Namna Ya Kupata Chochote (Ahadi) Toka Kwa Mungu

Ahadi

NAMNA YA KUPATA AHADI ILIYOMO KWENYE BIBLIA KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU.

1.Iamini Ile Ahadi Kuwa Ni NENO LA MUNGU KWAKO; Ifanye YAKO MWENYEWE… Weka Jina Lako Pale Badala Ya Jina La Huyo Mtu Au Kundi Ambalo Mungu Alikuwa Amewaambia Kuhusu Ahadi Hiyo… Hii Ni Kwa SABABU “YOTE YATAPITA, LAKINI NENO LA MUNGU HALITAPITA KAMWE, LITADUMU MILELE”… Ni Muhimu Ujue Kuwa, “NENO LA MUNGU LI HAI, TENA LINA NGUVU” (Waebrania 4:12)…NA KAMA LI HAI, MAANA YAKE LINAISHI, KILA ATAKAYELIAMINI NA KULICHUKUA KAMA LAKE BINAFSI BILA KUJALI ZAMA AU NYAKATI LITAMPA MATUNDA YALEYALE AU ZAIDI.

2.Anza KUMWOMBA Mungu Aifanye Halisi Ile Ahadi/ NENO Maishani Mwako; Kadri Utakavyokuwa UMEAMINI VEMA KATIKA ILE HATUA YA KWANZA, NA KULICHUKUA LILE NENO KAMA LAKO, Itakuwa RAHISI KULIWEKA KWENYE LUGHA YAKO YA MAOMBI…Kumbuka, “MUNGU SI MTU ASEME UONGO WALA SI MWANADAMU AJUTE, AKISEMA JAMBO ANALIFANYA, AKIAHIDI ANATIMIZA” (Hesabu 23:19).

3.Anza Kulazimisha MAWAZO NA FIKRA ZAKO ZIKUBALIANE NA KUPOKEA HIYO AHADI; Upinzani Mkubwa Kwa Mtu Anapoamua KUIAMINI AHADI YA MUNGU AU NENO, NI MAWAZO YAKO NA FIKRA ZINAZOJENGEKA NDANI YAKO… Hii Ni Kwa Sababu Sehemu Yako Ya AKILI (MAWAZO NA FIKRA) IMEZOEZWA KUAMINI “YANAYOONEKANA NA YALIYOPO” Yale YASYOKUWEPO HAYAPOKELEWI KWA URAHISI… Biblia Inasema, “HATUFANYI VITA KWA JINSI YA MWILI INGAWA TUMEVAA MWILI, MAANA SILAHA ZETU ZINA NGUVU KATIKA MUNGU HATA KUANGUSHA NGOME. TUKIANGUSHA NA KUTIISHA KILA WAZO NA KILA FIKRA ILIYOJIINUA KINYUME NA ELIMU YA MUNGU (NENO LAKE)” (2 Wakorintho 10:3-4).

4.BADILI LUGHA YAKO; ANZA KUONESHA IMANI ULIYONAYO MOYONI MWAKO KUPITIA MANENO YAKO… KAMA IMANI HAIJAKUA KIASI CHA KUUNDA LUGHA YAKO YA NJE, HAIWEZI KUTOA MIUJIZA… ANZA KUSEMA, KUZUNGUMZA NA KUKIRI SAWA NA ILE AHADI YA NENO KWAKO… ZUNGUMZA KWA “UHAKIKA” ONESHA “MATARAJIO YAKO” MAANA IMANI INAJUMUISHA “UHAKIKA NA MATARAJIO KWA PAMOJA”
(Waebrania 11:1)… Yule Mwanamke Aliyetokwa Na Damu Kwa Miaka 12, ALIONESHA IMANI YAKE KWENYE “MANENO YAKE”… BARTIMAYO KIPOFU ALIONESHA IMANI KATIKA “MANENO YAKE”… MWANAMKE MKANANAYO AMBAYE MWANAE ALITESWA NA PEPO, ALIONESHA IMANI YAKE “KWENYE MANENO YAKE”… YULE AKIDA WA KIRUMI ALIYETAKA YESU AMPONYE MTUMWA WAKE, ALIONESHA IMANI YAKE KWENYE “MANENO YAKE”… PETRO ALIPOVUA SAMAKI MCHANA NA NYAVU ZIKAANZA KUKATIKA NA MASHUA KUTAKA KUZAMA KWA WINGI WA SAMAKI, ALIONESHA IMANI YAKE KWA “MANENO YAKE”
KWENYE MANENO YAKO KUMEJAA MIUJIZA YAKO KAMA UKIYATUMIA VIZURI; LAKINI YATAKUANGAMIZA UKIYATUMIA KINYUME CHAKO.

5.ANZA KUISHI KAMA ALIYEKWISHA POKEA AHADI HUSIKA; ONESHA IMANI YAKO KWA KUISHI KAMA MTU ALIYEKWISHA KUPATA KILE ALICHOKUWA AKIKIHITAJI, ENDELEA KUISHI KWA UHAKIKA, USIKUBALI HALI YA NJE IKUONESHE KUWA HUJAPOKEA AU HUJAPATA, AHADI YA MUNGU HAIWEZI KUSEMA UONGO…UKIUNGANISHA NA IMANI YAKO NA MAOMBI YA KUKIATAMIA, HATIMAYE “KIFARANGA CHA MUUJIZA” KITATOTOLEWA.

Naamini Umepata Kitu KIKUBWA CHA KUBADILI MAISHA YAKO; MALALAMIKO, MANUNG’UNIKO, LAWAMA SASA VIUE KWA KUTENDEA KAZI HIZI HATUA 5 ULIZOJIFUNZA, HALAFU “MUDA WA MUNGU, MUDA SAHIHI UKIFIKA UTAMPATA ISAKA WAKO”

Mungu Akubariki Sana,
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo
3 comments on “Namna Ya Kupata Chochote (Ahadi) Toka Kwa Mungu
  1. jane says:

    amen kila ninapozidi kusoma nafunguliwa imani kwa kiwango cha tofauti

  2. Ameni nabarikiwa sana masomo yenu. anuani yangu nii – ********@yahoo.com na Mungu azidi kuwapa mafunuo.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: