Kauli zetu zitakua Mamlaka ya Mwisho

paulo

Unajua, Mungu Anatamani Tufikie Hatua Katika Kumjua Yeye Ambapo “KAULI ZETU” Zitakuwa “MAMLAKA YA MWISHO”!
Petro Alimwambia Yule Kiwete Kwenye Mlango Wa Mzuri, “FEDHA SINA WALA DHAHABU; BALI NIKUPACHO NDICHO HIKI…. KWA JINA LA YESU SIMAMA NA UENDE”
Angalia Hakusema, “Nitamwambia Yesu Aje Afanye Hicho” Au “Nitamwomba Yesu Aje Akupe Uwezo Wa Kutembea” Bali Alisema, “NIKUPACHO NDICHO HIKI…” Kwa Lugha Nyepesi, YEYE NDIYE ALIYEKUWA NA UAMUZI WA YULE MTU KUINUKA PALE AU KUENDELEA KUBAKI PALE…. Alijua MAMLAKA ALIYONAYO “NDANI YA YESU” Kupitia “NGUVU YA JINA LA YESU” Na “AKAAMUA [YEYE PETRO] KUUFANYA ULE MUUJIZA” Maana Alijua “NI MAPENZI YA MUNGU YULE MTU KUPONYWA”!

Unamkumbuka Petro Na Yule Mchawi ELIMA Aliyekuwa Anatumia Uchawi Wake Kujaribu Kuwazuia WATU WASIELEWE INJILI Aliyokuwa Akiwahubiria…. Petro Alipogundua Nani “ANATIA KAUZIBE” Aliamua Kumpa “ADHABU YA KUWA KIPOFU SAA ILEILE”…. Aina Ya Adhabu Na Muda Gani Itokee ALICHAGUA PETRO; Alijua ALICHOBEBA NDANI YAKE, ALIELEWA MAMLAKA YAKE NDANI YA KRISTO; Na Alijua Si Mapenzi Ya Mungu UCHAWI Kushindana Na INJILI… akaamua nini cha kufanya Kadri Ya Alivyotaka Saa Ileile!

Unamkumbuka Paulo Na Yule Kijakazi Aliyekuwa Na Pepo Wa Utambuzi? Yule Binti Alikuwa Mara Kwa Mara Akiwaona Anawaambia, “HAWA NI WATUMISHI WA MUNGU ALIYE JUU” Lakini Paulo Alipogundua Kuwa Anayesema Ndani Ya Yule Binti Ni Pepo; ALIAMUA NINI CHA KUMFANYA, NA SAA ILEILE AKAMWAMURU AMTOKE!
Paulo Alijua Nafasi, Mamlaka Na Nguvu Yake Ndani Ya Kristo Yesu!

Kila Walichokuwa Nacho Petro, Paulo Na Watumishi Wengine Wa Mungu Kwenye BIBLIA, Nawe Mkristo Uliyeokoka Unacho; Ila Kwakuwa Hujui THAMANI NA UKUBWA WA ULICHOBEBA NDANI YAKO, Ndiyo Maana UNAISHI CHINI YA KIWANGO!
Unadhani Wako Watu Maalum Wa Kufanya Mambo Yatokee, Si Kweli… Kila Aliyenunuliwa Kwa Damu Ya Yesu ANA UWEZO WA KUFANYA MAMBO YATOKEE; Unakosa UJASIRI NA KUCHUKUA HATUA, Ila Miujiza Ingetokea Na Kukufuata!

“KITABU CHA MATENDO YA MITUME KILIANDIKWA KWA KUWA MITUME NA KANISA LA KWANZA WALITENDA”
(Nukuu Toka Kwa Smith Wigglesworth).

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
9 comments on “Kauli zetu zitakua Mamlaka ya Mwisho
 1. consesa jackson says:

  barikiwa sana

 2. Yusha says:

  Amen,pia ingependeza kama mungeweza kuwa munatia haya za biblia kwa kutuelewesha vizuri,nina omba si shurtishi,hayo maandiko yanaweza kutusaidia kuwafunza wengine.please.

 3. mtage says:

  ubarikiwe sana nashukuru kwa huu ujumbe kwa kweli nimepata kitu kikubwa sana.

 4. Yusha says:

  Ninaomba nitumieni haya(vesi)za hili somo please.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: