Mungu anapatikana Mahali Pa juu

Ninajua Kitu Kimoja KIKUBWA SANA, Nacho Ni Hiki; MUNGU Anapatikana Na Kufanya Kazi Kwenye “MAHALI PA JUU” Na Ukitaka Kukutana Naye, Kukutana Na Baraka Zake, Sauti Yake, Uwepo Wake, Nguvu Zake Na Kila Alilonalo, LAZIMA Uamue “KUPANDA JUU ALIKO”
Zaburi 91:1 Inamwita, “ALIYE JUU” Na Pia Ukisoma Waefeso 2:4-6 Inasema TULIPOOKOLEWA KWA DAMU YA THAMANI YA YESU KUPITIA UPENDO NA REHEMA NYINGI ZA MUNGU, ALITUKETISHA “JUU SANA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO PAMOJA NA BWANA YESU”, Na Huko “JUU SANA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO” Ni Mahali Pa USALAMA, UTELE NA UTOSHELEZI Ambako Ni JUU SANA; JUU Ya Falme Zote, JUU Ya Mamlaka Zote, Juu Ya Kila Usultani, Juu Ya Kila Jina Litajwalo Katika Ulimwengu Huu Wa Sasa Na Ule Ujao (Waefeso 1:19-22).
Na Mtu Yeyote Ambaye MUNGU Amemkubali Na Kumfanikisha, Ni Lazima Kwanza Mungu “AMWEKE JUU TU NA WALA SIO CHINI KABISA” (Kumbukumbu 28:13).
Njia Rahisi Ambayo Mungu Ameiweka Ambayo Inaweza Kumfanya MWANADAMU WA KAWAIDA Aweze Kuja Na Kufika “JUU SANA ALIKO” Ni Kwa Mtu Kumwamini Na Kumpokea Yesu Kama BWANA NA MWOKOZI WAKE, Yaani Kuokoka, Akishaokoka Na Kumpata Yesu, Huyu Mtu “ANAKETISHWA JUU SANA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NA MUNGU” (Waefeso 2:4-6, Waefeso 1:19-23).
Na Kitu Pekee Kitakachomfanya MTU ALIYEOKOKA Kuendelea “KUWA JUU, KWENYE UWEPO WA MUNGU” Ni Kwa Yeye “KUISHI NA KUTENDA SAWA NA NENO LA MUNGU” Maana “NENO LA MUNGU LIKO JUU SANA, AMELIKUZA KULIKO HATA JINA LAKE” Na Ndiyo Maana Katika Isaya 55:10-11, Analifananisha Na MVUA “ISHUKAYO” Toka Mbinguni Kuja Ardhini. Na Kama “LINASHUKA” Kuja Kutimiza Makusudi Ya Mungu, Maana Yake “NENO LIPO JUU SANA NDIO MAANA HUWA LINASHUKA”
Ukiwa Mtu Anayeishi Na Kutenda Sawa Na NENO; MAWAZO YAKO NA NJIA ZAKO ZINAKUWA “JUU SANA KAMA MBINGU” (Isaya 55:8), Maana NENO LA MUNGU NI MUNGU, NA PIA NI MAWAZO YA MOYO WA MUNGU; YAKO JUU SANA KULIKO MAWAZO YA WANADAMU WA KAWAIDA!
Biblia Inatuhimiza “KUYATAFAKARI YALIYO JUU” Na Kamwe Tusiyatafakari YALIYO CHINI KATIKA NCHI (Wakolosai 3:1-3).
Namna Pekee Ya Wewe KUENDELEA “KUYATAFAKARI YALIYO JUU” Ni Kwa Wewe Kulipima Kila Wazo Na Fikra Kama Iko Sawa Na “NENO LA MUNGU”…Yale Yote Yasiyo Mema, Yasiyo Na Staha, Yasiyokuwa Na Usafi Ndani Yake, Yasiyokuwa Na Sifa Njema “YAKWEPE” Maana “YATAKUPOROMOSHA TOKA JUU KURUDI CHINI TENA” (Wafilipi 4:8).
Pia Ili “UENDELEE KUKAA JUU KWENYE UWEPO WA MUNGU” Lazima Uwe Mtakatifu Maana “PASIPO HUO, HAUWEZI KUMWONA MUNGU SASA KATIKA MAISHA HAYA NA MILELE MBINGUNI” (Waebrania 12:14).
DUMU KATIKA MAOMBI NA SALA; TUNZA UWEPO WA MUNGU, KAA JUU!

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: