UNA PICHA NDANI YAKO? BASI UNA RAMANI YA MAISHA YAKO… WEWE NI MTU MKUU SANA!

.

Usifanye KOSA La Kujilinganisha Na MTU YEYOTE Maishani Mwako. Iwe Ni Kwa Kufanikiwa Au Kwa Kushindwa Kwake!
Thamani Ya Maisha Yako Si Kupata Kile Ambacho Mtu Fulani Amefanikiwa Kupata Kwenye Maisha Yake. Bali Thamani Yako Inategemea PICHA KUBWA YA “WEWE” ULIYONAYO NDANI YAKO. Kama Unajiona Wewe Ni PANZI; Kiwango Cha Thamani Na Heshima Utakachopata Hakiwezi Kuwa Sawa Na Cha Yule Ambaye Akijiangalia Ndani Yake Anajiona TEMBO!
Ila Kumbuka, Hakuna Kitu Kibaya Kama Kuwa Na PICHA YA “WEWE” Ndani Yako Ambayo HUJUI Namna Ya kuifanya Kuwa Halisi!
Kama Una PICHA YA “WEWE” Ndani Yako, Hautafanya Jambo Lolote Kwa Vile Wengine Wanafanya. Hautatembea Kwa Sababu Ndugu, Jamaa, Au Marafiki Zako Wote Wanatembea. Utahakikisha Unafanya Yale Tu Ambayo Yanakusaidia KUIFANYA ILE PICHA YA WEWE NDANI YAKO IWE HALISI!
Watu Wenye PICHA “YAO” Ndani Yao, Wanajizuia, Wana Nidhamu, Hawafanyi Kila Kitu, Wala Hawafanyi Chochote Ili KUMFURAHISHA AU KUMPENDEZA MTU… Wanaifuatilia Tu NJOZI YAO… Hata Ikikawia Wanaingojea… Wanajua Kuwa Kama Mungu Akikupa Neema KUONA JAMBO MOYONI MWAKO Basi Linaweza KUWA HALISI!
Watu Wenye PICHA YAO Ndani Yao, Hawawezi Kukubali Kukatishwa Tamaa Na Hali Yao Ya Sasa. Maana Wanajua KUNA MAHALI PAO PA KWENDA. Wanajua Kuwa Hapo Walipo Si KITUO CHA MWISHO.

Kama Umeweza Kuona PICHA Ya Maisha Yako, Ndani Yako… Hata Kama Una Hali Ngumu Kiasi Gani Sasa, Unaweza kufika Hapo Na Kuyaishi Hayo Maisha, Maana Mungu Hajawahi Kuweka Ndani Ya Moyo Wa Mtu Kitu Asichoweza Kukipata. Mungu Akiweka RAMANI YA JENGO Kwenye Moyo Wa Fundi Ujenzi, Hata Kama Kuna KICHAKA KIKUBWA Kwenye UWANJA, Baada Ya Muda Utalikuta Jengo Limesimama. Ila Kumbuka Linakuwa Limetoka Moyoni Kwa Mjenzi!

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
2 comments on “UNA PICHA NDANI YAKO? BASI UNA RAMANI YA MAISHA YAKO… WEWE NI MTU MKUU SANA!
  1. Alice wilison says:

    God is good

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: