Nguvu ya Mungu

image

Nguvu ya Umeme

Unajua, Watu Waliishi Maelfu Ya Miaka Bila Kujua Kuwa Kuna NGUVU YA UMEME… Hata Walipougundua, Matumizi Hayakuwa Makubwa Kama Ilivyo Sasa… Lakini Baada Ya Muda Watu Waliuzoea Umeme, Na Kuanza Kuutumia Kwa Manufaa Na Maendeleo Yao… Tangu Siku Ya Pentekoste, NGUVU YA MUNGU, Roho Mtakatifu, Itendayo Kazi Ya KUPONYA MAGONJWA, KUFUNGUA WALIOFUNGWA, KUHARIBU HILA NA UONEVU WA SHETANI, KULETA MIPENYO KWA WANADAMU nk Iliachiliwa Duniani… Hii Ni Nguvu Asili Ya Mungu Mwenyewe, Ni Mungu Mwenyewe Kila Mahali Katika Uweza Wake Na Nguvu Zake Zote… Hii Nguvu Ya Mungu, Uweza Na Utukufu Wa Mungu Unaoweza Kurahisisha Maisha Ya Wanadamu Na Kuuzima Uonevu Wa Shetani Na Jeshi Lake Iko Hapo Ulipo, Hata Kama Huioni Kwa Macho… Imetulia Kama Vile Haipo Hapo Ulipo, Lakini Ukweli Ni Kwamba Nguvu Ya Mungu, Nguvu Ya Roho Mtakatifu Iko Kila Mahali, Muda Huu, Kesho Na Hadi Yesu Atakaporudi… ILA Kama Ulivyo Umeme; Nguvu Ya Mungu Iliyopo Hapo Ulipo Ina Vibebeo/ Visafirishi (Conductors) Vyake, Na Pia Ni Wajibu Wa Mtumiaji Umeme KUWASHA SWICHI Na Chombo Husika Cha Kutumia Umeme Ili Aweze Kuufaidi!

Ndivyo Ilivyo Kwa Nguvu Ya Mungu, Nguvu Ya Roho Mtakatifu, UPAKO Unaovunja Nira, Unaokata Kamba Za Mateso, Mauti Na Maumivu… Upako Unaoponya, Unaowafungua Waliofungwa Na Kusetwa, Upako Unaorahisisha Maisha Na Kuyapa Maana, Nao Una Vibebeo (Conductor) Vya Kuubebea, Upako Unabebwa Na Maarifa Sahihi Ya KWELI ZA NENO LA MUNGU Pamoja Na Mhitaji KUWASHA SWICHI YA IMANI Ili Nguvu Ya Mungu Itembee Na Kutoa Matokeo!
Kama Usipokuwa Na Maarifa Sahihi Ya Neno La Mungu Na Pia Kuwasha Swichi Ya Imani; Hiyo Nguvu Ya Mungu Iliyopo Hapo Ulipo, Iliyokuzunguka, Haiwezi Kuwa Na Matunda Kwako!
Kama Ilivyo Kwa Umeme; Anayejua Matumizi Mengi Ya Umeme, Ndiye Anayefaidi Nishati/ Nguvu Ya Umeme… Anayejua Matumizi Mengi Ya Upako, Na Namna Ya Kuuweka Kazini Ndiye Anayefaidi Matokeo Zaidi Maishani Mwake… NGUVU YA MUNGU IMEKUZUNGUKA, IKO HAPO ULIPO, UNAITUMIAJE? INAYANIFAISHAJE MAISHA YAKO? HII NI CHANGAMOTO KWAKO!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: