Namna ya Kupanda Mbegu ya Ukuu

HOW TO SOW THE SEED OF GREATNESS

NAMNA YA KUPANDA MBEGU YA UKUU (HOW TO SOW THE SEED OF GREATNESS).

“MBEGU YA UKUU” Inaweza Kupandwa, Kuota, Kukua Na Kutoa Matunda/ Matokeo Kwenye Udongo Wa Aina Moja tu “KUMJUA MUNGU”
Kadri Unavyozidi Kupata “UFUNUO” Kuhusu Mungu Na “KANUNI/ SHERIA ALIZOWEKA ZITAWALE JAMBO FULANI, NDIVYO AMBAVYO UTAKUWA MKUU KWENYE JAMBO HUSIKA”
Kuna Watu Ni Hodari Kiroho Lakini Ni Dhaifu Kwenye Ndoa Zao,
Kuna Watu Ni Hodari Kiroho Lakini Ni Dhaifu Kwenye Uchumi Wao,
Kuna Watu Ni Hodari Kwenye Maeneo Kadhaa Ya Maisha Lakini Maeneo Mengine Wamechoka; Tatizo Limekaa Kwenye “UPANA, UREFU, KIMO NA KINA CHA UJUZI WAKO KUHUSU MUNGU NA KANUNI ALIZOWEKA ZITAWALE MAISHA”
“Bali Watu WAMJUAO MUNGU WAO Watakuwa HODARI Na Watatenda MAMBO MAKUU” (Daniel 11:32).
“MJUE SANA MUNGU Ili Uwe Na AMANI Ndivyo MEMA YATAKAVYOKUJIA” (Ayubu 22:21).
“Na Uzima Wa Milele Ndio Huu, WAKUJUE WEWE, MUNGU WA PEKEE WA KWELI, Na YESU KRISTO Uliyemtuma” (Yohana 17:3).
Kiwango Cha Ubora Wa Maisha Yako HAKIWEZI KUZIDI Kiwango Cha SIRI ZA MUNGU Ulizonazo Kuhusu Maswala Ya Kila Siku Ya Maisha;
“Kama Nilivyokuwa Katika Siku Za Ujana Wangu, Hapo SIRI YA MUNGU Ilipokuwa Juu Ya Hema Yangu” (Ayubu 29:4 KJV).
Na Hili Upate SIRI ZA MUNGU Mlango Wa Kuingilia Huku Ni UCHA MUNGU Kwenye Maeneo Yote Ya Maisha Yako;
“SIRI YA BWANA Iko Kwao WAMCHAO, Naye [BWANA] Atawajulisha AGANO Lake” (Zaburi 25:14).
Hilo Jambo Unalohangaika Nalo Kwenye Maisha Ni Kwa Sababu Kuna SIRI Kuhusu Hilo HUIJUI; Usitumie Nguvu Kubwa, Waendee Waliofanikiwa Katika Hilo, WATAKUELEKEZA WAO WALICHOFANYA Halafu Utatoka… Wengine Huwezi Kuwaona, Au Kupata Nafasi Ya Kuonana Nao, Lakini Unaweza KUSIKILIZA CD/ DVD ZAO, Kusoma Vitabu Vyao, Kupitia Website Zao Nakadhalika… Fanya Hivyo Na Utakutana Na SIRI Ambazo Ziliwafanya Wao Wafike Hapo Unapotamani Kufika!

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
0655 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: