Nikiwa Jangwani Kwenye Semina Ya Baba Yangu

Mwalimu Mwakasege

Wakati Nikiwa Jangwani Kwenye Semina Ya Baba Yangu, Mwalimu Wangu, Darasa Na Kioo Changu Mwalimu Mwakasege; Alizungumzia “SADAKA” Aliyoiita “SILAHA YA VITA” Na Akasimama Na Andiko Toka Zaburi 27:1-10.

Aina Hii Ya Sadaka Ilikuwa MPYA MNO Kwangu; Lakini Nilikuwa Namsikiliza Mwalimu Huku Naendelea “KUNENA KWA LUGHA NDANI YANGU” Halafu Ghafla, Kama “KUFUMBA NA KUFUMBUA” Mungu Aliniletea “PICHA” Ya Nabii Samweli Akiwa Na Wana Wa Israeli, Wana Wa Israeli Wakiwa WANASONGWA NA KUONEWA NA ADUI ZAO WAFILISTI; Halafu Wakiwa Wamejikusanya Pale, Wafilisti Wakapata Taarifa Na Kuja Wakisemezana, “WAISRAELI WAMEJIKUSANYA KULE MISPA NA HAWAJAJIPANGA KIVITA, TWENDE TUKAWAMALIZE KABISA [Lets Finish Them Once And For All]”
Na Wakiwa Wanawazunguka Ili WAWAMALIZE; Walinzi Waliokuwa Eneo La Ibada Wakaleta Taarifa; Taarifa Ilipokuja, Wana Wa Israeli Wakaingiwa Na Hofu, Wakawa Wanamlilia Samweli Kuwa Wanakwenda Kufa, Na Wengine WAKAMSIHI AMLILIE MUNGU WAO, Mungu Wa Ibrahimu, Isaka Na Yakobo…. Halafu Nabii Samweli, Akawatuliza WANA WA ISRAELI, Halafu Wakati Wafilisti Wanajikusanya Na Wanaendelea Kuwazunguka; Samweli AKAMTOLEA BWANA ‘SADAKA YA VITA’ NA AKAAMBATANISHA NA MAOMBI YA KUMSIHI MUNGU ‘AWASHUGHULIKIE ADUI ZAO- WAFILISTI’ Na Maramoja, Bila Kuchelewa, Mungu Akamwitikia; AKAPIGA RADI NA NGURUMO, MSHINDO MKUBWA NA KUWAFADHAISHA WAFILISTI [ADUI] WAKAPIGWA NA KUANGAMIZWA!
Na Ikaja Haraka Ndani Yangu “1Samweli 7:5-13” Ambako Ndiko Kuna Hili Tukio Zima Alilokuwa Ananionesha!
CHA AJABU, HII PICHA NZIMA YA TUKIO LOTE HILI ILIKUJA KAMA NDANI YA SEKUNDE NNE AU TANO TU!!!
Yaani Spidi Ya Mbinguni Kutoa Ufunuo Ni Kubwa Mno Na Ya Haraka Kuliko Kitendo Cha Kuwasha Taa Ya Umeme Kwa Kubofya Swichi!
Nikiwa Njiani Nikiendelea Kutafakari Zaidi Kuhusu SADAKA HII YA VITA [SILAHA YA VITA] Ndipo Tena BWANA Akanisemesha Kitu Kilichopo Kwenye Zaburi 23, “HUNIANDALIA MEZA MACHONI PA WATESI/ ADUI ZANGU” Ambayo Kwa Lugha Nyepesi Inasema, “ANANIPA CHAKULA, BARAKA ZANGU NA HATUA MPYA ZA KIMAISHA HUKU ADUI ZANGU WAKINITAZAMA; WAKITAMANI WANIHARIBIE AU KUNIZUIA LAKINI UWEPO WA MUNGU ULIO JUU YANGU UNAWAFANYA WAISHIE KUNITAZAMA”
Nikawa Nimepata Ufunuo Wa Kutosha Kuhusu “SADAKA YA VITA [SILAHA YA VITA]” Ambayo Mtu Anaitoa, Anaiachilia Kwa Imani [Kadri Ya Vile Alivyosukumwa Ndani Yake], Ili Mungu ‘AMVUSHE’ Dhidi Ya ADUI Wanaojaribu Kumzuia Asiende KIWANGO KINGINE Cha Kimaisha. Wanaweza Kuwa Watu, Tabia Fulani Uliyoiombea Bila Mafanikio, Dhambi, Tatizo La Kifamilia, Kiofisi Ama Kwingine Unakozuiwa Kwenda HATUA/ KIWANGO KINGINE CHA MAISHA Na Adui Unayemfahamu!

Mungu Akutunze,
Tukutane Jangwani Tuendelee Kula MANA Tukue Kiroho.
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: