Kwa wanandoa na wale wenye malengo ya kuwa na ndoa siku moja

ndoa

Kama Unataka NDOA YAKO Nayo ISIINGIE Kwenye ORODHA Ya NDOA ZILIZOVUNJIKA… Hakikisha Kwanza Wewe “UMEOLOEWA NA NENO LA MUNGU” Kisha Ndipo Ukamtafute Huyo Mme/ Mke Ambaye Naye “AMEOLEWA NA NENO LA MUNGU” Na Ndipo Mtaweza KUKAA Mpaka Kifo Kiwatenganishe!

MWANAMKE ALIYEOLEWA NA NENO; Anajua Wajibu Wake Wa Kumtii Mmewe Kama KUMTII KRISTO…Hawezi Kufanya Chochote Kwa Mmewe Ambacho Asingeweza Kumfanyia BWANA YESU… Atasamehe 7 mara 70 Kwa Kila Kosa La Mmewe… Hatalipa Baya Kwa Baya, Bali Ataushinda Ubaya Kwa Wema… Atakuwa Kielelezo Ili Hata Wale Wasiookoka Wakimtazama WAVUTWE KWA YESU Kupitia MAISHA YAKE… Atamlinda Mmewe Kwa Maombi Na Kwa Kufanya Kila “JEMA” Ili Mmewe Asichukuliwe Na Kutekwa Na Adui… Atajitahidi Kuishi Sawa Na Viwango Vya Mithali 31… Atakuwa MSAIDIZI WA KWELI Wa Kila Jema Atendalo Mmewe…Atakuwa MFARIJI Wakati Wa Magumu Na RAFIKI Wa Nyakati Zote!

MWANAUME ALIYEOLEWA NA NENO; Atampenda Mkewe Kama “MWILI WAKE MWENYEWE” Hatamtendea Chochote Asichotaka Mwili Wake Utendewe… Atamtunza Mkewe Kwa Kiwango Kilekile Anautunza Mwili Wake Mwenyewe… Hatainua Mkono Wake Kumpiga Mkewe, Ulimi Wake Kumtusi Mkewe, Kumdharau Na Kumshusha Kwa Sababu Ya Mali Au Kiwango Cha Elimu; Maana Haya Yote Yeye Mwenyewe HAWEZI KURUHUSU MWILI WAKE UTENDEWE!
Mwanaume Aliyeolewa Na Neno La Mungu, ATAMPENDA MKEWE KAMA KRISTO ALIVYOLIPENDA KANISA (Hatampenda Mkewe Kwa Vile BORA, ANA ELIMU, NI MAARUFU, ANA KIPATO KIZURI, HAKOSEI Nk) Atampenda Mkewe KATIKA UDHAIFU WAKE Kama Kristo Alivyotupenda Katika DHAMBI NA MAKOSA YETU! Mwanaume Aliyeolewa Na Neno La Mungu ATAJUA NAMNA YA KUISHI NA MKEWE KWA AKILI ILI MAOMBI YAKE YASIZUILIWE… Mwanaume ALIYEOLEWA NA NENO LA MUNGU, Ataishi Kwa Kiwango Cha Neno La Mungu, Na Lazima Atakuwa Baraka Kwa Mkewe!

Kabla Ya Kutaka KUOA/ KUOLEWA Na Mwanadamu, Hakikisha Wewe Mwenyewe “UMEOLEWA NA NENO LA MUNGU”
Wanandoa, Na Vijana Mlioko Nje Mnaotarajia Kuwa Na Ndoa, Acheni UVIVU Wa Kutosoma Neno Na Kutafuta MAARIFA YA NENO LA MUNGU… Kiwango Chako Cha NENO LA MUNGU Ulichotunza NDANI YAKO Kitaamua “UHURU WAKO” Katika Ndoa Na Maisha Yako Kwa Ujumla!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
3 comments on “Kwa wanandoa na wale wenye malengo ya kuwa na ndoa siku moja
  1. ALEX SIMON MKUMBO says:

    Asante sana MUNGU AWABARIKI

  2. Elisha Reuben. says:

    Amina mtumishi ubarikiwe na Bwana Yesu kristo aliye Hai!!!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: