Uwezo wa Kuzikabili Habari mbaya

Kati Ya Vitu Ambavyo Vinawaua Au Kuwaletea Mateso Wanadamu Ni Uwezo Wa “KUZIKABILI HABARI MBAYA” Au MABAYA Yanapokuja Maishani Mwao!
Wengi Kwa Kutojua Namna Ya Kukabiliana Na Hali Mbaya Na Habari Mbaya Maishani Mwao Zinazowatokea Au Kuwajia, Wamejikuta Wakikwama, Wakishindwa Na Kutoendelea Kwenye Maisha.
Yesu Ametuokoa Ndiyo, Ametupa Uraia Wa Mbinguni, Sawa; Lakini Wakati Anaondoka Alisema, “DUNIANI MNAYO DHIKI” Hakusema “HAMTAPATA NYAKATI MBAYA AMA NGUMU MAISHANI MWENU” Ila Alitwambia Tena, “JIPENI MOYO NIMEUSHINDA ULIMWENGU” Akimaanisha “AMEPATA SULUHISHO JUU YA CHANGAMOTO ZITAKAZOJITOKEZA KATIKA SAFARI YAKO YA MAISHA” Na Majibu Yote Yamewekwa “NDANI YA NENO LAKE”
Kitu Pekee Kitakachokusaidia ZINAPOKUJA HABARI MBAYA Au MABAYA YANAPOJITOKEZA Ni Kutumia Kanuni Za Neno La Mungu Ambazo Wengine Walizitumia Wakiwa Katika NYAKATI MBAYA Au WALIPOKUTANA NA MABAYA… Nazo Ni;

1.Kujua Kuwa Mungu Hasinzii Wala Halali Kwa Ajili Yako; Na Kama Ameliacha Lije Au Litokee Ni Kwa Sababu Ana Njia Ya Kukusaidia Kutoka Salama (Zaburi 121:2-8).

2.Kujua Kuwa Mungu Amakuahidi Kukusaidia; Ukijua Hilo Itakusaidia Kuelewa Kuwa ALILIONA WAKATI LINAKUJA Na Atakuwa Nawe Kukusaidia Uvuke Salama, Hivyo Uhitaji Kukata Tamaa Au Kuvunjika Moyo (Waebrania 13:6, Isaya 41:10).

3.Kujua Kuwa “YESU YUKO PAMOJA NAWE SIKU ZOTE HATA UKAMILIFU WA DAHARI” Hata Kama Humwoni Kwa Macho Yako; Na Kama Yuko Nawe, Atakutetea Na Kukusaidia Katika Hilo Baya Lililojitokeza (Mathayo 28:20).

4.Kujua Kuwa “YESU KRISTO ANAJISHUGHULISHA SANA NA MAMBO YAKO” Na Ya Kuwa Yuko Tayari “KUJITWIKA FADHAA ZAKO” Ikiwa “UTAMTWIKA” (1Petro 5:7).

5.Kujua Kuwa “MUNGU HAPENDI WEWE KUJISUMBUA KWA JAMBO LOLOTE BALI KWA KILA NENO KUSALI, KUOMBA NA KUSHUKURU, HUKU HAJA ZAKO ZIKIJULIKANA NA MUNGU” (Wafilipi 4:6-7).

Lakini Ili Uweze Kuwa Na Mfumo Huu Wa Maisha, Lazima Kwanza Wewe Nawe Uweke Bidii Kujifunza NENO LAKE; KULITAFAKARI NA KULIELEWA VEMA KIASI CHA KULIHAMISHA TOKA KWENYE BIBLIA NA KULIWEKA KWENYE MAISHA YAKO YA KILA SIKU.
Daudi Anasema, ” [MWENYE HAKI] HATAOGOPA HABARI MBAYA; MOYO WAKE U IMARA UKIMTUMAINI BWANA… MOYO WAKE UMETHIBITIKA HATAOGOPA” (Zaburi 112:7-8).
Uimara Wa Moyo Wako Wakati Wa Magumu Unategemea “KIWANGO CHA NENO LA MUNGU ULILOJAZA HUMO”
“NENO LA KRISTO NA LIKAE KWA WINGI NDANI YAKO KATIKA HEKIMA YOTE” (Wakolosai 3:16-17).

Mwl D.C.K

 

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “Uwezo wa Kuzikabili Habari mbaya
  1. Peter says:

    Barikiwa.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: