Kufanikiwa au kushindwa

the way you think determines the way you look

Kabla Ya Mtu Yeyote Kufanikiwa Au Kushindwa Kwenye Maisha, Lazima Kwanza Ashindwe Ama Afanikiwe “KWENYE MTAZAMO WAKE”… Wote TUNATAZAMA MAMBO NA VITU Kwa “MACHO HAYA MAWILI YA NYAMA”, “MACHO YA AKILI ZETU” Na Pia Wapo Wanaotazama Kwa “MACHO YA NENO LA MUNGU”….Wote Hawa Wana “MITAZAMO” Ambayo Kila Mmoja Kwa Namna Yake “YUKO SAHIHI” Lakini Haimaanishi USAHIHI WAKE Utakuwa USAHIHI WA “USAHIHI HALISI”
Wapelelezi 10 Waliokwenda Kuipeleleza NCHI YA AHADI Walirudi Na Majibu Kutokana Na “MTAZAMO WA MACHO YA NYAMA NA MACHO YA AKILI ZAO” Wakasema “SISI TU MAPANZI NA WALE WENYEJI WA NCHI NI MAJITU; HATUWEZI HATA SIKU MOJA KUIRITHI NCHI YA AHADI”
Lakini Wapelelezi Wawili, Joshua Na Kalebu Walipoona “MTAZAMO WA MACHO NA AKILI UNAWANYIMA FURSA YA KUINGIA NCHI YA AHADI; WALIAMUA KUTAZAMA KWA JICHO LA AHADI YA MUNGU [NENO LAKE ALILOMWAMBIA IBRAHIMU KUWA WAJUKUU ZAKE WATAIRITHI KANAANI]; MARA MAJITU YAKAWA CHAKULA NA WAO WAKAONA FURSA YA KUINGIA KANAANI”
Mwisho Wa Siku Wale 10 Waliishia JANGWANI Halafu Joshua Na Kalebu Waliingia NCHI YA MAZIWA NA ASALI!

Ukiona Macho Ya Nyama Na Macho Ya Akili “YANAKUNYIMA UWEZO WA KUPENYA” Usiuchukue Huo MTAZAMO Bali Achana Nao; Chukua MTAZAMO SAHIHI WA MACHO YA MUNGU; AHADI YAKE KATIKA NENO LAKE!

“Mtu Hataishi Kwa Mkate Tu, Bali KWA KILA NENO LITOKALO KINYWANI MWANGU, Asema BWANA” (Kumbukumbu 8:3).

“Kama Mvua Ishukavyo Toka Mbinguni Kuja Kwenye Ardhi Na Kuchipusha Mazao Yake, Na Kumpa Mwenye Njaa Chakula, Na Mwenye Kupanda Mbegu; Vivyo Hivyo Ndivyo Lilivyo NENO LANGU; HALITANIRUDIA BURE, BALI LITATIMIZA KILA KUSUDI NILILOLIAGIZA”

(Isaya 55:10-11).

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo
4 comments on “Kufanikiwa au kushindwa
  1. Yusha says:

    Amin,Mungu akubariki mtumishi kwa neno hili,yaani lina niweka sawa kabisa.

  2. […] Kufanikiwa au kushindwa (yesunibwana.org) […]

  3. […] Kufanikiwa au kushindwa (yesunibwana.org) […]

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: