HATUA TATU ZA KUKUFIKISHA MBINGUNI (Kwa Kila Ambaye Anataka Kufika Mbinguni).

njia ile ni nyembamba

1.KUIONA NJIA

Biblia Inasema, “NJIA ILE NI NYEMBAMBA, TENA IMESONGWA ILE IENDAYO UZIMANI, NAO WAIONAO NI WACHACHE” (Mathayo 7:14)
Na Kwa Mujibu Wa Neno La Mungu, Yesu Kristo Ndiye NJIA, Mtu Hawezi Kuja Kwa BABA Pasipo Kupitia Kwake (Yohana 14:6).
Kuna Wengi Hawajui Kuwa Yesu Ndiye Hii Njia Nyembamba Iendayo Uzimani… Hawa Akili Zao Zimetiwa GIZA Na Ibilisi (mungu wa dunia hii) Ili Isiwazukie Nuru Ya Wokovu, Wakamwamini Yesu Aliye Utukufu Wa Mungu Na Sura Ya Mungu (2 Wakorintho 4:3-4).
Ndiyo Maana Ni Muhimu Kuhubiri Injili Kwa Kila Kiumbe, Kila Mtu Aisikie Injili Yenye Nguvu Za Roho Mtakatifu, Na Si Maneno Matupu. Injili Yenye Nguvu Za Mungu “NI UWEZA WA MUNGU ULETAO WOKOVU”
Kama Mtu Akiisikia INJILI YA KWELI, Lile Giza La Adui Litaondolewa Katika Fikra Zake Na Atamjua Yesu Aliye Utukufu Na Sura Ya Mungu! Na Kwa Kumjua Yesu Anakuwa Ameijua NJIA!

2.KUJA KWENYE NJIA

Hatua Ya Pili Mara Baada Ya Kujua Kuwa Yesu Ni Njia Kweli Na Uzima Na Ya Kuwa Alikufa Msalabani Kuchukua DHAMBI Na Uovu Wako, Lazima Sasa UKUBALI Ukweli Huu Moyoni Mwako, UAMINI Moyoni Na Kukiri Waziwazi Kwa Kinywa Chako Ili Uweze Kupata Wokovu Na Pia Kuhesabiwa Haki (Warumi 10:9-10).
Tunapomwamini Yesu Na Kazi Ya Msalaba, Tunachukua SHARE YETU Ya UKOMBOZI Toka Msalabani, Na Kuimilki Kisheria.

Wako Watu Wengi Wanaijua Njia [Wametimiza Hatua Ya Kwanza] Lakini Kwa Kweli Hawaja Chukua Hatua Ya KUYATOA Maisha Yao Kwa Yesu, Yaani Kuingia Kwenye Njia, Yaani KUOKOKA!
Watu Wengi Tuliomo Nao Kwenye Madhehebu Na Dini Zetu Ni Watu Ambao Wako Hatua Ya Kwanza. Lakini Lazima Uchukue Hatua Ya Pili, Uingie Kwenye Njia!

3.ANZA KUTEMBEA KWENYE NJIA

Hatua Ya Tatu Mara Baada Ya KUINGIA NJIANI, Ni KUANZA KUTEMBEA Na Kuelekea UZIMANI. Na Hatua Hii Ya Tatu Inahitaji Ujue Wapi Pa Kukanyaga. Safari Njiani Inahitaji Ujue Kuwa Imesongwa. Safari Njiani Inahitaji Ujue Kuwa Ni Nyembamba. Safari Inahitaji Ujue Kuwa WAIPITIAO Ni Wachache. Tena Waliojikana Nafsi Zao, Na Kujitwika Misalaba Yao Na Kumfuata Yesu!
Wanaosafiri Njiani Ni Wale Ambao NENO LA MUNGU NI GONGO LA NA FIMBO YAO KUWAFARIJI.
Wanaopitia Njia Hii Ni Wale Waliokubali WAONGOZWE Na Roho Mtakatifu Maana Yeye Ndiye Aijuaye NJIA VEMA. Ndiye Atakayetuokoa Na Mitego Ya Mwindaji. Ndiye Atakayetuokoa Na Wavu Wa Mwovu.
Wanaopitia Njia Hii Ni Wale Waliokubali KUFUMBA MACHO Yao Dhidi Ya Dunia Na Tamaa Zake. Walio Safarini Njiani Ni Wale Ambao Wamejiweka Wakfu Kwa Mungu Ili Wawe DHABIHU Kwake, Iliyo Hai, Takatifu Na Ya Kupendeza!
Na Wale Ambao Wako Njiani Wamechukua NGAO YA IMANI Ili Waizime Mishale Yote Ya Moto Ya Yule Adui… Walioko Safarini Njiani Ni Wale Ambao Wamevaa DRII YA HAKI Kifuani Mwao; Yaani Watu Ambao Maisha Yao Yote Wameamua KUISHI MAISHA YA HAKI….Ni Wale Ambao Wamekaza Jicho Lao Kwa Yesu, Na Hawaangalii Hali Zao Zikoje Au Wanahisi Nini Ama Wanasikia Nini… KAZA MWENDO RAFIKI; USIKU UMEENDELEA SANA, MCHANA UMEKARIBIA, YAVUE MATENDO YA GIZA NA UIVAE NURU!

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: