FUNGUO ZA KUFUNGUA KILA MLANGO

image

“NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI” (Mathayo 16:19).

1.Vitu Vyote Vilivyoko Hapa Duniani, Mungu Ameviweka Kwenye Usimamizi Na Uangalizi Wa MKRISTO ALIYENUNULIWA KWA DAMU YA THAMANI YA YESU.

“NAO WAIMBA WIMBO MPYA WAKISEMA, WASTAHILI WEWE (YESU) KUKITWAA KITABU NA KUZIFUNGUA MUHURI ZAKE; KWAKUWA ULICHINJWA, UKAMNUNULIA MUNGU MUNGU KWA DAMU YAKO WATU WA KILA KABILA, NA LUGHA NA JAMAA NA TAIFA, UKAWAFANYA KUWA WAFALME NA MAKUHANI WAFALME NA MAKUHANI KWA MUNGU WETU; NAO WANAMILKI [WANATAWALA NA WANA KAULI YA MWISHO] JUU YA NCHI” (Ufunuo 5:9-10 Tafsiri Ya Biblia Ya King James).

Mungu Hawezi Kufanya Kitu Huku Duniani, Bila Kwanza Kupewa Ruhusa Au Mlango Na Wafalme Na Makuhani (sisi tulionunuliwa kwa Damu Ya Yesu).
Ndio Maana USIPOFUNGUA, Mbinguni Hawafungui; USIPOFUNGA Na Mbinguni Hawafungi.
Kwa Lugha Nyepesi UFALME WA MUNGU UNATEGEMEA UWEPO WAKO WEWE MKRISTO (Mfalme) NA KAULI ZAKO ZA KUFUNGA NA KUFUNGUA, ILI NA WAO WAWEZE KUFUNGA AU KUFUNGUA CHOCHOTE!
Kila Kitu Kwenye Maisha Yako, Ndoa Yako, Kanisani Kwako, Kazini Kwako; HAKITABADILIKA MPAKA UTAKAPOKAA KWENYE NAFASI YAKO YA KIFALME NA KUANZA KUTOA MATAMKO YA KIMAMLAKA (KUPITIA MAOMBI YALIYO SAWA NA NENO LA MUNGU).
Wewe Mwenyewe Ndiye Unayesababisha MABADILIKO YASIWEPO; UKIAMUA KUYATANGAZA NA KUYASIMAMIA, NA MUNGU NAYE ATAYAFANYA KUWA HALISI; HALI YAKO NI MATOKEO YA MATUMIZI YAKO MADOGO YA NAFASI YAKO KAMA MFALME!

2.FUNGUO HIZI ZINAWEZA KUFUNGA MLANGO WOWOTE, NA ZINAWEZA KUFUNGUA MLANGO WOWOTE.

Kupitia Nafasi Yako Hii Ya Kifalme Unaweza KUFUNGA MLANGO ADUI ASIENDELEE KUFANYA KAZI KWENYE ENEO FULANI, NA MBINGUNI WATAKUSAIDIA KUUZIBA HUO MLANGO; HAWAWEZI KUFANYA CHOCHOTE MPAKA WEWE ULIAMURU HILO “KAMA MFALME”
Kupitia Nafasi Yako Kama Mfalme, Unaweza KUFUNGUA MILANGO YA MAENEO UNAKOPENDA UFALME WA MUNGU NA SERIKALI YAKE VIINGIE NA KULETA MABADILIKO CHANYA YALIYO BORA.
Unaweza Kufungua Milango Yako Ili UFALME WA MUNGU Kuingia Na Kuonekana Kwenye NDOA, FAMILIA, KANISA, KAZINI, OFISINI, FAMILIA YENU Nakadhalika Kwa KUFANYA MAOMBI YA TOBA YA KUUKARIBISHA UFALME WA MUNGU HAPO; TOBA INAONDOA UHALALI WA DHAMBI NA UASI KWENYE ENEO UNALOLIOMBEA, NA DHAMBI IKISHAFUTWA, SHETANI ANAPOTEZA UHALALI WA KUENDELEA KUSHIKILIA HAPO, NA HAPO NDIPO UNAWEZA KUMLETA YESU NA SERIKALI YA MBINGUNI WAJE!

Yesu Alisema, “TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI (SERIKALI YA MBINGUNI) UMEKARIBIA”
Hii Ni Aina Ya Toba YA KUMNYANGANYA IBILISI UHALALI WAKE WA KUWA PALE KWA SABABU YA DHAMBI NA UOVU; NA KUMFUNGULIA MUNGU ALIYE HAI NA SERIKALI YAKE KWENYE ENEO HILO, ILI KUWE NA MTEMBEO NA MKONO WA USTAWI WA MUNGU ALIYE HAI, NA MEMA YA PALE YAANZE KUONEKANA!

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “FUNGUO ZA KUFUNGUA KILA MLANGO
  1. Joshua emmess says:

    Kila tendo la mwanadamu hapa duniani ni ishara ya alivyo yeye. Maana mwanadamu kwa matendo yake ni Sawa na barua inayosomwa na watu. Je wewe mwenzangu unasomekaje?

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: