…Bali sisi tunalitaja jina la Bwana

https://yesunibwana.files.wordpress.com/2013/02/david-and-goliath-2.jpg?w=225

Ukisoma 1Samweli 16 Utazikuta Habari Za Mshindi Aitwaye Daudi Na JITU Alilolishinda Liitwalo Goliath… Kwa Kuwaweka Kwenye Mzani, Daudi “HATA KWA DAWA” Asingeweza Kumwangusha Goliath… Goliath Alikuwa Mtu Wa Vita Tangu Ujana Wake [Alikuwa Na Uzoefu Wa Kutosha]… Daudi Alikuwa Mchunga Kondoo Tu; Huenda Hakuwahi Hata Kupigana Na Wachungaji Wenzie Kule Malishoni… Goliath Alikuwa Mtu Mzima Tena JITU (Giant), Na Alizijua PROPAGANDA Za Uwanja Wa Vita:Alikuwa Na Maneno Ambayo Yanamfanya Adui Ashindwe Hata Kabla Hajapigana [Kwa Maneno Yale Aliweza Kuwanyamazisha Waisrael Kwa Siku 40]… Daudi Alikuwa Kijana Mdogo, Mwekundu Na Mzuri Wa Sura, Hata Matusi Yalikuwa Magumu Kuyasema Kwa Kinywa Chake, Ndiyo Maana Alipomsikia Goliath Akitukana ALIUMIA!
Kwa Hali Yoyote Ile, Daudi Asingeweza Kumshinda Goliath, Hakukuwa Na MZANIA Kati Yao… Kwa Ripoti Ya Milango 5 Ya Fahamu, Daudi Alishashindwa!
Lakini Daudi Alijua Siri Ya Ushindi, Alijua Namna Ya Kufidia Na Kuziba PENGO Kati Yao… Daudi Hakujipima Yeye Na Jitu Goliath, Bali Aliliweka Jitu Kwenye Mzani Na MUNGU ALIYE HAI, ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI… Ndio Maana Wakati Goliath ANALAANI NA KUTUKANA; Yeye Daudi Alisema, “Mungu Atakutia Mikononi Mwangu, Nami Nitakupiga Na Kukuua”
Mara Zote Unapolipima JITU (Jaribu Lako, Tatizo Lako, Changamoto Yako, Ugumu Unaopitia) Na Mungu, Unauona Ushindi Pale Ambapo Watu Wote Wanaona Na Kutangaza Kushindwa Kwako!
JITU DAWA YAKE MUNGU… “Wewe Unanijia Na Panga, Na Fumo Na Mkuki, Bali Mimi Nakujia Kwa Jina La BWANA, Mungu Wa Majeshi Ya Israeli Uliowatukana”
“Hawa Wanataja Magari, Wale Wanataja Farasi, Bali Sisi Tutalitaja Jina La BWANA, Mungu Aliyeziumba Mbingu Na Nchi”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: