Duniani Ambayo Dunia Haijawahi Kuyaona, Kwenye Maeneo Yote Ya Uchumi, Ubunifu, Teknolojia, Mawasiliano, Huduma, Ugunduzi, Sayansi nk
Mimi Nimeshajiandikisha Katika MTEMBEO HUU WA MWISHO Wa Nguvu Za Mungu Duniani Kupitia Utendaji Usio Na Mipaka Wa Roho Mtakatifu; Unaweza Kupima Ukweli Huo Kwa Kuangalia Umri Wangu Na Yale Ninayowaza, Kufikiri, Mtazamo, Hekima Na Ufahamu Wa Mungu Nilionao… Na Hapo Ni Mwanzo Tu Nimeingia Kwenye Darasa La Roho Mtakatifu, Kuna MAAJABU YANAKUJA!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: