Kama Kila Mkristo Angejua Kufanya Mambo Yafuatayo

image

Shetani, Ngvu Za Giza Kwa Ujumla Visingekuwa Topic Kwenye Midomo Yao, Bali Wangekuwa Chini Ya Miguu Yetu;

1.Kama Kila Mkristo Angeweza KUYACHAMBUA MAWAZO YALIYOKO NDANI YAKE, NA KISHA KUYATAMBUA YALE YALIYO KINYUME NA NENO LA MUNGU, Kisha Kuchukua Hatua Ya Kuyapinga Na Kuyaangusha Kwa Mamlaka Ya Jina La Yesu Na Neno La Mungu, Kusingekuwa Na Mkristo MWOGA, MWENYE MASHAKA, HOFU Nakadhalika; Vyote Hivi Ni Matokeo Ya Mkristo Kushindwa Na Mawazo Yaliyo Kinyume Na Neno La Mungu.
Hii Ndiyo Sababu Ya Mungu Kutuhimiza “KUJAZA NENO LAKE NDANI YETU KWA WINGI” Maana Likiwemo La Kutosha, Litakusaidia Kuchambua Kila WAZO HASI NA KISHA KULIPINGA NA KULIKATAA MARA UNAPOLITAMBUA, MAANA ANAKUWA NI SHETANI HUYO ANAJARIBU KUKUANGUSHA, KUKUPELEKA DHAMBINI, Nakadhalika!
(2 Wakorintho 10:3-5).

2.Kama Kila Mkristo Angeweza KUULINDA MDOMO WAKE; Kwa Kutoruhusu Mdomo Wake Unene Mambo Hasi, Mambo Yaliyo Kinyume Na Neno La Mungu, Mambo Manyonge, Mambo Yasiyojenga, Mambo Yasiyoinua Imani, Basi Kila Mmoja Wetu Angekuwa ANATEMBEA JUU YA SHETANI NA NGUZU ZAKE ZOTE!
Kila Neno Unalosema LILILO KINYUME NA NENO LA MUNGU, LINAMPA IBILISI MLANGO NA NAFASI KUKUSHAMBULIA NA KUKUSHINDA.
Ukiri Wako Utaamua Mamlaka Yako; Ukikiri Na Kuzungumza KILA KITU Sawa Na Vile Neno La Mungu Lilivyosema, UTAPATA MATOKEO CHANYA, IMANI YAKO NA UJASIRI WAKO KATIKA MUNGU UTAPANDA, MATUMAINI YAKO NA MATARAJIO KATIKA MAISHA YAKO PIA YATAINUKA; UTAONA KUISHI BADALA YA KUFA, UTAONA KUSHINDA BADALA YA KUSHINDWA, UTAONA KUFAULU BADALA YA KUFELI, UTAONA NGUVU YA MUNGU BADALA YA UNYONGE NA UDHAIFU, UTAONA UTAJIRI BADALA YA UMASIKINI, UTAONA UZIMA BADALA YA MAUTI!
Maneno Yote Yaliyo Kinyume Na Neno Yanakupiga Mweleka (Mithali 18:6-7, Mithali 6:2, Mathayo 12:34-37).
KAMA UNATAKA KUWA MSHINDI KWENYE MAISHA; ZUNGUMZA NENO LA MUNGU KAMA LUGHA YAKO YA KILA SIKU, NA YA KILA MJADALA…LAKINI HII ITATEGEMEA NA “KIWANGO CHA NENO LA MUNGU ULILOFANYA BIDII KULIWEA NDANI YAKO”
UKIWA NA NENO LA MUNGU LA KUTOSHA, UTAKUWA MSHINDI, NA UTAZUNGUMZA LUGHA YA MUNGU NA MTAZAMO WA MUNGU KWENYE KILA JAMBO!

3.Kama Kila Mkristo Angeliulinda MOYO WAKE; Akahakikisha Kuwa Hakuna HABARI AU TAARIFA MBAYA Inayopenya Kuingia Moyoni Kwake, Na Kuvuruga AMANI YAKE NA FURAHA, Kila Mkristo Angekuwa Mshindi.
Wakristo Wengi WANANYANYASWA NA IBILISI Kwakuwa Wanapopata Habari Za Huzuni, Masikitiko, Hofu Na Mabaya Wao WANAZIINGIZA MOYONI MWAO NA ZIKISHAINGIA HUMO ZINAKULA AMANI NA FURAHA YAO, Wanakondeshwa Mioyo Yao, Na Kuanza KUKIRI NJE MAUMIVU, HUZUNI, UCHUNGU, HASIRA, LAWAMA, KUSHINDWA Nakadhalika Ambavyo HUMTENGENEZEA ADUI MLANGO MKUBWA WA KUWASHINDA!
LINDA SANA MOYO WAKO KULIKO YOTE UYALINDAYO, MAANA HUKO NDIKO ZILIKO CHEMCHEMI ZOTE ZA MAISHA UNAZOZIHITAJI (Mithali 4:23).
Kila Habari Au Taarifa Inayokujia Iliyo Mbaya, Ya Kuumiza, Ya Kuhuzunisha Au Kusikitisha, USIKUBALI IVUKE KICHWANI NA KUINGIA KWENYE MOYO WAKO; FUNGA MOYO WAKO ILI HABARI MBAYA ZISIINGIE NA KUKUHARIBIA AMANI NA FURAHA YAKO.
Hakikisha UNAUFUNGUA MOYO WAKO KWA AJILI YA HABARI NJEMA TU; KILE AMBACHO NENO LA MUNGU LINASEMA, ZILE AHADI ZAKE ZA KUKUFANIKISHA, YALE MAKUSUDI YAKE MEMA NA YA AMANI YA KUKUPA TUMAINI KATIKA KESHO YAKE; JAZA MOYO WAKO KWA AHADI ZA MUNGU KUTOKA KWENYE BIBLIA, NA USIUFUNGUE KUPOKEA HABARI YOYOTE INAYOONDOA AMANI NA FURAHA YAKO!

4.Kama Kila Mkristo ANGELIKUWA MAKINI KULINDA MACHO NA MASIKIO YAKE; Angekuwa Salama Kutoka Kwenye DHAMBI NA UOVU.
Dhambi Nyingi Anazofanya Mtu Ni Matokeo Ya KUTAZAMA NA KUSIKIA MANENO NA TAARIFA HASI NA MBOVU ZA DUNIA HII ZILIZO KINYUME NA NENO LA MUNGU.
Kama Ukiwa Na Nidhamu Ya Kuzuia Macho Yako Yasianagalie UCHAFU, Na Masikio Yako Yasisikie TAARIFA MBAYA, Basi Utafurahia Ushindi Kila Siku, HII NI UCHAGUZI WAKO, HAKUNA WA KUKUFANYIA HILO!

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
3 comments on “Kama Kila Mkristo Angejua Kufanya Mambo Yafuatayo
  1. SEBASTIAN NDOHELO says:

    Mtumishi wa Mungu wa mbinguni aliye hai milele na milele zote… Nakutakia baraka za Bsana Katika maisha yako yote rohoni na mwilini.

  2. Asant rowland says:

    Mwl nmekuwa makini kufuatilia haya mafundisho,kw kwl najifunza sna;siach kukuombea MUNGU akufunulie zaid na zaid

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: