Ufalme wa Mungu unakaa ndani yetu

Nguvu ndani yetu

Kuwa Na Yesu Ndani Yako Ambaye “HAUMTUMII” Ni Sawa Na Kuwa Na MGODI Ambao Hauchimbwi Na Kuzalisha MADINI…. Mmilki Yeyote Wa MGODI Asiyechimba MADINI Atakuwa Masikini Japo Anamilki UTAJIRI!
Hivi Ndivyo Walivyo WAKRISTO WENGI WA KIZAZI HIKI; Hawajui Ndani Yao Yumo “YESU YULEYULE ALIYEFANYA INJILI ZA MATHAYO, MARKO, LUKA NA YOHANA ZIANDIKWE” Na Wanakuwa “MASIKINI WA UHALISI WA YESU HUYO WALIYEMBEBANA WANAYEMMILKI KIHALALI KUPITIA ZAWADI YA WOKOVU”
Usiwe Mkristo Jina; Thibitisha Kwa DUNIA YAKO Kuwa “UFALME WA MUNGU UNAKAA NDANI YAKO”
Mruhusu Mungu ATOKEZE NJE; Na Hiyo Itatokea Pale Utakapochukua Hatua Ya Kumruhusu Roho Mtakatifu ATAWALE Roho Yako [Utu Wako Wa Ndani], Nafsi Yako [Sehemu Yako Ya Akili, Maamuzi Na Utashi] Pamoja Na Mwili Wako [Ambao Pasipo Yesu Kupewa Ruhusa Unakuwa Na Uadui Dhidi Ya Mapenzi Ya Mungu]!
Na Ruhusa Kwa Roho Mtakatifu Inatolewa Kwa Wewe Kuwa Na Muda Wa Kutosha KUJIOMBEA “Yesu Aumbike Ndani Yako” Na Pia, “Mungu Akufungulie Ukurasa Mpya Kila Siku Katika Kumjua Yeye” Lakini Pia Pata Muda Wa Kusoma NENO Walau SURA MOJA (Chapter) Kwa Siku; Na Pia Weka Bidii Kusoma Vitabu Mbalimbali Vya Watumishi Mbalimbali Wa Mungu Vitakusogeza Kwa Kiwango Kikubwa Sana!

Haya Ninayokuwekea Hapa Nayafanya; Na Nimeona Matokeo Yake, Sikufundishi Nisichotenda: Yatendee Kazi Yatageuza Maisha Yako Jumla.

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “Ufalme wa Mungu unakaa ndani yetu

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: