Kila Mkiristo lazima aombe kila Siku

Maombi

KILA MKRISTO LAZIMA AOMBE WALAU SAA 1 KWA SIKU; ULAZIMA, UMUHIMU WA HILO NA MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA KWA SAA 1 AU ZAIDI… SOMA HII IKUSAIDIE KWENYE MAISHA YAKO YA MAOMBI!

Kiwango Cha Chini Kabisa Cha Muda Ambacho Mungu Anatarajia Mkristo Akitumie Kwenye Maombi “KWA SIKU” Ni “SAA 1”
Mathayo 26:37-44 Inatueleza Habari Ya Yesu Na Wanafunzi Wake Walivyokwenda Bustanini Kuomba; Yesu Aliomba Lakini Wanafunzi Wake Walisinzia.
Alipowajia, Yesu Aliwauliza Swali Lililobeba “KIASI CHA MUDA” Ambao Ni Wa Lazima Kwa Kila Mtu Kuutumia “KWENYE MAOMBI KWA SIKU”
“JE HAMKUWEZA KUKESHA NAMI WALAU KWA SAA MOJA?”
Yesu “ANAKAA KWENYE MAOMBI AKITUOMBEA SISI” (1Yohana 2:1-2, Waebrania 7:25, Warumi 8:34).
Lakini Yesu Anatarajia “KILA SIKU” Mimi Na Wewe “TUTAUNGANA NAYE KUOMBA” Kwa Walau “SAA 1” Yaani Kama Wanafunzi “WALIVYOKESHA NA YESU” Yesu Anatarajia Kuona Mimi Na Wewe “TUKIKESHA NAYE KILA SIKU KWA WALAU SAA 1 KWENYE MAOMBI”
Inawezekana Huna Uwezo Na Stamini Ya Kuomba “SAA 1 MFULULIZO” Lakini Hiyo Haigeuzi Ukweli Kuwa “YESU ANATAKA KILA SIKU UOMBE NAYE SAA 1 AU ZAIDI” Hata Kama Umebanwa Kiasi Gani, “SAA 1 KATI YA 24 ULIYONAYO, YESU ANATARAJIA ULITUMIE KWENYE MAOMBI PAMOJA NAYE, YAANI UKESHE NAYE KUPITIA MAOMBI”
Ili Kulifanya Hilo Liwezekane, Inahitaji “MBINU ZA MAOMBI” Ambazo “ZITAKUSAIDIA UWEZE KUTUMIA SAA 1 AU ZAIDI KWENYE MAOMBI”

MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA WALAU SAA 1 KILA SIKU NA BWANA YESU:

1.KUOMBA KWA VIPINDI VIPINDI
Unaweza Kuomba Kwa Vipindi Vipindi Kadhaa Kwa Siku. Unaweza Kuomba ASUBUHI NA JIONI, Ama Unaweza Kuomba Mara 3 Kwa Siku Yaani ASUBUHI, MCHANA NA JIONI, Au Unaweza Kuomba Mara 4 Kwa Siku Yaani ASUBUHI, MCHANA, JIONI NA USIKU KABLA YA KULALA!
Jambo La Msingi Ni Kwamba “JUMLA YA VIPINDI VYAKO VYA MAOMBI KWA SIKU VISIWE PUNGUFU YA SAA MOJA; VIWE SAA MOJA AU ZAIDI”

2.KUOMBA KWA KUTUMIA KANUNI YA UFALME WA MUNGU KWANZA
Mathayo 6:33 Inasema “UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE, NA HAYO MENGINE YOTE UYATAKAYO UTAZIDISHIWA”
Hii Mbinu Ni Maalumu Kwa Wale Ambao “HAWANA UWEZO WA KUOMBA SAA MOJA AU ZAIDI” Kwa Kigezo Kwamba “WANAISHIWA MAMBO YA KUOMBEA”
Unapoingia Kwenye Maombi, Anza Kwanza Kuombea “MASWALA YA UFALME WA MUNGU KWANZA KABLA YA KUOMBEA MAMBO YAKO BINAFSI”
-Ombea Huduma Zote Tano Za Kuujenga Mwili Wa Kristo (Waefeso 4:11), Yaani Ombea WAALIMU WA NENO LA MUNGU: Waombee Uwezo Wa Kukaa Barazani Kwa Mungu Na Kuchukua CHAKULA MEZANI PAKE KUKILETA KWA KANISA, Ombea WACHUNGAJI: Waombee Mungu Awape Nguvu Ya KUCHUNGA KONDOO ZAKE, Mungu Awape Nguvu Ya KUTAFUTA MALISHO KWA AJILI YA KONDOO, Mungu Awape Uwezo Wa Kuwajali Na Kuwa Tayari KUTOA UHAI WAO KWA AJILI YA KONDOO, Wasiwe WACHUNGAJI WA MISHAHARA TU BALI WANAOSIMAMIA MASLAHI YA UFALME WA MUNGU Nakadhalika, Ombea WAINJILISTI: Mungu Awape Roho Ya Hekima, Ufunuo Na Uweza, Ili WAIHUBIRI SIRI YA WOKOVU KWA UJASIRI NA NGUVU, HUKU ISHARA, MAAJABU NA MIUJIZA IKIFUATANA NAO… Ombea MANABII WA KWELI WA MUNGU: Mungu Awatetee Na Kuwapigania Mbele Ya Kila Mbinu Na Mpango Wa Adui Kujaribu Kuwapinga Na Kuwazuia, Mungu Azidi Kufungua Macho Na Masikio Ya Mioyo Yao Ili Wapokee PACKAGE ZA WATU, NCHI, KANISA Nakadhalika… Ombea MITUME, Mungu Awatumie Kufika Maeneo Ambako Kazi Ya Mungu Haijafika Na Wakaanzishe Kule Kazi Na Zisimame Na Kutoa Matunda!
UNAPOOMBA KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU; USIOMBEE KANISA/ DHEHEBU LAKO TU, OMBEA MAKANISA NA MADHEHEBU YOTE YANAYOSIMAMIA KAZI ZA UFALME WA MUNGU!

-Kwenye Kipengele Cha Kuomba Kwa Ajili Ya Ufalme Wa Mungu;
Ombea Watu Ambao WAMESHAOKOKA WASIMAME: Kwa Kuwaombea Wengine, UNAMFANYA MUNGU AKULINDE WEWE USIMAME KWENYE WOKOVU, Maana Kipimo Unachopima UNAPIMIWA!

-Kwenye Kipengele Cha Kuomba Kwa Ajili Ya Ufalme Wa Mungu;
Ombea UMOJA WA KANISA: Mitume Wawe Na Umoja Kihuduma, Manabii Wawe Na Lugha Moja, Walimu Wasimame Pamoja Na Kwa Umoja, Wainjilisti Wafanye Kazi Ya Injili Pasipo Mashindano Bali Kwa Upendo Na Umoja, Wachungaji Wapendane, Wawe Wamoja Na Wasiwe Na Mashindano… Kwa Kuwaombea WATUMISHI, UNAFUNGULIA MLANGO WA UMOJA, NA KUIZUIA ROHO YA UDINI NA UDHEHEBU NA KUINUA BENDERA YA YESU!

-Kwenye Kipengele Cha Kuomba Kwa Ajili Ya Ufalme Wa Mungu;
OMBEA AMBAO HAWAJAPATA NEEMA YA WOKOVU ILI NAO WAOKOLEWE: Kwa Kuombea Walioko Dhambini, Unamfungulia Mlango Mungu Kukusaidia Ili Wewe Usirudi Dhambini… Kwa Kuombea Ambao Hawajapata Neema Ya Wokovu Utakuwa Umefungulia Mlango Kwa Mungu Kuwaokoa Ndugu Zako, Marafiki, Jamaa Zako Ambao Hawajaokoka… Usisahau Yesu Alisema, “ANYWESHAYE NAYE ATANYWESHWA”

-Kwenye Kuombea Kipengele Cha Ufalme Wa Mungu;
KABLA YA KUOMBEA MAHITAJI YAKO KWANZA WAOMBEE WANA WA MUNGU WENGINE WALIOKO KWENYE SHIDA AU UHITAJI KAMA WAKO: Kwa Kufanya Hivyo Utakuwa UMEOMBEA VIUNGO WENGINE WA MWILI WA KRISTO, Na Mungu Atainua Watu Wa Kukuombea Na Wewe Pia, Lakini Pia UTAMFANYA MUNGU AONE UPENDO WAKO HALAFU ATAKUGUSA WEWE KWANZA HATA KABLA HUJALISEMA LAKO MBELE ZAKE!

-Kwenye Kipengele Cha Kuombea Ufalme Wa Mungu;
OMBA UDHIHIRISHO NA UHALISI WA UFALME WA MUNGU UONEKANE HAPA DUNIANI, KUPITIA WATU WALIOOKOKA KWENYE UCHUMI, UONGOZI, UTAWALA, UBUNIFU, UANZISHAJI MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO, NGUVU ZA MUNGU KUBWA MAKANISANI KIASI CHA WATU KUACHA KWENDA KWA WAGANGA NA KUJA KUTAFUTA SULUHU KWA YESU MAKANISANI: Ukiomba Ombi Hili Kwa Dhati, Mungu ATAANZA KUKUTUMIA WEWE KWANZA KUWA BORA KWENYE MAENEO YOTE HAYO NILIYOKUDOKEZA!

Je Hadi Hapa, Unadhani Utashindwa Kuomba Walau Kwa Saa 1 Kwa Siku Na Kukesha Na Yesu?
Naamini Umepata Cha Kukusaidia.

NINI KINATOKEA AU NINI MADHARA YA KUOMBA PUNGUFU YA SAA MOJA KWA SIKU?

1.Mwili Wako Unaanza Kuwa Na Maamuzi Na Sauti Kubwa Kuliko Roho Yako, Hivyo Kuishinda Dhambi Inakuwa Kitendawili… Ukiwa Na Utaratibu Wa Kuomba Kila Siku Wastani Wa Saa 1 Unakuwa Na Uwezo Rohoni Kwako Wa Kudhibiti Mwili, Na Kushinda Tamaa Za Mwili Na Udhaifu Wake. Ukisoma Ile Mathayo 26:37-44, Yesu Anasema “ROHO I RADHI LAKINI MWILI NI DHAIFU”… Udhaifu Wa Mwili Unathibitiwa Na Muda Wa Kutosha Kwenye Maombi.

2.Usipoweza Kuomba Kwa Saa Moja Au Zaidi Kwa Siku; Inakuwa Rahisi Kwako Kuingia MAJARIBUNI; Yesu Alipokuwa Akifundisha Kuhusu “SALA YA BABA” Alisema Tumwombe Baba “ASITUTIE MAJARIBUNI BALI ATUOKOE NA YULE MWOVU” (Mathayo 6:13), Usipoomba Kwa Saa 1 Au Zaidi KUMSIHI MUNGU AKUEPUSHE NA MAJARIBU; HAKIKA YATAKUKUTA UKIWA HAUJAJIPANGA NA SHETANI ATAKUSHINDA NA KUKUTOA HATA NJE YA IMANI.

3.Usipoomba Kwa Saa Moja Au Zaidi HAUTAPATA MKATE WAKO WA KILA SIKU; Kwenye SALA YA BWANA Yesu Anatuambia “TUMWOMBE MUNGU ATUPE MKATE WETU WA KILA SIKU” Hii Ina Maana Zote Mbili “KIROHO NA KIMWILI” Yaani Usipoomba Kwa Saa 1 Au Zaidi Kwa Siku, “UTAKULA KWA JASHO” Chakula Chako; Yaani SIKU ITAKUWA NGUMU KWENYE UTAFUTAJI NA KAZI MAANA UKO PEKE YAKO… Lakini Hautaweza Pia Kupata “MKATE [NENO AU UFUNUO]” Wa Kukusaidia Kwa Siku Husika Toka Kwa BWANA, Hivyo “UTA-STRUGGLE” Kama Mara Nyingi Ninavyosikia Watu Wakisema!

MUNGU AKUSAIDIE KUTENDEA KAZI SOMO HILI,
AKUPE NGUVU YA KUOMBA ZAIDI YA SAA MOJA KWA SIKU,
UOMBE KWA AJILI YA UFALME WAKE KWANZA,
UOMBEE WENGINE WENYE UHITAJI,
UOMBEE WALIOKO DHAMBINI WAFIKIE NA INJILI NA WAOKOLEWE,
HALAFU NDIPO UOMBEE MAMBO YAKO.
NDIPO UTAANZA KUONA MATOKEO YA MAOMBI YAKO!

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
0655 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
One comment on “Kila Mkiristo lazima aombe kila Siku
  1. ELISHA DAUDI says:

    Mungu akubariki mtumishi wa Bwana, nimebarikiwa na somo lako, Mungu anisaidie niweze kuomba walau hata saa 1 kwa siku,,

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: