Msaada wa kiroho kwa Wagonjwa

Maombi

Narudia tena; nataka kuja hapo ulipo mimi na bwana Yesu kupitia roho wake mtakatifu tukusaidie!

Nimetoa tangazo jana kuhusu utayari wangu kuja kufanya huduma kokote ambako wanahitaji msaada wa kiroho.
Watu wenye wagonjwa wa aina zote, wanaotibika hospitali na wale wasio na tiba kwa wanadamu.hata wale walioko vitandani hoi, wamepoteza matumaini ya kuishi; hata kama wako hospitalini, niko tayari kuongozana na wewe mwenye mgonjwa kwenda hospitali kumwona mgonjwa wako na kumsaidia.
Pia kuna wale ambao wanaishi na magonjwa miilini mwao na walishayafanya sehemu ya maisha yao ya kila siku na wameridhika kuishi nayo; wenye ukimwi, kansa, kisukari, shinikizo la damu (bp) aina zote, ulcers, vidonda ndugu visivyopona au kukauka, magonjwa ya ngozi yanayokula mwili na mengine yoyote yoyote unayoyajua wewe!

Watu wanaoteswa na adui kupitia mapepo, majini, mizimu, uchawi na namna zote za nguvu za giza; hata kama anafungwa kamba, au anaokota makopo… Hata kama kichaa chake kimetokana na madawa ya kulevya au bangi, hiyo bado ni kesi ndogo mno kwa Yesu!
Wale msioweza kulala usingizi mkaufurahia kwa sababu ya uonevu wa ibilisi, pia Yesu yuko tayari kuziharibu hizo kazi zote za adui.

Waliopata ajali wakavunjika mifupa, misuli au mishipa, na hospitali wakasema haiwezekani, mnatembelea magongo, wheel chair, fimbo au support ya aina yoyote; wanaotumia neck colar, wanaotumia vitambaa vya kusaidia migongo au nyonga zao; wote hawa Yesu anaweza kuwarejezea afya yao ya kwanza!
Wale waliopooza [walio-paralize] na wengineo ambao wamekuwa katika hali ya kutotembea kwa muda mrefu, nao wanaweza kurudi tena kutembea.
Viziwi, viwete, wanaosumbuliwa na matatizo ya mifumo ya fahamu kama kifafa na mengineyo; yote haya yako ndani ya uwezo wa wa Yesu.

Matasa, wagumba; haijalishi mmekuwa kwenye ndoa kwa miaka mingapi bila kupata watoto; tutakutana na kuongea kila kitu kwa mujibu wa neno la Mungu, halafu tutaufukuza huo utasa na ugumba na mtakuwa wazazi, ni rahisi sana namna hiyo!

Kwanini miujiza siku hizi ni adimu?

Wakristo wanaogopa kuiweka imani yao kwenye matendo; wanawaza itakuwaje nikimwombea mtu halau badala ya kupona akafa? Kwa taarifa yako, nimeshaombea watu kama watatu hivi na nikaamini wanapona, lakini wakafa; hiyo haikunikatisha tamaa au kunipa mashaka kuwa “nimeshindwa” hapana, mimi kazi yangu ni “kuweka mkono juu ya mgonjwa” halafu kazi ya “kuwapa uzima na afya” anaifanya mungu; si kesi yangu… Ni mungu kazini kupitia mikono yangu, imani yangu kwa neno lake na jina lake!

Imani isipowekwa kwenye matendo, tutaishia kusoma habari za matendo ya mungu kwenye biblia tu.
:kitabu cha matendo ya mitume kisingeandikwa kama mitume wasingetenda” (nukuu toka kwa smith wigglesworth).

Kumbuka “tu watenda kazi pamoja na mungu” ukiona mtu kapagawa na pepo, sogea pale “mtoe yule pepo kwa jina la yesu”, ukiona mtu kapata ugonjwa, sogea pale “weka mikono juu yake ufukuze huo ugonjwa” halafu mwachie mungu kumalizia sehemu yake ya “kuponya”

mwl d.c.k

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo, sala
2 comments on “Msaada wa kiroho kwa Wagonjwa
  1. Neema karia says:

    Naomba uniombee mtumishi wa Mungu nimekuwa sipati usingizi nateswa na mapepo na pia sins amani na ndoa yangu mime ananitenga na kunipuuza sana rana.

  2. Francis says:

    Ahsante mtumish wa MUNGU kwa ajili hyo.kwa kuwa unawatengenezea washirika msing wa iman ulo mzur

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: