Kama una Mashaka na Huamini huduma ya mtumishi fulani

Mashaka

KAMA UNA MASHAKA NA HUAMINI HUDUMA YA MTUMISHI FULANI, USIFUNGUE MDOMO KUMSEMA AU KUWASHAWISHI NA WENGINE WAWE NA CHUKI NAYE; KWA KUFANYA VILE, HATA KAMA UNACHOKISEMA NI SAHIHI, LAKINI TAYARI HAUJAKIFANYA KWA KANUNI ZA KIMUNGU, CHUKI YAKO NI SAWA NA UUAJI!
NJIA RAHISI YA KUSHUGHULIKA NA HUYO AMBAYE WEWE UNA MASHAKA NA HUDUMA YAKE AU HUAMINI KWAMBA NI MTUMISHI WA MUNGU, FANYA HAYA YAFUATAYO:

1.Yesu Alisema “TUTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO” (Mathayo 7:15-23) Yaani Tutawatambua Kwa “KILE WANACHOZALISHA” Yaani Kama “WANACHOTOA KINAJENGA UFALME WA MUNGU”, “KINAMTANGAZA YESU NA MSALABA”, “KINALETA WATU TOKA DHAMBINI KUINGIA KWENYE UTAKATIFU”, “KINATOA WATU KWENYE MIKONO YA ADUI KUWAINGIZA KWA BWANA YESU”
Angalia Huyo Mtumishi Anafanya Yafuatayo:
-Anaamini Na Kuhubiri Kuhusu Wokovu Kupitia Msalaba; Ulazima Wake, Umuhimu Wake Na Madhara Ya Kutookoka Hapa Duniani Na Maisha Baada Ya Kifo.
-Anakubali Na Kufundisha Kuhusu Umuhimu Wa Maisha Ya Utakatifu Na Kumcha Mungu Kwa Washirika Wake Na Watu Wengine.
-Anaiamini Na Kuiheshimu Biblia Kama NENO LA MUNGU Na MAAGIZO HALALI YA MUNGU Nakadhalika.

2.Kama Kimetoka Kwa Mungu “KITASIMAMA” Na Kama Hakijatoka Kwa Mungu “KITAKUFA”… Hauhitaji Kushindana Na Mtumishi Yeyote Wa Mungu, Au Anayejiita Wa Mungu: Hii Ni Kanuni Ya Kimungu Ya Kuamua Mambo, Chochote KISICHOTOKA KWA MUNGU KITAKUFA; ILA KILICHOTOKA KWA MUNGU HAKIWEZI KUFA, KADRI KINAVYOPIGWA VITA NDIVYO KINAVYOZIDI KUSTAWI NA KUONGEZEKA… Matendo 5:34-39.

3.Kama Unajua “WEWE UKO VIZURI NA MUNGU” Yaani Unajiona Wewe Ni Mkamilifu Na Rafiki Wa Mungu, Basi “OMBA HUYO NDUGU NA HUDUMA YAKE WANG’OLEWE” Maana “KILA PANDO ASILOPANDA BABA WA MBINGUNI LITANG’OLEWA” Lakini Ukiona “UMEOMBA NA KUKAZANA KUMNG’OA LAKINI BADALA YAKE NDIO ANAZIDI KUSTAWI NA KUONGEZEKA NEEMA NA NGUVU” Ujue “WEWE NDO UNA MATATIZO” Na Ujue “ULIKUWA UNASHINDANA NA MUNGU” Na “UMESHALIKOROGA”

4.Kama Una HEKIMA ZAIDI: Tumia BUSARA Aliyoitoa Yesu “KWENYE MFANO WA NGANO NA MAGUGU” Yaani “VIACHE MAGUGU NA NGANO VYOTE VIKUE PAMOJA” Halafu “MUNGU ATAFANYA MWENYEWE KAZI YA KUTENGA NA KUTOFAUTISHA NGANO NA MAGUGU”
Usijaribu Kufanya Kazi Ambayo Si Yako!

Ile tu Kwamba Mtumishi Fulani “HAHUBIRI AU KUFUNDISHA” Kama “MCHUNGAJI AU ASKOFU WAKO” Haimfanyi Kutokuwa MTUMISHI WA MUNGU… MUNGU ANAYETENDA KAZI NDANI YA WOTE NI MMOJA; LAKINI KWA KILA MTU MUNGU ANATENDA KAZI KWA NAMNA TOFAUTI… Usije Kujiingiza Matatani Ka Kutumia Vigezo Vyako Vya Macho Na Masikio Ya Utafiti!

Usiku Mwema,
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
0655 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: