Kati ya Tabia ambazo shetani na Mapepo

Kati Ya Tabia Ambazo SHETANI NA MAPEPO Wanazo Ni “KUTOJUA WAPI WANAKWENDA” Yaani Wao “KILA NJIA INAYOTOKEA MBELE YAO NI NJIA SAHIHI, WANAIFUATA” Yaani Hawana “KITUO MAALUMU” Cha Waendako; Wao Wako Kwenye Safari Zisizoeleweka Mwisho Wake!
Kwenye Kitabu Cha Ayubu Mungu Alimuuliza Shetani, “UNATOKA WAPI?” Naye Akajibu, “NATOKA KUZUNGUKA HUKU NA HUKO NA HUMU”
Yaani Kwa Lugha Nyepesi, “MIMI NILIKUWA NAFUATA KILA NJIA NILIYOIONA; SIKUWA NA SEHEMU MAALUMU YA KWENDA; WALA SIKUWA NA MALENGO YA SIKU; NILIKUWA NAZURURAZURURA TU BILA MPANGILIO WALA MALENGO”

Na Hainishangazi Kuona Kuna Watu WAPOWAPO TU; Hawana Ratiba Wala kusudi Ama Mpangilio Wa Siku Yao Au Mambo Yao; Bila Kuwauliza Hawa Watu Lazima Utawakuta “WANATENDA DHAMBI NA UOVU MAISHANI MWAO” Maana Yeyote “ASIYEKUWA NA MAONO HANA UWEZO WA KUJIZUIA”
Ni Kawaida Ya Shetani Na Mapepo, “KUZUNGUKA HUKU NA HUKO” Ila Si Kawaida Ya Mungu, Malaika Wala Watu Wa Mungu KUISHI BILA MALENGO AU MIPANGILIO!
Badili Huo Mfumo Wa Maisha Maana UNAZALISHA DHAMBI, UOVU NA UMASIKINI KWENYE MAISHA!
MUNGU NI MUNGU WA UTARATIBU; VIVYOHIVYO NDIVYO WALIVYO WALE WALIO WAKE HAPA DUNIANI WALIONUNULIWA KWA DAMU YA YESU.

Mungu Aliyaanzisha Maisha Yakiwa Ni MFUMO MAALUMU Unaowakubali Na Kuwapokea WENYE MIPANGO, MALENGO, UTARATIBU NA MAKUSUDI; Wote Wanaoishi Bila Haya, Maisha Huwa YANAWATAPIKA!
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
3 comments on “Kati ya Tabia ambazo shetani na Mapepo
 1. Novic BCvm says:

  Amina nimejifunza:
  Mimi kama mwana wa Mungu napaswa kuwa na tabia za Mungu kwa maana nimeumbwa kwa mfano wake.

  Kutoenda kwa mipango,maono na malengo ni kuiga tabia zisizonihusu
  Jehova awabariki.

  #Novic /BCvm

 2. Yusha says:

  Amin,nimebariiwa na somo .

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: