Kujua yale yaliyo yako

Ayubu

Hakuna Kitu Kibaya Kama Kutojua Yale Yaliyo Yako, Yale Uliyonayo… Ukisoma Kwenye Kitabu Cha Ayubu, Shetani Analalamika Mbele Za Mungu Anasema, “UMEMZINGIRA AYUBU NA NYUMBA YAKE NZIMA KWA WIGO WA MOTO, UMEMBARIKI NA KUMUONGEZA YEYE NA KILA ALIFANYALO” … Lakini Ayubu Hakujua Kuwa Kuna Kitu Kama Hicho, Yeye Aliishia Kusema, “LILE NILICHALO NDILO UNIPATA, LILE LINITIALO HOFU UNIJIA” … Shetani Alijua Jinsi ULINZI, BARAKA, USTAWI Vimeachiwa Kwa Ayubu Na Nyumba Yake… Alijua Ni Kwa Kiasi Gani Amejaribu KUIBA, KUCHINJA NA KUHARIBU Lakini Akaishia Kukutana Na Wigo Wa Moto… Hivi Ndivyo Ilivyo Hata Kwa Wakristo Wengi,

Wao Wanayatazama Maisha Yao Kwa Vile Macho Yao Yanachoona, Wanajiona Ni Masikini, Wahitaji, Wasiojiweza Na Wanakiri Namna Hiyo, Wanatangaza Ukata Na Ugumu Walionao… Lakini Shetani Akiangalia Kwenye Ulimwengu Wa Roho [Yale Yasiyoonekana Kwa Macho] Anaona Jinsi Mungu Alivyowabariki Na Kuwastawisha. Anaona Baraka Zao Walizokwisha Kubarikiwa Na Zile Zitakazowajia Kesho, Wiki Hii, Mwezi Huu, Mwaka Huu, Miaka 5 Ijayo, Miaka 10 Ijayo Nk… Lakini Kwa Vile Ambavyo Wakristo MMEKAZANA Kumlaumu Na Kumlalamikia Mungu, Na Kukiri Unyonge Na Udhaifu Wenu [Kwa Kuangalia Mazingira Yenu] Shetani Anapata Nafasi Ya KUIBA Vya Kwenu, ANAHARIBU Vya Kwenu, ANACHINJA Maisha Yenu Na Ya Wale Muwapendao… Maana MNAMPATIA NAFASI, MNAMFUNGULIA MLANGO Kwa MANENO YENU NA MAWAZO YENU HASI NA YA KUSHINDWA… Ayubu Hakujua Yaliyokuwa Sirini, Hakujua Kuwa Kuna Baraka Zinaachiwa Juu Yake Na Nyumba Yake, Lakini Aliweza Kuzihifadhi Baraka Na Mafanikio Yake Kwa KUTOMLAUMU MUNGU WALA KUMUWAZIA MUNGU KWA UPUMBAVU… UJINGA WAKO NDIO UNAOKUMALIZA Rafiki!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: