Huu ndio ukweli wa Mungu aliye Juu

Huu ndio ukweli

Huu Ndio Ukweli Wa Mungu Aliye Hai Juu Ya Kila Mwanae Aliyemnunua Kwa Damu Ya Thamani Ya Yesu;
“MAPENZI YA MUNGU [MATAKWA NA FURAHA YAKE] HAYAWEZI KUKUPELEKA MAHALI AMBAKO NEEMA YAKE HAIWEZI KUKULINDA”

Mapenzi Ya Mungu Yalimpeleka YUSUFU Misri Utumwani Kwa Potifa; Neema Ya Mungu Ikampa Kibali Cha Kuwa Kiongozi Na Msimamizi Wa Mali Zote Za Potifa.
Mapenzi Ya Mungu Yalimfanya Atunze Utakatifu Wake Mbele Ya Mke Wa Potifa Na Kuishia Kutupwa Gerezani; Neema Ya Mungu Ilimpa Kuwa NYAMPARA/ KIONGOZI WA WAFUNGWA Na Hatimaye Kuwa WAZIRI MKUU WA MISRI!

Mapenzi Ya Mungu Yalilipeleka Taifa La Israel Utumwani Misri; Lakini Neema Ya Mungu ILIWATOFAUTISHA NA WAMISRI WAKATI WA MAPIGO… Wamisri Walipokuwa Gizani, Waisrael Walikuwa Nuruni. Wamisri Walipokuwa Wakiteswa Na Vyura, Chawa, Panzi Nakadhalika Haikuwa Hivyo Kwenye KAMBI YA WAISRAEL Kule GOSHENI… Wamisri Walipofiwa Na WAZALIWA WAO WA KWANZA; Neema Ya Mungu Iliwatunza Wazaliwa Wa Kwanza Wa Israel Kwa DAMU YA PASAKA!

Unapokaa Kwenye Mapenzi Ya Mungu; Utapata Changamoto Kama Watu Wengine Wote, Lakini NEEMA YA MUNGU Itakuwepo KUKUTOFAUTISHA WEWE NA WAO.
Daniel Alipata Changamoto Ya Kuingizwa Kwenye TUNDU LA SIMBA Kwa Sababu Ya Mapenzi Ya Mungu Lakini NEEMA YA MUNGU Iliwaamuru MALAIKA WAFUNGE VINYWA VYA SIMBA (Danieli 6).

Shedraka, Meshaki Na Abednego Walifikia Hatua Ya “KUTUPWA MOTONI” Kwa Sababu Ya Mapenzi Ya Mungu, Lakini Mwisho Wa Siku, NEEMA YA MUNGU Iliwatunza “HATA UNYWELE WAO HAUKUUNGUZWA NA ULE MOTO ULIOKOLEZWA MARA SABA ZAIDI YA MOTO WA KAWAIDA” Badala Yake “MTU WA NNE” Aliwatokea Huko (Danieli 3).

Mapenzi Ya Mungu Yalimpeleka Ayubu MIKONONI MWA SHETANI, Akateswa, Akajaribiwa, Akapoteza Mali Zake, Akapoteza Watoto Wake Na Hata Afya Yake; Lakini NEEMA YA MUNGU Ilimsaidia ASIMKANE MUNGU Na Hatimaye “MWISHO WAKE UKAWA MWEMA NA MKUU MNO KULIKO MWANZO WAKE”

Unapokuwa Umesimama Kwenye MAPENZI YA MUNGU; “KUMI ELFU WATAANGUKA MKONO WAKO WA KUUME NA ELFU KUSHOTO KWAKO LAKINI HAUTAANGUKA WEWE, BALI KWA MACHO YAKO UTATAZAMA NA KUYAONA MALIPO YA WASIO HAKI” (Zaburi 91).

Unapokuwa Umesimama Kwenye MAPENZI YA MUNGU, Utapata Mtikisiko Na Changamoto Lakini Mwisho Wa Siku Utasema Kama Daudi; “WAO WAMEINAMA NA KUANGUKA BALI SISI TUMEINUKA NA KUSIMAMA” (Zaburi 20:8).

Ni Uamuzi Wako UDUMU KWENYE MAPENZI YA MUNGU [Hata Kama Yanakuumiza] Ili NEEMA YA MUNGU Pia Iwe Nawe, Ama Uyakwepe Na Kutenda Kinyume Na NENO LAKE Kisha UIPOTEZE NEEMA YAKE! <

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: