Nataka huu mtazamo na msimamo wa kifikira uwe sehemu ya maisha yako; maana ndivyo ulivyo.

Muujiza
Naamini Miujiza Ndiyo, Lakini Kubwa Kuliko Yote, Mimi Ni Muujiza Unaoishi.
Hakuwahi Kuishi Mtu Mwingine Aliye Kama Mimi,
Kwa Sasa Kati Ya Watu Zaidi Ya Bilioni 7 Wanaoishi Hakuna Mtu Aliye Kama Mimi,
Baada Yangu Hatakuwepo Mtu Mwingine Atakayekuwa Kama Mimi Kamwe.

Mimi Ni Muujiza Unaoishi, Mungu Alinijua Hata Kabla Sijawa Katika Tumbo La Mama Yangu; Siko Duniani Kama Matokeo Ya X Ya Mama Na Y Ya Baba.
Kabla Sijawa Katika Tumbo La Mama, Mungu Alinitakasa (Alinitenga Maalumu, Kwa Ajili Ya Kusudi Maalumu Ambalo Hakuna Mwingine Aliyenalo Wala Hatakuja Mwingine Aliyenalo).

Mimi Ni Muujiza Unaoishi, Mungu Ameniumba Nikiwa Na Sura Na Mfano Wake, Nimebeba Asili Ya Mungu,
Kubwa Zaidi Amenipa BARAKA Ya Kuzaa Katika Kila Kitu Na Sio Kuzaa Tu Bali Na Kuongezeka Na Kuzidi Sana Katika Kila Chema Nitendacho.

Mimi Ni Muujiza Unaoishi, Ni Kweli Dhambi Iliingia Ulimwenguni, Na Shetani Kuwa Adui Yangu, Lakini Mkataba Ule Wa Edeni Unanibeba Mimi,
Nitamponda Nyoka Kichwa Chake, Na Miguu Yangu Itafunikwa Na Damu Ya Mwanakondoo Iliyotoka Miguuni Mwa Yesu, Shetani Hatakigonga Kisigino Changu,
Kila Vita Na Changamoto Yangu Na Shetani Nitaibuka Mshindi Kwa Damu Ya Mwanakondoo Na Kwa Neno La Ushuhuda Wangu.
Nitashinda Na Zaidi Ya Kushinda Kwake Yeye Aliyenipenda,
Maana Aliyemo Ndani Yangu Ni Mkuu Kuliko Aliyemo Katika Ulimwengu Huu,
Nitamkanyaga Nyoka, Na Ng’e Na Kila Kazi Na Nguvu Zote Za Yule Adui, Na Kamwe Hakutakuwa Na Chochote Cha Kunidhuru.

Mimi Ni Muujiza Unaoishi, Niko Duniani Lakini Si Wa Dunia Hii,
Ni Raia Wa Mbinguni Niliye Hapa Duniani Kwa Muda Mfupi,
Kama Mpitaji Ninawajibika Kutoa Nuru Gizani,
Na Mataifa Wataikimbilia Nuru Yangu.
Kama Chumvi Ya Dunia Nitatia Radha Kila Mahali Palipopwaya,
Na Pia Nitahifadhi Kila Jema Ili Adui Asiliharibu Kama Vile Chumvi Inavyohifadhi Vyakula Viharibikavyo.

Mimi Ni Muujiza Unaoishi, Kama Baba Yangu Alivyo Mwanzo Na Mwisho,
Nami Ametangaza Mwisho Wangu Wa Ushindi Tangu Mwanzo Wangu.
Kila Mlima Na Kilima Vimeshushwa, Kila Palipoparuza Pamesawazishwa, Kila Bonde Limeinuliwa, Na Utukufu Wa Mungu Unapita Maishani Mwangu, Na Watu Wote Wanionao Wananiita Heri, Wananiita Mbarikiwa Ajaye Kwa Jina La BWANA,
MIMI NI MUUJIZA UNAOISHI.

Mimi Ni Muujiza Unaoishi, Mungu Mwenyewe Ndiye Mwalimu Wangu,
Siku Zote Ananifundisha Ili Nipate Faida.
Kila Sekunde Ananionyesha Njia Ya Kuiendea, Na Kila Muda Ananishauri Huku Jicho Lake Likinitazama.
Hatua Zangu Zinaongozwa Na Bwana.

Mimi Ni Muujiza Unaoishi, Malaika Wa Bwana Amepewa Jukumu La Kutangulia Mbele Yangu Kunipeleka Hadi Mahali BABA YANGU Ameniandalia,
Malaika Wamepewa Kazi Ya Kunitumikia Na Kunilinda,
malaika Wa BWANA Wanafanya Kituo Juu Yangu, Wanapigana Vita Zote Upande Wangu.

Mimi Ni Muujiza Unaoishi, Mungu Amenipa Uwezo Wa Kuumba Dunia Yangu Kupitia MANENO YA KINYWA CHANGU NA ULIMI WANGU,
Ninao Uwezo Wa Kuachilia Uzima Au Mauti Kwa Kinywa Changu,
Ninao Uwezo Wa Kubariki Au Kulaani Kwa Kinywa Changu,
Ninao Uwezo Wa Kujenga Au Kubomoa Kwa Ulimi Wangu,
MUNGU AMENIPA UWEZO WA KUAMUA UMBALI WA MAISHA YANGU NA UBORA WA MAISHA YANGU KWA KUTUMIA ULIMI NA MANENO YANGU.

Mimi Ni Muujiza Unaoishi Hakika,
Wewe Ni Muujiza Unaoishi Jamani, Usijidharau, Haya Yote Yanakuhusu Wewe, Hasa Kama UMEOKOKA!

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo
3 comments on “Nataka huu mtazamo na msimamo wa kifikira uwe sehemu ya maisha yako; maana ndivyo ulivyo.
 1. hope says:

  hakika!

 2. Dr August says:

  this is who I am,tears were flowing while eating this truth from God through you holly Servant,
  Ubarikiwe Sana Mwal.D.C.K

 3. jane says:

  amen great man of God

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: