Furahi, shangilia, inua moyo wako tena,

washindi

kila kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu… hii ndiyo kauli mbiu ya washindi wote ambao Yesu amewanunua kwa damu yake ya thamani… tunakutana na kila ugumu na changamoto; njaa, uchi, udhia, na kila kinachoumiza kama watu wengine… ila “mtazamo wetu” kuhusu hali za kimaisha ndio unaotufanya kuwa “washindi na zaidi ya washindi”… changamoto na mazito yanapokuja kwetu, “hatuondoi jicho kwa Yesu” na kuyapa nafasi yawe “bwana kwetu”… magumu yakija, “Yesu anakuwa yote na juu ya yote”… Yesu anakuwa njia pasipo na njia; anakuwa nuru palipo na giza; anakuwa bendera ya ushindi katika kila vita inayoinuka; Yesu anakuwa “mkate wa uzima na maji yaliyo hai” wakati wa uhitaji; Yesu anakuwa “mchungaji mwema” kila tunapopita katika bonde la uvuli wa mauti; Yesu anakuwa mwamba na ngome yetu kila muda shetani anapoiwinda amani na furaha yetu…. kitu gani cha kututenga na upendo wa Mungu baba katika kristo Yesu?? (warumi 8:34-37).

usikubali kupotoshwa na kupelekwa nje ya neno la Mungu na nje ya mapenzi ya Mungu kwa sababu ya changamoto au ugumu unaopitia; kila jambo linalokupata kama mwana wa Mungu, si bahati mbaya; baba yako wa mbinguni ameziruhusu, lakini atakuwa nawe kwenye tundu la simba…atakuwa nawe kwenye moto kama akina shedraka, meshaki na abednego… unapitia kwenye kuimarishwa na kujengwa ili uweze kuaminiwa kwa makubwa na mazuri yanayokuja… akiisha kukujaribu utatoka kama dhahabu; furahi, shangilia, usiyumbishwe na hilo unalopitia; aliyeko ndani yako ni mkuu…unaliweza hata hilo katika kristo Yesu akutiaye nguvu!

furahi, shangilia, inua moyo wako tena,
mwl d.c.k

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: