Mungu ambako amekusudia tufike

Ni Kawaida Ya Mungu Kuyatumia MATUKIO TUSIYOPENDA/ YANAYOUMIZA MAISHANI MWETU Kama Ngazi Ya Kutupeleka Kule Ambako AMEKUSUDIA TUFIKE!
Kwa Hali Ya Kawaida Haipendezi Kumwona “HOUSE GIRL” HAJIRI Akimzaa ISHMAEL Wakati Sara Akiwa TASA; Wala Haileti Maana Kuona Mungu Akimwambia Hajiri Kuwa “ATAMBARIKI ISHAMEL AZAE MASEYIDI (Wanaume Wanaounda Makabila) KUMI NA WAWILI” Haikuwa Nzuri Machoni Pa Sara Lakini Mungu Alimruhusu ISHMAEL Azaliwe Ili Wana Wa Ishmael WAMNUNUE YUSUFU Wampeleke Misri Akawe WAZIRI MKUU Huko; Kuwako Kwake Kupelekee Taifa La Israel Kuja Misri Na Kuwa Utumwani Na Kisha MUSA ATOKEE, Miujiza Ya Kumtukuza Na Kumwinua Mungu Itokee Na KUMTAMBULISHA MUNGU WA BIBLIA Kwa Dunia Nzima!

Bahari Ya Shamu Mbele Ya Israel Ilikuwa HABARI MBAYA Ukizingatia Nyuma Kulikuwa Na Jeshi La Farao Na Kwingine Kote Wamezungukwa Na Milima; Lakini Kwa Mungu Bahari Ya Shamu Ilikuwa NJIA YA ISRAEL KUENDEA KANAANI NA KABURI LA WAMISRI!

Ukisoma Habari Za Lutu Na Wanawe Wa Kike Wawili Unawaona Wakimpa Kileo Baba Yao Na Kuzaa Naye Taifa La MOABU; Kwa Hali Ya Kawaida Ni Chukizo Na Uasi Kwa Mtu Kuzaa Na Baba Yake, Lakini Mungu Aliona Zaidi Ya Hilo; Alimwona RUTHU, Mkwe Wa Naomi Tunayesoma Habari Zake Kwenye Kitabu Cha Ruthu… Huyu Alikuja Kuolewa Na Boazi Ambaye NI SEHEMU YA UKOO WA BWANA YESU; Kama Ruthu Aliyetokana Na Moabu Asingekuwepo, YESU ANGETOKEA WAPI? Hesabu Za Mungu Ziko Juu Sana Kuliko Mawazo Na Akili Zetu!

Kifo Cha Lazaro Wa Bethania Tena Baada Ya Kuwa Wamepeleka Taarifa Mapema Kwa Yesu Kuwa “YULE UMPENDAYE HAWEZI” Lilikuwa Jambo Gumu Kwa Mariamu Na Martha Dada Yake, Na Wenyeji Wote Wa Bethania, Lakini Mbali Ya Kuwa Mbaya Kwa Watu, Kwa Mungu ILIKUWA FURSA YA KUJITAMBULISHA KWAO NA KUKUZA IMANI YAO NA KUJIFUNUA KWA KIWANGO KINGINE; Kumponya Lazaro Kwenye Ugonjwa Lilikuwa Hitaji Lao La Kwanza, Na Yalikuwa Maombi Yao Ya Msingi, Lakini Mungu Aliwaza MUUJIZA MKUBWA ZAIDI, YAANI KUFUFUA MAITI ILIYO KABURINI KWA SIKU NNE!
Ni Sawa Na Mimi Na Wewe Tunavyoomba Na Kupeleka Mahitaji Yetu Kwa Mungu Tukidhani TUMEOMBA MEMA NA MAKUBWA, Kumbe Yeye ANAWAZA MEMA NA MAKUBWA Kuliko Tuombayo Na Tufikiriyo!
Kwa Watu Wa Bethania Kifo Cha Lazaro LILIKUWA JANGA, Bali Kwa Mungu ILIKUWA FURSA!

Ni Vema Ukue Toka Kwenye Kiwango Cha KUMWAMINI TU MUNGU, Uingie Kwenye Kiwango Cha KUMJUA MUNGU NA NJIA ZAKE, Ya Kuwa ANAYO MASULUHISHO MAKUBWA NA YA KUDUMU NA YA KUSHANGAZA KULIKO TUWEZAVYO KUOMBA NA KUTAMANI!

“Mungu Anabaki Kuwa Mungu Hata Asipojibu Maombi Yako Sawa Na Ulivyomwomba Au Kumtarajia” (Mwl Mwakasege).

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: