Je Unaumwa?

yesu mwokozi wetu

JE UNAUMWA AU KUNA NDUGU YAKO ANAUMWA NA YUKO KARIBU NAWE? NENDA PALE ALIPO NA USOME UJUMBE HUU PAMOJA NAYE, NA YESU ATAMPONYA HAPO HAPO!
Umeokolewa Kwa Imani, Kwa Kumwamini Yesu Na Kazi Yake Njema Msalabani, Si Kwa Juhudi Yako Au Tendo Lako Lolote Jema (Waefeso 2:8-9)… Na Baada Ya Kuokoka, Mungu Ameweka Mfumo Wa Maisha Unaopaswa Kuenenda Nao Ama Kuuishi, Na Mfumo Huo Unaitwa “KUISHI KWA IMANI” Maana Imeandikwa, “Mwenye Haki Wangu ATAISHI KWA IMANI; Naye AKISITA SITA, Roho Yangu Haina Furaha Naye” (Waebrania 10:38)…
Kuishi Kwa Imani Ni Nini?
Kuishi Kwa Imani Ni Kuishi Kwa Ripoti Ya Kile Neno La Mungu Limesema, Bila Kujali Hali Ya Mazingira Yanayokuzunguka Ikoje. Kuishi Kwa Imani Ni Kuyaendesha Maisha Yako Bila Kujali Milango Mitano Ya Fahamu Inasemaje. Ni Kuishi Kwa Kuzingatia, Kuamini Na Kukiri Kile Ambacho Mungu Amesema Kwenye Neno Lake Hata Kama Macho Yako Hayakubaliani Na Hilo Au Yanaona Mengine… Ni Kuishi Kwa Kukubaliana Na Kile Ambacho Mungu Amesema Hata Kama Masikio Yako Yanasikia Taarifa Tofauti Toka Kwa Wataalamu, Wanasayansi, Wachumi, Watawala Au Wajuzi Wa Dunia Hii… Ni Kuishi Kwa Kanuni Hii, “MAADAMU BIBLIA IMESEMA; BASI HIYO NI KWELI”
Kuishi Kwa Imani Ni Kufungia Nje Kila Wazo Au Fikra Iliyo Tofauti Na Neno La Mungu… Kama Haujafikia Hatua Ambayo Lolote Lisilo Sawa Na Neno La Mungu Kutokuwa Sehemu Ya Maisha Yako, Bado Haujawa Mtu Wa Imani… Mtu Wa Imani Ni Yule Anaye Yaendesha Maisha Yake Kwa Kutegemea Chanzo Kimoja Tu Cha Taarifa; NENO LA MUNGU!
Kama Haujafikia Mahali Pa Kupanga, Kuamua, Kuendesha Maisha Yako Sawa Na Kile Neno La Mungu Limesema, Bado Haujawa Mtu Wa Imani!

Kwenye Kitabu Cha Hesabu Sura 13 Na 14, Tunamwona Musa Anawatuma Wapelelezi 12 Kuipeleleza Nchi Ya Ahadi Na Kati Ya Hao, Wapelelezi 10 Wanarudi Na Ripoti ‘YA KILE AMBACHO MACHO YAMEONA, MASIKIO YAMESIKIA, HISIA ZAO ZIMEWAAMBIA Nk” Hawa Wapelelezi 10 Walikuja Na Ripoti Ya ‘HALI HALISI YA MAMBO’ Na Kwakweli Hawakusema ‘UONGO’ Maana Waliyosema Ndiyo Yaliyokuwa Huko, Waliyosema Ndio Waliyoyaona, Waliyosema Ndiyo Waliyasikia Na Ndiyo Waliyoyahisi Kwa Hisia Zao… Halafu Wapelelezi Wawili, Joshua Na Kalebu Wakaja Na Ripoti Nao Mbele Ya Musa Na Israeli… Ripoti Yao Ilisema, “YOTE WALIYOSEMA WENZETU 10 NI SAWA KABISA, MAANA HAYO NDIYO MACHO YAMEONA, HAYO NDO MASIKIO YAMESIKIA, HAYO NDO TUMEHISI KWA HISIA ZETU, HIYO NDO RIPOTI YA MILANGO MITANO YA FAHAMU, HUO NDO UKWELI WA WAKATI HUU, ILA SI UKWELI WA MILELE, UKWELI WA MILELE, YAANI RIPOTI YA MUNGU INASEMA TUTAWAONDOSHA HAO ADUI ZETU NA KUIRITHI NCHI YA AHADI… SISI HATUANGALII NINI TUMEONA AU KUSIKIA, BALI TUNAKIAMINI KILE MUNGU AMESEMA, KILE MUNGU ALIMWAMBIA IBRAHIMU HATA KABLA HATUJAJA MISRI, KILE MUNGU ALITWAMBIA HATA KABLA FARAO HAJATUPA RUHUSA TUONDOKE MISRI… TUNASHIKAMANA NA RIPOTI YA MUNGU ALIYEFANYA NJIA KATIKATI YA BAHARI YA SHAMU NA KUWAZIKA ADUI ZETU HUMO… TUNAIAMINI RIPOTI YA MUNGU ALIYETULISHA KWA MANA NA KWARE JANGWANI… TUNAIAMINI RIPOTI YA MUNGU ALIYETUPA MAJI TOKA KWENYE MWAMBA…. TUNAIAMINI RIPOTI YA MUNGU ALIYETULINDA KWA WINGU MCHANA NA NGUZO YA MOTO USIKU… MUNGU HUYO HUYO ATAWAFANYA HAWA WANEFILI WAWE CHAKULA CHETU… ATATUPA HIYO NCHI NASI TUTAIMILIKI”
Sawa Sawa Na UKIRI WAO, Sawa Sawa Na Kutoangalia Kwao Ripoti Ya Milango Mitano Ya Fahamu, Joshua Na Kalebu Ndio Watu Wazima Pekee Walioweza Kuingia Kwenye Nchi Ya Ahadi, Nchi Ya Maziwa Na Asali!

Kama Una Nia Ya Dhati Ya Kuuona Mkono Wa Mungu Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako, Ni Lazima Ukubali KUIKANA Ripoti Ya Kile Unachoona, Kile Unachosikia Au Kuhisi Kama Kiko Kinyume Na Neno La Mungu!
Hautaingia KANANI Yako Kama Utaikubali Ripoti Ya Milango Mitano Ya Fahamu… Hautayafurahia Maziwa Na Asali, Hautamilki Na Kutawala, Hautastawi Na Kuwa Mtu Mkuu Ambaye Mungu Alikukusudia!

Kama Ni Mgonjwa, Na Umeambiwa Una Ugonjwa Fulani Na Daktari Au Mtaalamu Wa Afya; Hiyo Ni Ripoti Ya Milango Mitano Ya Fahamu… Hicho Ndicho Alichoona Kwa Macho Yake, Alichohisi Kwa Hisia Zake Na Kusema Kwa Mdomo Wake… Huyo Daktari Ni Mwanadamu, Amekupa UKWELI WAKE Ila Hajakupa UKWELI WA MUNGU NA NENO LAKE… Ukweli Wa Mungu Na Neno Lake Unasema, “YESU ALICHUKUA MAGONJWA YAKO NA UDHAIFU WAKO WA KILA NAMNA” (Mathayo 8:16-17) Na Kama Aliyachukua, Kwanini Ukubaliane Na Daktari Na Kuyabeba Tena? Kwanini Ukubaliane Na Hisia Za Maumivu Ya Mwili Wako Na Kuyachukua Tena Hayo Magonjwa Ambayo Yesu Aliyachukua Tayari Kwa Ajili Yako Miaka Zaidi Ya 2000 Iliyopita? Mungu Si Mtu Aseme Uongo, Neno Lake Linasema “YESU ALICHUKUA DHAMBI ZAKO MWILINI MWAKE, NA KWA KUPIGWA KWAKE, WEWE ULIPONYWA” (1 Petro 2:24)… Kwanini Ukubali Kuwa Mgonjwa Wakati Unaamini Mungu Alikusamehe Dhambi, Makosa Na Uovu Wako? Kama Unaamini Mungu Alikusamehe Dhambi Na Uovu Wako, Amini Tena Kuwa Na Magonjwa Yako Aliyalipia Gharama Kwa Damu Ileile Alipopigwa Kwa Ajili Yako. Maana Imeandikwa, “Akusamehe Maovu Yako, Akuponya Magonjwa Yako Yote” (Zaburi 103:3)
Je Umeambiwa Kwamba Ni Mgonjwa Hospitalini? Je Daktari Amekwambia Ugonjwa Wako Hauna Dawa? Na Wewe Umekata Tamaa Na Umechoka Na Unasubiria Kifo Kwa Huzuni? Hii Ni Habari Njema Kwako, Yesu Anataka Kukuponya Sasa Hivi, Nimesema Mungu Anataka Kukuponya Sasa Hivi, Je Uko Tayari Kuwa Mzima? Je Uko Tayari Kutoka Kwenye Hayo Maumivu Na Mateso Sasa? Kama Unaamini Kuwa Yesu Anaweza Kukusaidia, Nataka Uamini Sasa, Maana Ni Haki Yako Kuwa Mzima Sasa… Yesu Alishayachukua Magonjwa Yako Yote… Kumbuka; Hakuna Ugonjwa Yesu Asioweza Kuponya… Hakuna Maradhi Ambayo Yesu Hawezi Kutibu… Yeye Alilipa Gharama Ya Afya Yako, Na Saa Hii Yuko Hapo Kukusaidia Na Kukuponya… Roho Wake Mtakatifu Yuko Hapo Ulipo Kukutoa Kwenye Mateso Yako… Je Uko Tayari Kuwa Mzima? Je Tayari Imani Yako Imepanda? Je Tayari Uko Tayari Kuwa Mzima Sasa Hivi? Inatosha Yesu Yuko Hapo Kuiponya Damu Yako, Kuganga Mifupa Yako, Kuponya Macho Yako, Kukutoa Hapo Ulipo Bila Msaada… Sasa Omba Maombi Haya Mafupi Ya Imani, Na Mara Umalizapo Kuomba, Tayari Umepokea Uzima wako, ” Bwana Yesu, Asante Kwa Upendo Wako, Asante Kwa Kujitoa Msalabani Kwa Ajili Yangu, Asante Kwa Kuchukua Dhambi Yangu, Magonjwa Yangu Na Umasikini Wangu… Saa Hii Naupokea Uzima Wangu, Napokea Nguvu Ya Afya Toka Kwako, Kuanzia Utosi Wa Kichwa Changu Hadi Unyayo Wangu Napokea Afya Na Uzima Wako Sasa, Damu Yako Ya Thamani Initakase Kila Eneo La Mwili Wangu, Katika Jina La Yesu Wa Nazareth, Amen”
Tayari Umeponywa; Jaribu Kufanya Kile Ulichokuwa Huwezi Kufanya, Kama Ulikuwa Kitandani, Inuka… Kama Ulikuwa Huwezi Kutembea Bila Msaada, Simama Na Utembee, Kama Ulikuwa Huwezi Kuona, Fumbua Macho Na Uone Tena, Kama Ulikuwa Unapumua Kwa Vifaa Maalumu, Vitoe Na Upumue Kwa Pua Zako, Kama Ulikuwa Unateswa Na Nguvu Za Giza, Tayari Zimekuachia… Umekuwa Mzima sasa, Utukufu Kwa Yesu!

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in sala

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: