Kwa waliooa na kuolewa tu

… Ambao hamna ndoa pia si mbaya kusoma kama maandalizi kwa hatua hiyo~ Yesu Alisema, “WATU WAWILI WATAKUWA WAMELALA, MMOJA ATATWALIWA NA MMOJA ATAACHWA” Lakini Hii Haitatokea Kwa WANANDOA WAKRISTO KWELIKWELI… Maana Kama Ni Wanandoa WAKRISTO WA KWELI, Watakuwa Na Kristo Mioyoni Mwao… Lakini Pia Kubwa Zaidi Watakuwa WAMEKUA NA KUFIKIA HATUA YA KUWA “MWILI MMOJA” … Hivyo Kama Ni KUACHWA WOTE KAMA MWILI MMOJA WATAACHWA… Na Kama Ni Kwenda WOTE WATAKWENDA~ Wanandoa Wanaojua Maana Halisi Ya Ndoa WANAKUWA WAMOJA KWENYE KILA KITU… KAMA ANANIA NA SAFIRA WALIVYOKUWA WAMOJA HATA KUFA KWA MAAMUZI YAO YA PAMOJA YA “KUMWIBIA MUNGU”… Ndivyo Pia WANANDOA WA SASA WAPASWAVYO KUWA NA KAULI MOJA NA KUWA WAMOJA/ MWILI MMOJA… Kama Wamekusudia Kufika MBINGUNI, Basi Wote. Kama Wameamua Kwenda Jehanamu Basi Wote WANAKWENDA. Sielewi Inakuwaje WANANDOA MNAKAA NYUMBA MOJA, KITANDA KIMOJA, MWILI MMOJA, Lakini Mkeo/Mmeo HAJUI MSHAHARA WAKO… Ama Umefikia Hatua Ya Kuanzisha BIASHARA, MRADI Au KITEGA UCHUMI Mahali “KIMYAKIMYA” Bila Mwenzio Kujua… NDOA SIO TENDO LA NDOA TU…COME ON, Hata WAZINZI NA WAASHERATI WANAWEZA HIYO! Ndoa Ni TAASISI Ambayo Kusudi La Kwanza Si UNYUMBA NA KUZAA WATOTO, Bali Kuunganisha WATU WAWILI AMBAO WAKO TAYARI KUUNGANISHA NAFSI, MIOYO NA MAWAZO YAO KUTIMIZA KILA KUSUDI AMBALO MUNGU AMEWEKA MAISHANI MWAO. Ni Ili Kuunganisha Watu Wawili Ambao WATATIANA NGUVU NA KUINUANA, ILI KWA UMOJA NA PAMOJA WATIMIZE ZILE NDOTO AMBAZO MUNGU AMENDIKA MIOYONI MWAO TANGU ALIPOWAUMBA. Na Lazima Hawa Watu Wawe WANAAMIANA, KUPENDANA NA KUTHAMINIANA KIASI CHA KUSHIRIKISHANA MAMBO YAO YOTE… KAMA WANAWEZA KUSHIRIKIANA MIILI YAO, WANASHINDWAJE KUSHIRIKIANA VITU VINGINE HIVI VIDOGO… WANANDOA FIKIRINI SAWAWA~ Shikamoo Mliooa Na Kuolewa, Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: