Kufufuka Kwa Yesu

Kufufuka kwa Yesu

(SIRI YA JEURI YA MKRISTO ANAYEIJUA)~

“YESU Akamwambia, Mama, Unalilia Nini? Unamtafuta Nani? Naye Huku Akidhani Ni Mtunza Bustani, Akamwambia, Bwana Ikiwa Umemchukua Wewe, Uniambie Ulipomweka, Nami Nitamwondoa. YESU Akamwambia, Mariamu. Yeye Akageuka, Akamwambia Kwa Kiebrania, RABONI! (Yaani Mwalimu Wangu). YESU Akamwambia, Usinishike; Kwa Maana Sijapaa Kwenda Kwa Baba. Lakini Nenda Kwa NDUGU ZANGU Ukawaambie, Ninapaa Kwenda Kwa BABA YANGU NAYE NI BABA YENU, KWA MUNGU WANGU NAYE NI MUNGU WENU” (Yohana 20:15-18).

Hapa Ndipo UKRISTO UNAPONOGEA… Hapa Ndipo Siri Ya Ajabu Ilipo Inayotupa Kuwa Na Sauti Ya KUFUNGA LOLOTE DUNIANI NA MBINGU ZIKALIFUNGA, Hapa Ndipo Tunapopata Sauti Ya KUFUNGUA LOLOTE DUNIANI LIKAFUNGULIWA MBINGUNI… UFUNGUO WA MAMLAKA YA MKRISTO NA UTOFAUTI WAKE NA WATU WENGINE WOTE UMEKAA KATIKA MISTARI HIYO HAPO JUU!

Yesu Amefufuka, Kabla Hajapaa Kwenda Mbinguni, PATAKATIFU PA PATAKATIFU KUWEKA AGANO JIPYA KWA BABA, Anaongea Na Mariamu Magdalene Akimzuia ASIMGUSE Maana HAJAENDA KWA BABA BADO!
Lakini Kubwa Ni MANENO YANAYOFUATA BAADA YA HILO, YESU Anasema SIRI ZA AJABU… Anazungumzia NAFASI YETU MARA TU BAADA YA KUFUFUKA KWETU… YESU Anasema:
“Lakini Nenda KWA NDUGU ZANGU Ukawaambie….Ninapaa Kwenda Kwa BABA YANGUNAYE NI BABA YENU, KWA MUNGU WANGU NAYE NI MUNGU WENU”

Nini Tunapata Hapa? Kuna Ufunuo Gani Umekaa Ndani Ya Maneno Haya?
Hapo Juu Kwa Lugha Nyepesi YESU Anasema, ” TANGU SASA BAADA TU YA MIMI KUFUFUKA, NINYI SI WATUMWA WANGU, WALA SI MARAFIKI TU; NINYI MMEKUWA NDUGU ZANGU KIHALALI NA KISHERIA KWA DAMU YANGU NILIYOIMWAGA NA KWA MAUTI YANGU… NIMEYASHINDA MAUTI NA KIFO ILI MUNGU BABA YANGU AWE BABA YENU KISHERIA KABISA KAMA ALIVYO BABA YANGU… SASA MNAYO HAKI YA MUNGU WANGU KUWA MUNGU WENU NA KUPATA CHOCHOTE KWAKE SAWA NA MIMI NINAVYOPATA MAANA KIHALALI NA KISHERIA KWA KUFUFUKA KWANGU, MIMI NA NYIE TUMEKUWA FAMILIA MOJA BILA MIPAKA WALA TABAKA… MIMI NA NINYI TUNA FURSA NA NAFASI SAWA MBELE ZA BABA YETU… MIMI NA NINYI SOTE TU WARITHI, TURITHIO PAMOJA KILA ALICHONACHO BABA YETU NA MUNGU WETU”

Huu Ndio Ukweli, Kila Sekunde NAWAZA, NATAFAKARI, NATENDA, NAONGEA, NASEMA, NAKIRI NA KUISHI NIKIJUA MIMI NA YESU SI MTU NA MWOKOZI WAKE TU, BALI PIA NI “NDUGU YANGU” … MIMI NA YESU TUNACHANGIA BABA MMOJA, MUNGU ALIYE HAI… NINA HAKI YA KISHERIA KUPATA KILA AMBACHO YESU ANAWEZA KUPEWA NA MUNGU BABA… NINA FUNGUO ZA KUWEZA KUTENDA KILA AMBACHO YESU ALITENDA HAPA DUNIANI NA ZAIDI, KWA KUWA KAMA YEYE ALIVYO NDIVYO NA MIMI NILIVYO KATIKA ULIMWENGU HUU~

Hii Ndiyo Siri Ya Ajabu Ya KUFUFUKA KWA YESU Ambayo Kila Aliyeigundua HAWEZI KUWA TENA MTU WA KAWAIDA… YOTE MABAYA YASIYOWEZA KUMPATA YESU HAYAWEZI KUMPATA NA YULE ALIYEJUA HADHI NA NAFASI YAKE MPYA KUTOKANA NA KUFUFUKA KWA YESU… MIMI NAJUA NA HATA KWA NAMNA YOYOTE HUNITOI HAPO… HII NDIYO KWELI YOTE~

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: