Maajabu ya damu ya Yesu

damu ya Yesu

MAAJABU YA DAMU YA KUNYUNYIZA YA YESU; OMBA KWA KUTUMIA DAMU YA YESU UTASHANGAA KUPATA MATOKEO YAFUATAYO!

Wakati Waisraeli Wakiwa Utumwani, Mungu Alipiga Pigo La Kumi Na La Mwisho, Lakini Pigo Lilifanyika Kwa Imani Kupitia Damu Ya Kondoo Ambaye Walimpa Jina La Pasaka; Ambaye Kwa Agano Jipya “YESU KRISTO NI PASAKA WETU AMBAYE AMEKWISHACHINJWA”
Walipotumia Damu Ya Yesu Kwa Kupaka MIMO YA MAMALANGO KWA IMANI, Yalitokea Mambo Kadhaa:

1.Wote Waliokuwa Ndani Ya Nyumba Za Waisraeli Zilizopakwa Kwa Damu Ya Pasaka [Damu Ya Yesu Kwa Agano Jipya] HAWAKUPATWA NA MAUTI YA WAZALIWA WA KWANZA WAO.
Ripoti Ya Vifo Vya Wazaliwa Wa Kwanza Wa Misri Haikuwagusa Waisraeli; MHARIBU [SHETANI KWA AGANO JIPYA] Alipopita KUsababisha Vifo Na Mauti, HAKUWEZA KUINGIA KWENYE NYUMBA ZA WAISRAELI!
Ukiitumia Damu Ya Yesu [KWA IMANI LAKINI] Ukaipaka Kwenye MALANGO YA ROHONI YA FAMILIA YAKO; NDUGU ZAKO, WAZAZI WAKO, NA WATU WOTE WA NYUMBA YAKO, SHETANI HATAWEZA KUKATISHA MAISHA YAO WALA MAISHA YA MIFUGO YENU!

2.Waisraeli Walipopaka Damu Ya Kondoo Pasaka [Ambaye Kwa Agano Jipya Ni Yesu] WATESI WAO, YAANI FARAO NA WAMISRI WALIANZA KUWAOMBA NA KUWABEMBELEZA WAONDOKE; SI WAMISRI WALIOOMBA RUHUSA TENA, BALI WAMISRI WALIANZA KUWABEMBELEZA WAONDOKE!
Ukiitumia Damu Ya Yesu Kwa Imani Kwenye Maisha Yako, Familia, Wazazi Na Ndugu Zako; KILA PEPO, JINI, MCHAWI AMA MGANGA ALIYEWAFUNGA WASIFANIKIWE, WASIMCHE MUNGU, WASIOE/ WASIOLEWE, WAWE NA NDOA ZISIZODUMU, WAWE NA MITALA, WAWE NA UCHUMI MBOVU; WANAFANYA KAZI “TEMBO” MATOKEO “SISIMIZI” LAZIMA HAO WALIOWAWEKA UTUMWANI WAANZE KUJA KUOMBA MSAMAHA, KUWASIHI MUONDOKE BURE… Damu Ya Yesu Itawafanya MUWE KAMA MOTO MIKONONI MWA WALIO WAKAMATA; HAWATAWEZA KUENDELEA KUWASHIKILIA; UHURU WA KIROHO, KIUCHUMI, KIMAHUSIANO, NDOA NA MAMBO YOTE YATAKUWA SAWA!

3.Waisraeli Walipopaka Damu Ya Kondoo Wa Pasaka [Ambaye Kwa Agano Jipya Ni Yesu]; Wale Waliowateka Nyara Na Kuwatumikisha WALIGEUKA WATUMWA KWENYE NCHI YAO; Waisraeli HAWAKUONDOKA MIKONO MITUPU, WALIONDOKA NA MALI ZAO ZILIZOKALIWA NA KUZUILIWA NA WATESI WAO WAMISRI!
Utakapoanza KUIAMINI Na Kuitumia DAMU YA YESU KWA AJILI YAKO, FAMILIA, NDUGU ZAKO, NA WATU WAKO; UCHUMI ULIOKWAMA KWA MIAKA MINGI UTAREJEA… UTASHANGAA KIBALI NA UPENDELEO KWAKO, FAMILIA YAKO NA NDUGU ZAKO VIMERUDI KWA SPIDI KUBWA, HATA WALE WALIOKUWA WATEKAJI WATAKUJA KUPIGA MAGOTI KWENU NA KUWAPA UTAJIRI; WEWE NA WATU WAKO MTAWATEKA NYARA WATESI WENU!

4.Wana Wa Israeli Walipopaka Damu Ya Kondoo Wa Pasaka [Ambayo Kwa Agano Jipya Ni Damu Ya Yesu] GHAFLA MSIMU WA MAISHA YAO UKAGEUKA; WAKATOKA MSIMU WA KUWA WATUMWA, WAKAANZA KUWAMILKI ADUI ZAO… WAKATOKA MSIMU WA KUZUIWA KUMTAFUTA NA KUMWABUDU MUNGU WAO NA KUPATA UHURU WA KUMWABUDU MUNGU [HALI YAO YA KIROHO IKAUHISHWA]… WAKATOKA KWENYE MSIMU WA KUWA WAHITAJI, WAKATEKA MALI NA VITU VYA ADUI ZAO [UCHUMI WAO UKABADILIKA]… MSIMU WA MUNGU WAO KUDHARAULIWA NA KUSHUSHWA UKAFUNGWA NA UKAJA MSIMU AMBAO DUNIA NZIMA IKAJUA WANA MUNGU!
Utakapoitumia Damu Ya Yesu Kwa Imani, Utashangaa MISIMU YA NDUGU ZAKO KIMAISHA INAANZA KUGEUKA; WALIOKATAA KWENDA SHULE WATAAANZA KUULIZIA SHULE, WALIOKUWA WAMEZALIA NYUMBANI WATAPATA WAUME NA KUWA NA NDOA ZA KUELEWEKA, WALIOKUWA MASIKINI WA KUTUPWA AKILI ZAO ZITAFUNGUKA NA WATABUNI MAMBO NA MIRADI MIKUBWA NA KUWA NA MAISHA YA MAANA, WALE WALIOKUWA WANAUPINGA WOKOVU WATAOKOKA NA KUYATOA MAISHA YAO KWA YESU…. HAKIKA UTASHANGAA DAMU YA YESU ILIVYOFUNGUA KIWANGO KIPYA NA BORA CHA MAISHA YAO!

Itumie Damu Ya Yesu Kwa Imani, Hakika Itakufanyia Mambo ya Ajabu,
Utabaki Ukiisifu Na Kuitukuza Damu Ya Mwanakondoo Wa Mungu!
Weka Masomo Haya Kwenye Matendo Na Ulete Ukombozi Kwenye Maisha Yako, Wazazi Na Ndugu Zako!

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo
3 comments on “Maajabu ya damu ya Yesu
  1. ELIA KONGA says:

    AMINA

  2. GERALD MGANWA says:

    NI.KWELI KATIKA DAMU YA YESU KUNA MAAJABU MENGI SANA YSTENDEKAYO MA NI FUNGUO TOJS KWA MAMBO YOTE YALIYOSHINDIKANA TUITUMIE ILI TUPATE LUWEKWA HURU

  3. annastella says:

    Asanteni. Na pia ni vema kujifunika kwa damu ya yesu kila siku na kukiri kuwa hatutokufa bali tutaishi…

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: