Si sawa kwa mkristo (hasa aliyeokoka) kuwa mgonjwa!

Mungu hakuumba ugonjwa

Wakristo Wengi Wanadhani KUWA WAGONJWA Ni Sehemu Ya MAISHA YAO KAMA WANADAMU, Na Kwa Hili Wako Sawa!
Lakini Tukirudi Kwenye Maana HALISI YA UKRISTO, ULIOZALIWA MSALABANI, MKRISTO HAPASWI KUWA MGONJWA, WALA KUFA KWA UGONJWA WOWOTE ULE!

Baadhi Ya Sababu Ambazo Zinanipa KIBURI Cha Kutokuwa Mgonjwa Tangu Nimemuelewa Yesu Kwa Mapana Yake, Nimeziweka Hapa Chini Ili Zikusaidie Kufikiri Sawasawa;

1.MUNGU HAKUUMBA UGONJWA WOWOTE NA WALA SI MWASISI WA MAGONJWA

Ukisoma Biblia Yako Katika Kitabu Cha Mwanzo Sura Ya 1 Na Ya 2 Habari Za UUMBAJI, HUONI KOKOTE MUNGU ALIUMBA UGONJWA, UDHAIFU, MARADHI, UNYONGE, DHAMBI Nk!
Utaona Mungu Baada Ya Kumaliza Kuumba ALIFANYA TATHMINI YA UUMBAJI WAKE NA KISHA AKASEMA YA KUWA KILA KITU ALICHOKIUMBA “NI CHEMA” (Mwanzo 1:31)
Hivyo Kila Kitu Ambacho HAKINA WEMA NDANI YAKE SI SEHEMU YA UUMBAJI WA MUNGU!

2.KAMA MUNGU ANGEKUWA MUASISI/ MWANZILISHI WA MAGONJWA, HALAFU AKAYAPONYA MWENYEWE, NA KUPITIA YESU, MITUME NA SISI WATUMISHI WA SASA; BASI MUNGU ATAKUWA NA “KIGEUGEU” Au “ANABADILIKA BADILIKA” Yaani “HANA MSIMAMO NA KAULI MOJA”

Mungu Anajitambulisha Kama “MUNGU ATUPONYAYE” (Kutoka 15:26)… Yaani Anasema Yeye Ni Daktari Wetu!
Pia Kupitia Manabii Wa Zamani Pia Aliponya Watu, NAAMANI YULE MKOMA TOKA NCHI YA WASHAMI ALIPONYWA NA NABII ELIYA KWA KUJICHOVYA YORDAN MARA 7 SAWA NA NENO LA NABII ELISHA!
MFALME HEZEKIA NAYE ALIPONYWA JIPU LILILOKUWA LINAELEKEA KUMUUA NA NABII ISAYA MWANA WA AMOZI!
Baada Ya Zama Za Manabii Akaja YESU KRISTO (MUNGU KATIKA MWILI) “AKAZUNGUKA HUKO NA HUKO AKIWAPONYA WOTE WALIOONEWA NA IBILISI KWA KUWA MUNGU ALIKUWA PAMOJA NAYE” (Matendo 10:38)…Ukifuatilia Katika HUDUMA YA YESU DUNIANI, KUMEJAA MIUJIZA YA UPONYAJI MINGI MNO Toka Mathayo Hadi Yohana Mtakatifu!
Kama MAGONJWA YANATOKA KWA MUNGU, ANGEMRUHUSUJE YESU AYAPONYE? KAMA YESU ANGEPONYA MAGONJWA WAKATI MUNGU AMEYARUHUSU NA KUYALETA DUNIANI, ANGEKUWA ANAMPINGA MUNGU!
Wakati Yesu Anataka KURUDI Mbinguni Alikabidhi KIJITI CHA KUYASULUBU MAGONJWA KWA “WAKRISTO” Yaani “SISI WANAFUNZI WAKE” Na Ndio Maana Ukisoma KITABU CHA MATENDO YA MITUME KIMEJAA HABARI NYINGI ZA WATU KUPONYWA MAGONJWA NA UDHAIFU WA MIILI YAO, Kama Ingekuwa MUNGU HATAKI TUWE NA AFYA NJEMA, BASI ASINGEWAACHA NA KUWARUHUSU MITUME WAPONYE MAGONJWA!

3.MAGONJWA YOTE CHANZO CHAKE NI SHETANI NA DHAMBI

Kwakweli Mwanzilishi Wa Kila UGONJWA, MATESO, UDHAIFU NA MARADHI NI SHETANI. Alipata MWANYA Kupitia MLANGO WA DHAMBI NA MAOVU YETU!
Ukisoma Katika Zaburi 103:3 Utaona Kuwa Kati Ya Mambo YANAYOTOKEA Baada Ya Mtu Kusamehewa Dhambi Yake, Pia ANAPONYWA MAGONJWA YAKE YOTE!

Hii Ndiyo Sababu Kubwa Ambayo Ilimfanya Yesu Alipokuwa Hapa Duniani Kuwaambia Wagonjwa Walioletwa Kwake, “JIPE MOYO MWANANGU, DHAMBI YAKO IMESAMEHEWA” Na Kila Alipokuwa Akisamehe Dhambi Yao Na Magonjwa Yao Pia YALIKUWA YAKIPONYWA PAPO KWA PAPO, Maana HATI YA UGONJWA KUMKALIA MTU IMEKAA KWENYE DHAMBI. Na Hiyo Dhambi Inaweza Kuwa Imetendwa Na Mtu Mwenyewe Au Wazazi/ Watangulizi Wake. Ukisoma Yohana Mtakatifu 9 Utaona Kitu Hiki Katika Ule Mstari Wa 2 Ambapo Wanafunzi Walimuuliza Yesu “NI YUPI ALIYETENDA DHAMBI KATI YA HUYU MTU NA WAZAZI WAKE, HADI SHIDA HII IKAMPATA?”
Kumbe Ukichunguza Vema Utajua DHAMBI NI MLANGO WA MAGONJWA… Ndiyo Maana Yesu Alipokuwa Akiponya Watu Alikuwa Akiwaambia, “ANGALIA UMEKUWA MZIMA/ UMEPONYWA ENENDA NA USITENDE DHAMBI TENA” (Yohana 5:14)! Maana Anajua Wakitenda DHAMBI WATAMFUNGULIA IBILISI MLANGO WA KUWEKA MAGONJWA JUU YAO!
Ukisoma Matendo 10:38 Utaona Kuwa Wale Wote YESU ALIOWAPONYA “WALIKUWA WAMEONEWA/ WANAONEWA NA IBILISI”
Lakini Pia Ukisoma Luka 13 Utamwona Mwanamke Aliyekuwa AMEPINDA MGONGO KWA MIAKA 18…Yesu Alisema Yule Mama Alikuwa “AMEFUNGWA NA IBILISI”
Hivyo Ugonjwa Mwilini Mwa Mtu Ni SHAMBULIZI LA SHETANI KWAKE, Na LAZIMA Anakuwa AMEPATA MLANGO SEHEMU Kwenye MATENDO YAKO, MANENO/KAULI NA UKIRI WAKO WA KILA SIKU, MAWAZO NA FIKRA ZAKO Nakadhalika!

Kama MAGONJWA YAMETOKA KWA MUNGU, Au Ni ADHABU YA MUNGU KWETU Kama Wasemavyo Baadhi Ya Wahubiri, Basi MADAKTARI WANAOTIBU WAGONJWA WATAKUWA WANAMTENDA MUNGU DHAMBI… Lakini Sivyo, Mungu Amewapa Madakatari Akili Na Ujuzi Ili WAYADHIBITI MAGONJWA, Na Ndiyo Maana Mtu Akijisikia Vibaya Kiafya, Anakwenda Mwenyewe Mbio Hospitali, Hii Ni KWA SABABU Magonjwa Si ZAWADI TOKA KWA MUNGU; Mungu Hutoa Vitu Vyema Na Vilivyo Na Ukamilifu Ndani Yake (Yakobo 1:17). Chochote KISICHO CHEMA NI CHA ADUI SHETANI!

MIMI SIWEZI KUWA MGONJWA KWA KUWA;

1.Mimi Ni Mali Ya Mungu, Ni Mtu Wa Nyumbani Mwa Mungu, Na Zaidi Ni Hekalu La Roho Wake Na Masikani Ya Mungu…Ugonjwa Au Maradhi Yatapata Wapi Nafasi Kuweka Makao Ndani Yangu?

2.Mimi Ni Mtumishi Wa Mungu, Ni Mwajiriwa Wa Serikali Ya Mbinguni, Mimi Ni Wakili Wa Siri Za Mungu Na Balozi Wa Serikali Ya Mbinguni Hapa Duniani…Kile Ambacho Mungu anataka Kukifanya Anakifanya Kupitia Mimi; Je Nikiwa Mgonjwa Itakuwaje? Maana Yake Shughuli Za Ufalme Wa Mungu Zita-stop Kisa Mimi Mgonjwa Niko Kitandani? Kwa Hali Hii, Mungu Hawezi Kuniruhusu Niwe MGONJWA Maana “MAVUNO NI MENGI, WATENDA KAZI WACHACHE” Na Mimi Mmoja Kati Ya Hao Wachache Nikiugua, Si Nitakuwa NIMEUTIA HASARA UFALME WA MUNGU? Hivyo Mungu Mwenyewe ANAWAJIBIKA KUITUNZA AFYA YANGU Ili Nitumike Pasipo Na Tatizo… HATA WEWE NI MTUMISHI WA MUNGU HAPO KWENYE FAMILIA YAKO, NDOA YAKO, KAZINI KWAKO, KANISANI KWAKO, JAMII YAKO Nakadhalika; Ukiwa Mgonjwa Mambo Mengi Ya Ufalme Wa Mungu Yanakwama, UAMUZI NI WAKO!

Kwa Leo Inatosha, Mungu Akusaidie Uone Hii Siri, Ili MAGONJWA YASIKUWEZE TENA NA UISHI MAISHA YA KUTOKUWA MGONJWA MAISHA YAKO YOTE YALIYO SALIA HAPA DUNIANI!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
One comment on “Si sawa kwa mkristo (hasa aliyeokoka) kuwa mgonjwa!
  1. Asant rowland says:

    Ahh hii ni content nzito sana..ni siri iliyo fichika ubarikiwe mwl…!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: