Agano Jipya,Agano lililo bora

Unajua AGANO JIPYA Linaitwa, “AGANO LILILO BORA, LENYE AHADI ZILIZO BORA” Na Agano Jipya Limeanza Kazi Rasmi Yesu Alipoangikwa Msalabani Na Kumwaga DAMU YAKE YA THAMANI… Maana “HAKUNA AGANO PASIPO KUMWAGIKA KWA DAMU”… Na Biblia Yangu Inaiita Damu Ya Yesu Kuwa Ni “DAMU YA AGANO LA MILELE” …. Na Sisi Wakristo, Wale Tulioyatoa Maisha Yetu Kwa Yesu Ili Awe Bwana Na Mwokozi [Achana Na Wale Wakristo Wa Dini], Sisi Tulioiamini Kazi Njema Ya Yesu Msalabani, Na Kununuliwa Kwa Damu Yake Ya Thamani Kwa Njia Ya Imani Kupitia “WOKOVU” Na Kujazwa Na Nguvu Za Roho Wake Mtakatifu, Tumefanywa Kuwa “WARITHI PAMOJA NA KRISTO” Warithio Vya Mungu Pamoja Naye!

Wana Wa Israel, Kupitia Agano La Kale, Walikuwa Na Ahadi Nzuri Sana, Mfano: Mungu Aliwahakikishia Atakibarikia Chakula Chao Na Kinywaji Chao [Hawatakuja Kuwa Na Uhitaji Kwenye Eneo La Kula Yao], Akawaahidi Ataondoa Magonjwa Kati Yao [Ugonjwa, Maradhi Hautakuwa Fungu Lao] Na Pia Akasema Kati Yao Hapatakuwa Na Tasa Wala Mwenye Kuharibu Mimba, Akawahakikishia Kuwabariki Mjini Na Mashambani, Akaahidi Kubariki Kazi Za Mikono Yao, Wanyama Wao, Akawahakikishia Kuwa Baraka Itawafuata Kila Waendapo Na Itawapata [Yaani Wao Hawataifuata Bali Baraka Itawafuata Na Kuwapata], Akawahakikishia Hawatakufa Wakiwa Na Umri Mdogo, Yaani Hesabu Ya Miaka Yao Ataitimiza, Kupitia Kinywa Cha Nabii Isaya Akasema Mtu Atakayekufa Akiwa Mdogo Ni Yule Mwenye Miaka 100, Akawahakikishia Kuishi Na Kuwaona Wana Wa Wana Wao Hata Kizazi Cha Tatu Na Hata Cha Nne, Aliwahakikishia Kuwa Watakuwa Vichwa Na Si Mikia, Watakuwa Juu Tu Na Sio Chini Kabisa, Aliwahakikishia Kuwapa Kibali Na Upendeleo Katika Maeneo Yote, Aliwahakikishia Kuwapa UTISHO MBELE YA MATAIFA MENGINE Nk… LAKINI, Yote Haya Yalitegemeana Na BIDII YAO Katika KUSIKIA SAUTI YA BWANA MUNGU WAO, KUTUNZA NA KUFANYA YOTE AWAAGIZAYO!
Agano Lao Lilikuwa Zuri Sio? Wasingekuwa Wagonjwa, Wasingekuwa Masikini, Wasingekufa Kabla Ya Wakati Na Katika Umri Mdogo, Wangekuwa Baraka Kwenye Maeneo Yote… HILI LILIKUWA AGANO LA KALE, LIKIWA NA AHADI NZURI MNO!

Sisi Tunalo AGANO JIPYA, AGANO LILILO BORA, LENYE AHADI ZILIZO BORA… Tumepata Fursa Ya Mungu Kuwa Baba Yetu Kupitia Kwa Kristo Yesu [Tunayo Nafasi Ya Kupata Chochote Kwa Mungu, Yeye Akiwa Baba Mwenye Kuwajibika Kwetu Watoto Wake Na Familia Yake]… Tumepata Fursa Ya Kupeleka MAOMBI, DUA, SALA Na HOJA Zetu Mbele Zake MOJA KWA MOJA, Bila Kupitia Kwa Kuhani Mkuu Kwa Mlango Ulio Wazi Uliofunguliwa Kupitia DAMU YA KUHANI MKUU WA MILELE, DAMU YA YESU, “Sasa Tunao Ujasiri Wa Kukisogelea Kiti Cha Rehema Kwa Damu Ya Yesu”… Tunazo Funguo Za Ufalme Wa Mungu, Lolote Tutakalolifungua Hapa Duniani [Kwenye Huduma Zetu, Ndoa, Familia, Kazi Na Shughuli Zetu, Koo Na Kabila Zetu Na Taifa] Na Mungu Naye Analifungua… Tunalolifunga Hapa Duniani, Na Mungu Naye Analifunga. Yaani Tumepewa Nafasi Ya KURUHUSU AU KUZUIA CHOCHOTE HAPA DUNIANI… Hii Si Ajabu? Waisrael Hawakuwa Na Nafasi Kama Hii Tuliyonayo, Hawakuwa Na Sauti Kubwa Katika Ulimwengu Wa Roho Kama Tuliyonayo Sisi Sasa… Unajua Mungu Ameturudishia Mamlaka, Utawala Na Nguvu Kuamua LOLOTE Hapa Duniani… Sielewi Ni Kwa Namna Gani Unafaidi Hii Fursa! Mungu Ametupa ASILI YAKE Ndani Yetu, Tunao Ushindi Dhidi Ya DHAMBI, Waisrael Hawakuwa Na Uwezo Wa Kuishinda Dhambi, Kulikuwa Na Adhabu Kali Za Kutisha, Hata Kifo Kwa Watenda Dhambi, Lakini Bado Walitenda Dhambi Tena, Hawakuwa Na NGUVU Ya Kuidhibiti Na Kuishinda Dhambi… Sisi Watu Wa AGANO JIPYA Tunatembea Kwa Ushindi Na Uhakika, YESU ALIIBEBA DHAMBI YETU MWILINI MWAKE… Ameiharibu Na Kuivunja NGUVU YA DHAMBI Kwa Ajili Yetu, Na Ametupatia Huo Ushindi Ndani Yetu Kupitia NGUVU YA ROHO WAKE MTAKATIFU, Anayeendesha Maisha Yake Matakatifu Ndani Yetu… Kila Anayedumu Katika Ushirika Na ROHO MTAKATIFU [Kupitia Maombi, Neno La Mungu] Anao Ushindi Dhidi Ya Kila Namna Ya Dhambi, Na Ndani Yake DHAMBI Si Changamoto Tena Maana Amepoteza RADHA YAKE… Je Hili Si AGANO LILILO BORA? Watu Wa AGANO JIPYA Tumepewa Nafasi Ya Kuwa WASHIRIKA WA TABIA ZA KIUNGU… Tumepewa Fursa Ya Kuwa Na Aina Ya Uzima Ulio Ndani Ya Mungu; Watu Wa Agano Jipya Tunao UZIMA WA MILELE NDANI YETU… Sisi Ni Wa Milele Kama Alivyo Mungu Wetu, Kwetu Kifo Sio Mwisho, Tunalo TUMAINI, Tunayo MAISHA YASIYOZIMWA Na NGUVU YA KABURI Kama Alivyokuwa Yesu Mwenyewe… Maana Yeye Amwaminiye Kristo Yesu HATAKUFA KAMWE, Na AJAPOKUFA ATAKUWA ANAISHI… Kwetu KIFO Ni Mlango Wa Kuwa Na Baba Milele… Kwetu “Kuishi Ni Kwa Ajili Ya Kristo Na Kufa Ni Faida” … Tunao Uhakika Na Maisha Katika Hali Zote, TUWE HAI AU TUMBONI MWA KABURI Huo Si Mwisho Kwetu Sisi… UZIMA WA MUNGU, UZIMA WA MILELE Unakaa Ndani Yetu… Je Hili Si Agano Lililo Bora?

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: