Kuuishi kwa Imani kuunahusisha pia Mahitaji yako

Imani

Kuishi Kwa Imani Kunahusisha Pia MAHITAJI YAKO MUHIMU Kama Vile KULA, KUNYWA, KULALA NA MAVAZI; Kuishi Kwa Imani Hakuhusishi MAMBO YA ROHONI TU Bali MAMBO YA KAWAIDA YA KILA SIKU.
Bwana Yesu Anatufundisha Kitu Kuhusu “KUISHI KWA IMANI KATIKA MAHITAJI YA MUHIMU YA KILA SIKU” Naye Anasema Hivi;
“MSISUMBUKIE MAISHA; MKISEMA TUTAKULAJE,AU TUTAVAAJE. JE UZIMA/ UHAI SI BORA KULIKO CHAKULA NA MWILI JE SI BORA KULIKO MAVAZI? MWAWAONA NDEGE WA ANGANI? HAWANA SHAMBA, HAWAPANDI NA WALA HAWALIMI LAKINI MUNGU HUWALISHA; MWAYAONA MAUA YA KONDENI? HAYAFANYI CHOCHOTE LAKINI MUNGU HUYAVIKA NA KUYATUNZA; HATA SULEIMANI KATIKA FAHARI YAKE YOTE HAKUWAHI KUTUNZWA KAMA MOJAWAPO LA HAYA MAUA. IKIWA MUNGU HUWATUNZA NDEGE WA ANGANI NA MAUA YA KONDENI, JE SI ZAIDI NINYI WA IMANI HABA? MSIJUSUMBUE BASI KWA KUWA HATA MATAIFA [WASIO NA UHUSIANO NA MUNGU KAMA BABA YAO] HUYATAFUTA HAYO; NI VEMA KUJUA YA KUWA BABA YENU WA MBINGUNI ANAJUA YA KUWA MNAYAHITAJI HAYO; BALI UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE, HAYA MENGINE YOOOTE MTAZIDISHIWA” (Mathayo 6:25-33 Ikiwa Na Msisitizo Wa Mwalimu)

NI MUHIMU UJUE HAYA YAFUATAYO:
1.Mungu Anajua Kuwa Unahitaji KULA VIZURI, KUNYWA VIZURI, MAKAZI MAZURI NA MALAZI MAZURI (Mstari Wa 32).

2.Yesu Anasema IMANI Ndio Ufunguo Wa Wewe Kupata CHAKULA KIZURI, KINYWAJI KIZURI, MAKAZI MAZURI NA MALAZI MAZURI. (Mstari Wa 30).
Yaani USIPOMWAMINI MUNGU Kwamba “Kama Analisha Ndege Wa Angani Ambao SI WATOTO WAKE Kama Mimi Nilivyo Kupitia Kristo Yesu, Basi HAKIKA Atanitunza Mimi Na Kunipa Kila Kitu Kuliko Ndege Wa Angani Maana Thamani Yangu Kwake Ni Kubwa Kuliko Ya Ndege Au Maua Ya Kondeni”
USIPOKUWA NA IMANI HII; NA KUAMUA “KUWA TEGEMEZI” KWA MUNGU, HAUTAWEZA KUPATA “MAHITAJI YAKO KWA NJIA YA IMANI”
Katika Mstari Wa 30 Yesu Anatuonesha Kuwa KITU PEKEE Kinachozuia Wakristo Wasipokee MAHITAJI YAO YA KILA SIKU NA YA KAWAIDA Ni “KUWA NA IMANI HABA”… Uhaba Wa Imani Unamfungia Mungu Mlango Wa Kukupa Chakula, Mavazi, Malazi Nakadhalika!

3. Mungu Anataka UTHAMINI Kwanza UHAI/ MAISHA Kuliko CHAKULA, Na MWILI WAKO Kuliko MAVAZI (Mstari Wa 25).
UHAI/ MAISHA Ndiyo Yanayopelekea CHAKULA Kiwe Na Thamani; WALIOKUFA Huwa HAWALI… Thamini Kwanza UHAI/ MAISHA Kwanza Kama Unataka Mungu Akupe Chakula.
Thamini Kwanza MWILI WAKO Kwanza Kuliko MAVAZI; Mavazi Yamepata THAMANI Kwa Sababu Ya Uwepo Wa Mwili Unaovaa Nguo!
Inakubidi Uwe Na Mfumo Sahihi Wa Kifikra Kuweza Kujua VIPAUMBELE Kwenye Maisha Ili Ufanikiwe; UHAI KWANZA Halafu Chakula Pia MWILI KWANZA Halafu Mavazi…. Mshukuru Mungu Kwanza Kwa Uhai/ Maisha Kama Unataka Akupe Chakula… Mtukuze Mungu Kwakuwa Na Mwili Unaoweza Kupokea Mavazi!

4.Hakikisha Unatafuta Kwanza UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE Halafu Haya Mahitaji Yatakuja Bila Hata Kuyawekea Nguvu Na Muda Mwingi (Mstari 33).
-Uwe Na Muda Mwingi Wa kudumu Na Mungu (Kwenye Ushirika Na Mungu, Kupitia Maisha Yako Ya Kila Siku; Yote Utendayo Kwa NENO NA KWA TENDO Yatende KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU, Kwa Kuzingatia HAKI YA MUNGU, MAPENZI YA MUNGU NA SAWA NA NENO LAKE LILIVYOAGIZA).
-Ufalme Wa Mungu Ni FURAHA, AMANI NA HAKI KATIKA ROHO MTAKATIFU (Warumi 14:17).
Anaposema Tafuta Ufalme Wa Mungu Kwanza Maana Yake Kabla Ya Kuwaza ULE NINI, UVAE NINI AMA ULALE WAPI; Kwanza Tafuta FURAHA YA KWELI ILIYO KWA MUNGU NA AMANI YA KWELI ILIYO KWENYE MAISHA YA USAFI NA UTAUWA…PIA DUMU KUTENDA HAKI!

Hizi Kanuni Zitakufanya Uwe Na Chakula Kizuri Na Cha Kutosha, Mavazi Mazuri, Nadhifu Na Ya Kutosha, Makazi Mazuri Na Malazi Bomba. Ila Usipotenda Kanuni Zote Bila Kupunguza Hata Moja “UTAISHIA KUSIKIA WEMA WA MUNGU KWA WENZAKO”

Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
4 comments on “Kuuishi kwa Imani kuunahusisha pia Mahitaji yako
  1. lilian kiwelu says:

    May Almight bless u abondantly, huduma yako ikue na kuwafikia wote kwa ukombozi katika Kristo Yesu.

  2. Joshua m makubi says:

    Asante Yesu kwa kusema nami kupitia mtumishi wako!MUNGU azidi kukubariki mtumish,i maana nimebarikiwa sana na ujumbe wa neno hilo.

  3. vicky says:

    I AM REALLY BLESSD WITH YOUR SERVICE…MAY ALMIGHTY GOD BLESS YOU ABUNDANTLY!!!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: