Mambo yatakayokufanya uwe na furaha wakati wote kama Mkristo wakati wenzako wote wanalia!

Kuna Watu Wanadhani Mungu Anafurahi Au Anawapenda Zaidi Wakiwa Wanapita Kwenye MAGUMU AU MASIKITIKO; Hizi Ni Fikra Mgando, Si Kile Neno La Mungu Limesema Kuhusu Mungu Wangu Wa Biblia!
Yeye ANACHOKIPENDA KILA SIKU NI KUONA MKRISTO AKIWA AMEJAA FURAHA KILA SEKUNDE.
Ndiyo Maana Anatuhimiza Kuwa Na Furaha Muda Wote;
“FURAHINI KATIKA BWANA SIKU ZOTE, TENA NASEMA FURAHINI” (Wafilipi 4:4).
Anataka Tufurahi “KATIKA YEYE” Siku Zote: Hii Ina Maana Kila Aliyeokoka [ALIYE KATIKA YEYE] Amepewa “ZAWADI YA FURAHA NA SABABU YA KUFURAHI SIKU ZOTE”
Mimi Sielewi Inakuwaje Unafikia Wakati Wa Kusahau Ukweli Huu Na Kuweka JICHO LAKO Kwenye MATATIZO, CHANGAMOTO, UHITAJI, KUPUNGUKIWA Nakadhalika Kiasi Cha Kupoteza FURAHA AMBAYO “YESU ALIKUNUNULIA NA KULIPIA MSALABANI” Maana Imeandikwa Wazi Ya Kuwa, “HAKIKA [NI KWELI NA SI UONGO] YEYE [YESU] AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU NA AMEJITWIKA HUZUNI ZETU” (Isaya 53:4), Mimi Sielewi Kwanini Unatega SIKIO KWA DUNIA NA KUFUNGUA JICHO LAKO KWA HALI YAKO NGUMU BADALA YA AHADI NA KWELI ZA NENO LA MUNGU; Wote Wanaoshi Kwa Kukubali Na Kupokea Kile Yesu Amewafanyia, “WANAISHI MAISHA YA RAHA NA YA JUU” Bila Kujali “HALI YAO YA NJE INAONEKANAJE AU INASEMAJE”

Anachokipenda Mungu Kwa Watoto Wake Ni Hiki;
“FURAHINI SIKU ZOTE…OMBENI BILA KUKOMA…SHUKURUNI KWA KILA JAMBO; MAANA HAYO NDIYO MAPENZI YA MUNGU KWENU KATIKA KRISTO YESU” (1 Wathesalonike 5:16-18).
Mungu Anataka TUFURAHI SIKU ZOTE; Lakini Anatufundisha Na Mambo Yatakayoifanya FURAHA YETU ISIONDOKE MAISHANI MWETU!

Mambo Yatakayokufanya UENDELEE KUWA NA FURAHA MAJIRA YOTE, BILA KUJALI UNAPITIA WAKATI GANI AU JAMBO GANI NI;

1.KUOMBA BILA KUKOMA
Watu Ambao Wana Tabia Ya Kukaa KWENYE MAOMBI, Wenye Muda Wa Kutosha Na Mungu; Ambao HUPELEKA MAGUMU NA CHANGAMOTO ZAO KWA MUNGU NA KUMTWIKA FADHAA ZAO, SIKU ZOTE UTAWAKUTA WAKIFURAHI, MAANA WANAJUA “KESI ZAO ZINAJULIKANA MBINGUNI NA MUNGU ANAZISHUGHULIKIA”
Hivyo Muda Wote WAMEJAA IMANI NA MATUMAINI AMBAYO HUINUA FURAHA NA CHANGAMKO MIOYONI MWAO!
Yesu ALIHUSIANISHA “KUKOSA FURAHA KAMILIFU NA KUTOOMBA KWA JINA LAKE” Naye Anasema Hivi:
“HATA SASA HAMJAOMBA KITU CHOCHOTE KWA JINA LANGU; OMBENI NANYI MTAPATA, ILI FURAHA YENU IWE KAMILI” (Yohana 16:23-24).
Hapa Yesu Anatufundisha Na Kutufunulia Kitu Cha Ajabu Mno, Na Kitu Hicho Ni Hiki; “MUNGU YUKO TAYARI KUJIBU OMBI LAKO UTAKALOMWOMBA KWA JINA LA YESU ENDAPO KUJIBU KWAKE OMBI LAKO KUTASABABISHA WEWE UPATE FURAHA KAMILIFU”
Angalia Hapa, Hasemi FURAHA TU, Bali “FURAHA KAMILIFU” Na Ni Kweli Kuwa Kuna Maombi Yako Mengi “MUNGU HAJAYAJIBU KWA KUWA HAYAKUPI FURAHA YA KUDUMU/ FURAHA KAMILIFU” Bali Ni Ya Kukufurahisha Kwa Muda Tu Na Mwisho Yataleta Huzuni Tena!
MUNGU HATAJIBU OMBI LAKO KAMA HAONI MWISHO WA KUJIBIWA KWAKO “ITAKUPA FURAHA KAMILIFU”
Haimsumbui Mungu Kutojibu Ombi Lako Hasa Kama Limelenga FURAHA YA MUDA MFUPI NA SI FURAHA KAMILIFU!

2.SHUKURUNI KWA KILA JAMBO
Jambo La Pili Na La Muhimu Sana Litakalokusaidia Kuwa Na Furaha Kamilifu Maishani Mwako Ni KUJIJENGEA TABIA YA KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO LINALOTOKEA MAISHANI MWAKO; Bila Kujali Ni Zuri Au Baya, Unalipenda Ama Hulipendi, Unalifurahia Ama Hulifurahii!
Ni Muhimu Ujue Kuwa “MUNGU ANAKUWAZIA MAWAZO MEMA NA YA AMANI NA SI MAWAZO YA MABAYA” (Yeremia 29:11). Pia Ni Muhimu Ujue Ya Kuwa, “HASINZII WALA HALALI KWA AJILI YAKO” (Zaburi 121:3-8). Ni Muhimu Pia Ujue Ya Kuwa, “AMEKUCHORA KWENYE KIGANJA CHAKE NA KUTA ZAKO ZI MBELE YAKE DAIMA” (Isaya 49:16). Amekuhakikishia Kuwa “KILA AKUGUSAYE ANAIGUSA MBONI YA JICHO LAKE” (Zekaria 2:8). Na Amekuhakikishia “ATAKUWA PAMOJA NAWE TAABUNI; ATAKUOKOA NA KUKUTUKUZA” (Zaburi 91:15).
Sasa Kama Haya Ndiyo Mawazo ya Mungu Kwako, Unadhani Likitokea LOLOTE BAYA, LINALOUMIZA HALIONI? Si Kweli Anaona Kila Kinachokujia Chema Ama Kibaya; Amekiruhusu Ukipitie “KWA MUDA TU” Kama “DHAHABU IPITAVYO MOTONI” Na Wala “HATORUHUSU UJARIBIWE ZAIDI YA IMANI YAKO” Bali Atakuwepo Kukusaidia Na Kukuonesha WOKOVU WAKE Kama “DANIEL KWENYE TUNDU LA SIMBA” Ama “AKINA SHEDRAKA KWENYE TANURU YA MOTO”… Kwakujua Yote Haya “KUHUSU MUNGU WAKO NA UPENDO WAKE KWAKO” Utakuwa Na Sababu Ya Kumshukuru Mungu Kwa Kila Jambo Na Hautaruhusu AMANI YAKO NA FURAHA YAKO ICHUKULIWE NA MAZINGIRA MAGUMU UNAYOPITIA!
Lexie Semsela Soma Hii Na Pia Mpe Mama Naye Apitie Ni NENO LA MUNGU KWENU.

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
5 comments on “Mambo yatakayokufanya uwe na furaha wakati wote kama Mkristo wakati wenzako wote wanalia!
 1. Flora Fabian says:

  asante mtumishi wa Mungu aliye hai,hili nimelifanya kwa vitendo nimemwona Bwana. Mungu akubariki saaana.

 2. Evodius yohana says:

  NMEBARKIWA SANA MTUMISH MUNGU AKUBARK

 3. Evodius yohana says:

  Mtumishi tangu nmetambua hili naish kwa furaha sana siku zote mpaka watu wananishangaa somo hili limenivusha ng’ambo thank you holy sprit for your servant i pray for your ministry

 4. Essau James. says:

  Ubarikiwe sana mtumishi…!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: