Neno La Mungu Ndani yetu

neno ndani yetu

Biblia inatuambia kuwa, ukitaka kuona matokeo ya neno la Mungu kwenye maisha yako; lizungumze kila muda, lifanye lugha yako ya wakati wote na mahali pote!

“na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena, uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo, yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako; tazama yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya ya malango yako” (kumbukumbu 6:6-9).

Tunaposema kukiri neno, wakristo wengi wanadhani kukiri ni ule muda tukiwa kanisani, au muda wa ibada tu; kukiri neno maana yake ni kuhakikisha unazungumza sentensi za maneno yako zikiwa zimejaa neno la Mungu ndani ya kila maongezi ufanyayo… Unapokuwa nyumbani kwako hakikisha kila maongezi yako yamejaa neno la Mungu linalonena mema au kutabiri mema kwako na watu wa nyumba yako…. Ukiwa kazini iwe hivyo wakati wote… Ukiwa umekaa kuzungumza na marafiki, hakikisha kila kitu unachosema kiwe kwenye mstari wa neno, na kiwe kinaubeba unabii wa neno la Mungu juuu ya maisha yako… Walee na kuwakuza watoto wako kwa msingi huu wa neno la Mungu, jenga mazoea ya kuwasomea mistari ya biblia inayozungumza juu ya baraka, mema na future yao njema, pamoja na yale ambayo yanawakumbusha wajibu wao wa kuwatii na kuwaheshimu wazazi na Mungu!

Jizoezeni kulifanya neno la Mungu lugha ya kila siku ya kila jambo lako, hata kama mazingira yako kinyume; neno la Mungu ni lugha ya ufalme wa Mungu, ni lugha pekee inayopenya kwa haraka sana kwenye moyo na akili ya Mungu!

 

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: