Ushindi juu ya Dhambi

Yesu Msalabani

Kama Kuna Dhambi Umejaribu KUIACHA Au KUISHINDA Lakini Juhudi Zako Zote Zimegonga Mwamba… Leo Nataka Nikusaidie Mambo Gani Utafanya Ili Uwe Na Ushindi Dhidi Ya Dhambi Na Ufurahie Maisha Matakatifu;

1.Kubali Kuwa Huwezi Kuishinda Hiyo Dhambi Kwa Juhudi Na Mbinu Zako (Kubali Kuwa Ujanja Wako Umeishia Mfukoni Tayari, Kubali Kuwa Mbio Zako Za Sakafuni Zimefikia Ukingoni)

2.Kubali Kuwa Unahitaji Msaada Wa Mungu Mwenyewe Kwenye Hiyo Dhambi Yako: Pale Tunapokubali UDHAIFU WETU Ndipo Mungu Huanzia Kutuvika UWEZA NA NGUVU ZAKE.

3.Hesabu Gharama: Je Kweli Uko Tayari Kulipa Gharama Ya Kuipoteza Hiyo Dhambi, Watu Waliokuwa Wakishirikiana Na Wewe Katika Dhambi Husika [Marafiki Wabaya, Waliokuwa Wakikusogeza Dhambini], Uko Tayari Hata Kubaki Peke Yako Bila Hao Watu Kama Ni Njia Ya Wewe Kutoka Katika Hiyo Dhambi? Fikiria Mwenyewe, Yesu Alisema, “Yeyote Ampendaye Kaka, Dada, Mama, Baba, Rafiki, Ndugu Kuliko Mimi, Huyo Hanifai Na Hafai Katika Ufalme Wa Mungu”

4.Tubu Na Kuacha
Biblia Inasema, “Afichaye Dhambi Yake Hatafanikiwa, Bali Aziungamaye Na Kuziacha, Atapata Rehema” Kama Umekubali Kuitelekeza Hiyo Dhambi, Na Umeamua Kuwa Na Maisha Matakatifu, Unahitaji Msamaha Wa Mungu Kwenye Dhambi Husika… Kwa Maneno Yako Mwenyewe, Kwa Imani Pasipo Mashaka, Mwombe Mungu AKUSAMEHE [Maana Mungu Yuko Hapo Ulipo Na Anasikia Ukimwomba]
5.Omba Nguvu Ya Mungu Kukusaidia
Kumbuka Hauwezi Kuishinda Dhambi Kwa AKILI NA MBINU ZA KIBINADAMU… Maana Dhambi Ni Kitu Cha Rohoni, Kinaondolewa Na NGUVU ZA ROHONI… Mwombe Mungu Kwa Dhati Ya Moyo Wako Ya Kuwa Akupe Nguvu Ya Roho Wake, Nguvu Ya Utakatifu Ya Kumpendeza Na Kumuishia Yeye (Haya Yawe Maombi Yako Ya Mara Kwa Mara Kila Upatapo Muda Wa Kuomba… Baada Ya Muda Utashangaa Kiu Na Njaa Ya Kuipenda Ile Dhambi IMEKUFA NDANI YAKO)

6.Jisamehe
Kwa Kuwa Umemwomba Mungu Toba, Umemwomba Akusamehe Dhambi Yako, Basi Na Wewe Jisamehe, Maana Tayari Mungu Amekusamehe Tayari, Kwanini Wewe Uendelee Kujihukumu Na Kujishutumu Ndani Yako Kwa Kitu Ambacho Mungu HAKIKUMBUKI TENA (Isaya 43:25, Isaya 1:18)


7.Badili Mwenendo Wako
Dhambi Nyingi Kwenye Maisha Yetu Zinatokana Na Milango Mikuu Miwili; MACHO NA MASIKIO YETU…. Kama Ukiamua Kubadilika, Kubali Kuacha Yale Mambo Yaliyokuwa Yakiingia MACHONI Pako Na MASIKIONI Mwako Na Kukufanya UWAZE NA KUJENGA FIKRA ZA KUTENDA DHAMBI… Kama Ni MAJARIDA, MAGAZETI, MOVIES, VIPINDI FULANI VYA REDIO AU TV… Lipa Gharama Ya Kuviacha, Achana Navyo, Si Chakula Kwamba Usipokula Utakufa! Kama Unaona Ni Changamoto Kwako Kuacha, Anza Maombi Maalum Ya Kuomba Msaada Na Nguvu Ya Mungu Kukusaidia Katika Eneo Hilo… Kama Kuna Rafiki Au Mtu Unayemwamini Ya Kuwa Amekomaa Katika Kumjua Mungu, Mshirikishe Na Muanze Kuombea Hiyo Tabia, Baada Ya Muda Utakuwa Umefunguka Kabisa Na Hautakuwa Na Kiu Wala Njaa Ya Kitu Hicho!

8.Kuwa Rafiki Wa Biblia
Pata Muda Wa Kujisomea Biblia Yako… Ndani Yake Limo Neno La Mungu, Na Neno La Mungu Lina Nguvu Ya Kukufanya Kuwa Mtakatifu Na Kukutenga Na Dhambi… Neno La Mungu Litakuonesha Nini Cha Kufanya Na Kipi Usifanye… Litakusaidia Kuyafanya Mapenzi Ya Mungu!
Hakikisha Walau Kwa Siku Unasoma Walau Sura Moja/ Mlango Wa Biblia Yako… Usikubali Siku Iishe Bila Wewe Kusoma Kitu Kipya Kwenye Biblia Yako… Neno La Mungu Ni Uzima Wako!

9.Mahali Pa Maombi
Pata Muda Wa Kuomba Juu Ya Maisha Yako, Familia, Kanisa, Taifa, Kazi Na Shughuli Zako… Unapojizoeza Kukaa Na Mungu Kwenye Maombi, Tabia Zako Zinaanza Kubadilika Kuwa Kama Yeye, Utukufu Wake Unaanza Kukubadili Na Kukufanya Bora!

Kama Ukizingatia Yote Niliyokutajia Hapo Juu, Na Kuyatenda, Nakuhakikishia DHAMBI Haitakuwa BINGWA KWAKO…. Utaishinda Na Kuitiisha Chini Yako!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
5 comments on “Ushindi juu ya Dhambi
  1. ERICK ERNEST says:

    MUNGU AKUBARIKI SANA MTUMISHI KWA NENO HILO ZURI NA TAMU,KWANI NIMEBARIKIWA SANA!MUNGU AKUONGEZEE MAFUNUO MAPYA SIKU ZOTE.AMINA!

  2. underson mwasikundima says:

    hakika ni mafunzo ambayo yananijenga ktk imani ya kuendelea kumfuata kristo,najihisi ni mtu mwenye furaha kila mara napo soma mambo mbalimbali ktk page hii.MUNGU AENDELEE KUWAPA UFUNUO WA KUTUFUNDISHA YALE YANAYO TULENGA KTK TABIA AMBAYO HAIMPENDEZI MUNGU BABA.

  3. Asante sana mtumishi says:

    Nashukuru

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: