Namna ya kutimiza ndoto/maono au njozi yoyote uliyonayo (soma hii, ielewe itakusaidia; kisha share kwa wengine nao wasaidike)!

Ndoto kuwa kweli

Siku Zote Mungu Huwa Ana Tabia Ya Ku-Support MAONO (Vision) Aliyokupa. Lakini Hataweza Kui-Support Kama HAUJACHUKUA HATUA YA KUIHAMISHA “TOKA KICHWANI” Ije Kwenye “KARATASI-MAANDISHI” Ili WATU WENGINE Wapate Nafasi Ya KUISOMA NA KUIELEWA KAMA MAJI (Yaani Iwe Katika Namna Rahisi Na Inayoelewaka Sana, Kiasi Kwamba Kila Utakayekwenda Kumpelekea Aisome Au Kumshirikisha, Aielewe Kwa Wepesi)!
“Akanijibu Akaniambia, IANDIKE NJOZI (Write Down Your Vision) UKAIFANYE IWE WAZI SANA KATIKA VIBAO, ILI KILA AISOMAYE APATE KUISOMA KAMA MAJI (Make It Simple And Plain That Everyone That Reads It Understands It Deeply)” (Habakuki 2:2).
Watu Wakielewa MAONO YAKO Uliyobeba, Inakuwa Vyepesi Kwa Wao KUWEKEZA MUDA, PESA, HEKIMA NA NGUVU YAO Hapo; Maana Kila Mtu Anapenda Kuwa Sehemu Ya JAMBO LINALOACHA ALAMA NA KULETA MABADILIKO CHANYA KWENYE JAMII, Ili Naye Awe Sehemu Ya Historia Ya Walioleta Mabadiliko Au Maendeleo.
MAONO YAKO Yakieleweka Kwa Watu Ukafanikiwa KUPATA “UTAJIRI WATU” Tayari Utakuwa Umepata Msingi Wa Kuanzia; Kutokana Na Watu Hao, Utakuwa Umepata WATU WA KULIOMBEA PAMOJA, Watu Wa Kukutia Moyo, Watu Wa Kukushauri, Watu Wa Kukusaidia KUINGIA MAHALI AMBAKO PEKE YAKO USINGEFIKA!
Jinsi Unavyoendelea Kushirikisha Watu Zaidi, Ndivyo Unavyozidi Kukutana Na Watu Zaidi [WABAYA KWA WEMA] Lakini Kitakachokusaidia NI WEWE KUWA MWOMBAJI, Na Kumsihi Mungu AWAZUIE WASIO WEMA WASIINGIE, NA AKUKUTANISHE NA WATU SAHIHI, ALIOKUWEKEA KUKAMILISHA MAONO HAYO ALIYOKUPA!

Usiogope Kuwashirikisha Watu MAONO YAKO, Maana Usipowashirikisha UTABAKI PEKE YAKO, Na “HAKUNA MTU YEYOTE AMBAYE AMEWAHI KUFANYA JAMBO LOLOTE KUBWA AU KUTIMIZA MAONO YOYOTE BILA KUSHIRIKIANA NA WATU; HAKUNA HATA MMOJA”
Usiogope Kwamba “WATAKUIBIA MAONO YAKO”… Anayekuibia Maono Yako, HAWEZI KUKUIBIA WATU WAKO, HAWEZI KUKUIBIA HEKIMA YA KUYAFANYA KUWA HALISI, HAWEZI KUKUIBIA “MIPANGO NA MALENGO NA NAMNA YA KUITENDA” Hivyo ATAKWAMA, Maana Yako Mengi Kwenye MAONO Ambayo HUBAKI NDANI YA MBEBA MAONO!
Hivyo Usiogope Kuweka Wazo Lako Wazi Kwa Watu [Japo Fanya Hivyo Baada Ya Kuomba] Na Kwa Kufanya Hivyo Utawapata Watu “POTENTIAL” Na “INSTRUMENTAL” Ambao WATAKUPA MKONO WA SHIRIKA Hadi HILO ULILOBEBA LIWE HALISI.

JAMBO LA MSINGI NA LA KUZINGATIA;
Watu Wengine Wanashindwa Kufanikiwa Na Kutimiza Ndoto, Maono Na Njozi Zao Kwa Kuwa HAWAJAJUA Kuwa “HAKUNA MAONO YALIYOWAHI KUTIMIZWA NA MTU MMOJA” Lazima Ushirikiane Na Watu; Usiogope Kuhusu HESHIMA YAKO KAMA MUASISI WA MAONO, Itabaki Palepale Maana Wengine Wote Watajua Wazi Kuwa “WEWE NDIWE ULIYEKUWA MWENYE HIYO NJOZI”
Hivyo Ushinde “UMIMI” Kama Unataka KUFANIKIWA NA KUTIMIZA MAONO NA NDOTO ULIYOBEBA MAISHANI MWAKO!

Pili; Jijengee MOYO WA SUBIRA, Ondoa Ndani Yako Wazo La Kufanya Kitu Cha Kimaono Na Kikatokea Hapo Kwa Hapo.
Utakutana Na Vita Na Changamoto, Lakini UVUMILIVU WAKO Ndio Utakaokusaidia Kufikia Lengo.
KADRI Unavyokutana Na Changamoto Lakini Ukashikilia MSIMAMO WA KUENDELEA KUFUATILIA Lile Jambo Bila Kujali LIMEKUANGUSHA KIASI GANI NA MARA NGAPI, Utajikuta Unapata Mlango Wa Kutokea Na KUTIMIZA NDOTO YAKO!
Biblia Inatupa Uhakika Na Uhalisi Wa Mambo Yafuatayo Kuhusu MAONO/ NJOZI;

1.HAITATOKEA KWA MUDA MWAFAKA ULIOJIWEKEA AU ULIOJIPANGIA; Lakini Maadamu Unaona Hilo Jambo Linawezekana Kufanyika Na Kuwa Halisi, INGOJE HIYO NJOZI MAANA “INA MUDA MAALUMU WA KUWA HALISI HAPA DUNIANI”… Kuna “MAJIRA KWA KILA KUSUDI CHINI YA MBINGU” (Mhubiri 3:1).

2.NJOZI/ MAONO HAYAWEZI KUSEMA UONGO, YANGOJE; Hata Siku Moja, Mungu Akikupa Uwezo Wa KUJENGA PICHA NDANI YAKO YA JAMBO LA MAENDELEO, NI KWAMBA TAYARI AMESHALITHIBITISHA NA KULIRUHUSU LIZALIWE HUKU DUNIANI… Iamini Ndoto Yako, Ukijaribu Leo Ukakwama, Haimaanishi Hilo Jambo Si La Mungu.
Mgunduzi Wa Umeme EDSON THOMAS Alifanya Majaribio 10,000 Ndipo Alipoweza Kubadili MTIRIRIKO WA UMEME KUWA MWANGA WA UMEME.
Kama Angefanya Majaribio 10 tu Na Kukata Tamaa, Huenda Leo Tusingekuwa Na Mwanga Wa Umeme.
Lakini Aliendelea KUJARIBU NA KUJARIBU NA KUJARIBU Na Hatimaye Akafanikiwa KUTIMIZA MAONO YAKE YA KUPATA MWANGA WA UMEME!
Kwanini Umelikatia Tamaa Wazo Lako La Biashara Kisa Umekosa Mtaji? Je Umewafuata Watu WAELEWA WANGAPI Ambao Wamegoma Kukusaidia Walau Hata Mawazo?
Kwanini Umekata Tamaa Ya Kufanya Hiyo Shughuli Eti Kisa Uliianzisha Mara 2 Au 3 Na Ikafa Na Umefikia Hatua Ya Kusema Eti HUNA MKONO Au BARAKA Katika Hilo? AMKA, FANYA TENA, NA TENA NA TENA, Huku Ukimsihi Na Kumwitia MUNGU ALIYE HAI; KITAELEWEKA TU!
Malizia Habakuki 2:3.

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: