Chakula Cha Kila Mkristo

mkiristo

mkiristo

>> HASA WEWE UNAYEPENDA KUTOA MISAADA KWA MASIKINI NA WASIOJIWEZA (MUHIMU).

mkiristo

mkiristo

 

 

Mithali 19:17
“AMHURUMIAYE MASIKINI HUMKOPESHA BWANA; NAYE ATAMLIPA KWA TENDO LAKE JEMA”

Hivi Unakuwa Na Maana Gani Unapopita Kwa OMBAOMBA Ukampa Shilingi 100 au 200? Ile Kweli Ni SADAKA Ambayo Unalenga KUMKOPESHA MUNGU AU NI USHABIKI TU?
Unapata Wapi UJASIRI Wa Kumwona Mtu Yuko Kwenye UHITAJI (Ndo Maana Halisi Ya Masikini) Halafu Wewe Unachukua VILE VIJICHENJI ULIVYOKUWA NAVYO MFUKONI NDO UNAMPATIA… HUU SIO UTOAJI AMBAO ANAYETOA ANA LENGO LA KUMKOPESHA MUNGU… Unapotoa Kwa MASIKINI/ MHITAJI Kama Sadaka Ya Kumkopesha Mungu Lazima Uhakikishe Umetoa SEHEMU YA KILE KILICHOKUWA NDANI YA MIPANGILIO YAKO (BAJETI)… Mungu Hawezi Kupokea MAKOMBO!
Kila MASIKINI AU MHITAJI Unayepata MSUKUMO WA KUMPATIA KITU, NI “MADHABAHU” NA MUNGU ANAKUWEPO “KUPOKEA HIYO SADAKA YAKO NZURI AU MBOVU… IKIWA NZURI KAMA YA HABILI, “MUNGU ATAKUTAKABALI WEWE KWANZA, HALAFU NA SADAKA YAKO ATAIPOKEA”, IKIWA SADAKA MBOVU/ MAKOMBO, “UNAPATA LAANA KWANZA WEWE (Kama Anania Na Safira Ama Kaini) JAPO SADAKA YAKO HAITARUDISHWA”

Kuna Wengi Mnataka MUNGU Awabariki Na Kuwafanikisha Wakati MMEPANDA MBEGU MBOVU/ ZA UHARIBIFU… Lazima Mvune UHARIBIFU.
Yesu Anasema, “YOYOTE MNAYOPENDA KUTENDEWA NA WENGINE, BASI NINYI NANYI MYATENDE KWA WENGINE; NAYO MSIYOPENDA KUTENDEWA, MSIYATENDE KWA WENGINE PIA” (Mathayo 7:12).
Kama Wewe Usivyoweza Kufurahia Sh 100, Au 200 Unapopewa Kama Zawadi Au Sadaka Ya Upendo, Vivyo Hivyo Nawe USIMTENDEE BINADAMU MWINGINE “UFIDHULI HUO” HATA KAMA NI KILEMA AU OMBAOMBA; KUMBUKA HUYO NAYE NI KAZI YA MIKONO YA MUNGU, AMEUMBWA KWA SURA NA MFANO WA MUNGU.

Acheni Kuchuma Laana Ilhali Kulikuwa Na FURSA Ya Kupata Baraka, Si Kila UTOAJI Unaleta Baraka, Utoaji MBOVU Huleta Laana Na Hata Vifo; MUNGU HADHIAKIWI, UNACHOKIPANDA HAKIKA UTAKIVUNA TU~

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: