Tukifa pamoja naye,Tutaishi Pamoja Naye

Tutaishi Pamoja naye

“Ni Neno La Kuaminiwa. Kwa Maana Kama Tukifa Pamoja Naye, Tutaishi Pamoja Naye Pia, Kama Tukistahimili, Tutamiliki Pamoja Naye, Kama Tukimkana Yeye, Yeye Naye Atatukana Sisi, Kama Sisi Hatuamini, Yeye Adumu Wa Kuaminiwa, Kwa Maana Hawezi Kujikana Mwenyewe” (2 Timotheo 2:11-13).

-Watu Wengi Walio Ndani Ya Mwili Wa Kristo Hawatafanikiwa KUISHI Katika MAISHA YA USHINDI, UKAMILIFU NA UTELE Kwa Kuwa WAMEKATAA KUFA PAMOJA NA YESU; Wamekataa Kuyatoa Maisha Yao, Miili Yao, Mipango Na Kila Linalowahusu Kuwa Chini Ya UONGOZI NA USIMAMIZI WA YESU; Wanataka Wao Wawe Na Sauti Ya Mwisho Kwenye Maeneo Mengi Ya Maisha Na Yesu Aishie KUWAOKOA NA KUWAINGIZA MBINGUNI; Usipokubali Kufisha Akili Na Hekima Yako, Na Kumruhusu YESU Ashike Usukani Wa Yote, Hautaweza KUISHI MAISHA YA JUU NA YA UTUKUFU AMBAYO MBINGU ZILIKUKUSUDIA!
Paulo Anasema, “SI MIMI NINAYEISHI, BALI KRISTO YESU YU HAI NDANI YANGU, NA UHAI NILIONAO NINAO KATIKA IMANI YA MWANA WA MUNGU ALIYENIPENDA NA KUJITOA AFE KWA AJILI YANGU” (Wagalatia 2:20).
Ili Uishi Na Kustawi Sawa Na Ahadi Ya Mungu Kwako, Lazima Ukubali Kufisha VIUNGO VYAKO VILIVYO KATIKA NCHI!

-Hautaweza KUMILIKI Kama Hautakubali KUSTAHIMILI Kila Gumu Na Changamoto Inayoibuka Na Kuja Kinyume Chako. Waliofanikiwa Kumiliki Ni Wale Waliokubali KUTULIZA MIOYO YAO KWENYE AHADI ZA KWELI ZA MUNGU, NA KUMNGOJA BWANA, Mpaka Alipojiridhisha Na Usafi Na Uaminifu Wa Mioyo Yao Na AKAWAMILKISHA MEMA.
Kama Ukiamua KUIUZA IMANI YAKO, Kama Ukiamua KUSHUSHA VIWANGO VYA YESU WAKO ILI KUPATA VITU FULANI, ITAKUGHARIMU… ITAKUFUNGIA MLANGO WA WEWE KUMILIKI NA KUSTAWI KATIKA MAKUBWA SAWA NA MUNGU ALIVYOKUWA AMEKUKUSUDIA!

-Umwamini Ama Usimwamini Mungu Hautamgeuza.
Uliamini Ama Usiliamini Neno Lake, Hautageuza UKWELI, UHALISI NA USAHIHI WAKE KWENYE MAISHA YETU SISI TUNAOMWAMINI.
Umwamini Yesu Ama Usimwamini, Hautatuzuia Sisi Tuliokwisha Kumwamini Kuendelea Kuuona WEMA NA UZURI WAKE.
“HATA USIPOMWAMINI, ANABAKI WA KUAMINIWA”

Mwl D.C.K

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “Tukifa pamoja naye,Tutaishi Pamoja Naye
  1. Dionise Majaliwa says:

    Yesu yu hai ktkameno km haya yaliyojaa nguvu kuu ya roho wa Mungu Hakika tutapona ikiwa tutamtii roho wa Mungu anenaye masi kupitia mtumishi wake; M.D.K Mwalimu Mungu wa mbinguni aishiye milele Akutimizie haja za moyo wako na aendelee kukufanya msaada kwa watu wake!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: