Niseme kidogo kuhusu utoaji wa fungu la Kumi/Zaka!

zaka

Hii ni asilimia kumi ya mapato yako yote kutoka shughuli zako za uzalishaji; kilimo, ufugaji, ajira, biashara nakadhalika.

Hii Mungu amesema wazi inatolewa kwa walawi (watumishi wa madhabahuni), yatima, wajane na yatima (kumbukumbu 26:2, kumbukumbu 14:28-29). Zingatia haya;

1. kwahiyo wakati wa utoaji wa zaka/ fungu la kumi kuna maelekezo/ maagizo Mungu huwa anayaweka moyoni kwa mtoaji; hayo maelekezo yanakupa msukumo wa wapi pa kuitoa (madhabahu ipi); Mungu anaweza kukupa msukumo hiyo zaka umpelekee mtumishi wake wa madhabahuni (mlawi) yeye binafsi ama anaweza kukupa msukumo wa kuitoa kwenye kazi yake [kanisa/ huduma] anayotaka yeye; hapa kazi inakuja kama mtoaji wa zaka ni mtu aliyefungwa na u-dhehebu au u-kanisa; hawezi kutii kuipeleka kwingine hata kama anasikia msukumo ndani yake wa kufanya hivyo!
Lakini pia Mungu anaweza kukusukuma ukaitoe kwenye madhabahu iitwayo “mjane fulani” au “yatima fulani” au hata “mgeni fulani” usiyemjua!
Thamani ya zaka yako si kule kuwa zaka kamili; bali thamani ya zaka au sadaka yoyote nyingine ni kuitoa sawa na maelekezo uliyowekewa ndani/ unayosikia moyoni mwako/ msukumo ndani yako!

2.  Hakikisha unapopata faida, mshahara au pesa kutoka kwenye chanzo chako cha uchumi; kabla ya kuitumia ile pesa kwa jambo lingine lolote; kwanza kabisa tenga hela yako ya fungu la kumi pembeni, halafu hiyo 90% inayobaki ndo uanze kuitumia kwa kadri ya mpangilio wa bajeti yako!
Lakini ni vema sana ukatenga hela ya sadaka ndani ya ile 90% iliyobaki, halafu zitakazobaki zitumie kama ulivyopanga kwenye bajeti yako!

Kwanini ni lazima na muhimu kufanya hivyo??

Unapotenga hela ya zaka/ fungu la kumi kwanza kabla ya kutumia hela yako kwa chochote kingine, unamuonesha Mungu kuwa anayo nafasi ya kwanza kwako na ya kuwa kabla ya maswala ya maisha yako “Mungu ndiye wa kwanza”
“ufalme wake na haki yake kwanza halafu mengine yote mtazidishiwa” (mathayo 6:33).

Ushauri wangu;

1. hakikisha unatoa fungu la kumi lililotimia yaani isiwe pungufu ya asilimia kumi… Biblia inahimiza kutoa “zaka kamili” (malaki 3:8-11).
Ni bora uzidishe iwe zaidi ya 10% kuliko kuifanya iwe pungufu; anayetoa pungufu ni sawa na asiyetoa kabisa, wote biblia inawaita wezi!

2. kabla ya kutumia kipato chako, mshahara, faida ya biashara, kilimo au mifugo; hakikisha umetenga kwanza asilimia kumi ya Mungu/ zaka maana hiyo ni mali yake (walawi 27:30), kwenye 90% inayobaki, tenga hela yako ya sadaka kutegemeana na unavyosukumwa na kuongozwa ndani yako; halafu hiyo inayobaki ndipo ukaitendee kazi zako sawa na bajeti na mipango yako!

3. ni muhimu kuwa mtulivu na msikivu kwa Mungu hasa linapokuja swala la utoaji wa zaka au fungu la kumi; sikiliza vizuri maelekezo na msukumo moyoni mwako wa wapi uipeleke zaka yako; kanisani kwako, au kwa mtumishi fulani, au kwa mjane, au kwa yatima, au kwa mgeni… Swala si kutoa zaka, ila na mahali pa kuitoa sawa na usukumwavyo ni muhimu sana; sikiliza sauti ya moyo wako1

MWL D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
8 comments on “Niseme kidogo kuhusu utoaji wa fungu la Kumi/Zaka!
 1. Sarah Mayanja says:

  Mfano unadaiwa karo ya sh 10000 na ukapewa 10000 ili ulipe na uweze kuingia mtihan. Je hapo fungu la kumi litakuwaje.

 2. wambura festo says:

  kama nimepata mshahara na nina ndugu na wazazi ambao wanahitaji pesa kwa ajili ya matibabu na ni zaidi ya hii niipatayo nafanyaje kuhusu hilo niwasaidie au nitoe fungu la kuni nisiwasaidie wao

 3. Rabanation says:

  Fungu la kumi linaweza kutolewa kwa walawi (Watumishi wa madhabahuni) je ikiwa mimi ni mmoja wa hao watumishi Ninaweza kula funga la kumi?

 4. daniel kiondo says:

  Hivi je kama ni mjasiriamali nimekopa hela bank million 2 kwa ajili ya biashara hapa fungu la kumi nitatoa kwanza hata kabla ya kuzalisha au nizalishe kwanza ndio nitoe kwenye faida ninayopata?naomba nielewe hapa zaidi

 5. daniel kiondo says:

  Naomba hebu hapa pa kutoa fungu la kumi tupaweke sawa kiasi cha mtu aweze kuelewa ili tusiendelee kutotoa kuliko kamili
  1.ktk mkopo ninaokopa natoa fungu la kumi kwenye hela niliyopewa ya mkopo au ninatoa kwenye faida baada ya kufanya biashara?
  2.Na kama nilikuwa na shida nikamwomba ndugu yangu anisaidie hela na akanipatia hela je hiyo nayo naiitolea fungu la kumi?

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: