nizungumze kidogo kuhusu BARAKA

https://i1.wp.com/www.commentsyard.com/graphics/blessings/blessings36.jpgBiblia Inatuambia Wazi Ya Kuwa, “BARAKA YA MUNGU HUMKALIA MWENYE HAKI KICHWANI” (Mithali 10:6). Na Pia Tunaambiwa Kuwa, “BARAKA YA BWANA HUTAJIRISHA, WALA HACHANGANYI HUZUNI NAYO” (Mithali 10:22).
Hii Ina Maana Hii:

1.BARAKA ZINATOKA KWA BWANA; YEYE NDIYE CHANZO CHA BARAKA ZOTE; Kama Isemavyo Mwanzo 1:28 Ya Kuwa “MUNGU AKAWABARIKI [BINADAMU ALIOWAUMBA] AKASEMA ZAENI, MKAONGEZEKE NA KUIJAZA NCHI”
Kuwa Na Uwezo Wa “KUZAA” Na Baada Ya Kuzaa Inafuata Hatua Ya “KUONGEZEKA NA KUIJAZA NCHI [DUNIA YAKO]”

2.BARAKA HUWA INAMKALIA MWENYE HAKI
BARAKA YA MUNGU HAIKAI JUU YA KILA MTU; Ni Wale WANAOISHI MAISHA YA HAKI KWENYE MAENEO YOTE, HAO NDIO WALIO KWENYE “FOLENI” YA KUBARIKIWA NA BWANA.
Mithali 8:20-21 Mungu Anasema “NINAPITA KWENYE NJIA YA HAKI; KATIKATI YA MAPITO YA HUKUMU [NENO/ SHERIA YANGU] ILI NIWARITHISHE MALI WALE WANIPENDAO”
Kiukweli “JICHO LA MUNGU LIMEWEKWA JUU YA MTU WA HAKI”
Kama Ni MJANJA MJANJA; Unafanya UONGO/ USWAHILI KWENYE MAISHA YAKO: “HAUTAKUTANA NA BARAKA YA MUNGU HATA SIKU MOJA” Na Hicho Unachokusanya “KWA NJIA HARAMU” Kuna Siku Inakuja “KITAPIGWA NA KUPOTEA MARA” Au “KITAKUGHARIMU; MALIPO YA ASIYE HAKI NI HAPAHAPA DUNIANI”

3.BARAKA HUKAA KWENYE KICHWA CHA MWENYE HAKI
BIBLIA INASEMA NI KWENYE KICHWA: Inakuja Kama “MAWAZO” Au “MAONO” Au “NDOTO FULANI YA MAISHA” Ambayo “UKIITII NA KUITENDEA KAZI SAWA NA MAELEKEZO KUNA SIKU ITAKUTOA”
Mungu “HAWEKI PESA MKONONI, WALA UTAJIRI KWENYE MFUKO WAKO” Bali “ANAKIJAZA KICHWA CHAKO NA MAARIFA NA SIRI ZAKE AMBAZO KAMA UKIZITENDEA KAZI ZINAKUTOA CHINI KWENDA JUU”
SIRI ZA MUNGU ZIKO KWAO WAMCHAO; NAYE KAMWE HAACHI KUWAJULISHA WATUMISHI WAKE SIRI ZAKE [MAWAZO, MAONO NA NDOTO ZA KUGEUZA NA KUINUA MAISHA YAO]!
Yusufu Alipopata Baraka Ya Mungu; Ilikuja Kichwani Kwake; AKAJUA SIRI YA NDOTO YA FARAO… AKAJUA SIRI YA KUFANYA NYUMBA YA POTIFA ISTAWI… AKAJUA SIRI YA KUWA BORA GEREZANI HADI AKAWA KIONGOZI WA WAFUNGWA NAKADHARIKA!
BARAKA YA MUNGU INASHUGHULIKA NA KICHWA CHA ALIYEBARIKIWA; NA UKIANZA KUIWEKA KWENYE MATENDO, MUNGU ANAKUWEPO “KUSIMAMIA IWE HALISI BILA KAUZIBE ZA ADUI [SHETANI] NA WANADAMU”

4.BARAKA YA MUNGU INATAJIRISHA
Baraka Ya Mungu Inasukumu UTAJIRI UJE MAISHANI MWA ALIYEBARIKIWA; HAUTUMII NGUVU NA JASHO KUTAJIRIKA, WALA HAUTUMII MUDA WAKO KARIBU WOTE WA SIKU UKIKIMBIZA UTAJIRI NA MALI; BALI KUNAKUWA NA “NEEMA NA REHEMA ZA MUNGU” AMBAZO ZINAKUSAIDIA “WAKATI WA MAHITAJI”
UNATUMIA ILE BARAKA “KICHWANI” KWENYE MATENDO, HALAFU MAMBO YANATOKEA!

5.BARAKA YA MUNGU HAICHANGANYI HUZUNI
KAMA KWELI HICHO ULICHONACHO UMEKIPOKEA KWENYE MIKONO YA MUNGU; HAKIWEZI KUKULETEA HUZUNI… KINAAMBATANA NA UWEZO WA KUKUFARIJI, KUKUTIA MOYO NA KUINUA FURAHA NA AMANI YAKO MAISHANI!
IBRAHIMU ALIPOPOKEA BARAKA YA MUNGU; MBALI YA KWAMBA HAKUWA NA MTOTO, NA ALISUBIRI MIAKA ZAIDI YA 25 LAKINI BADO HAKUWA NA HUZUNI WALA KUKOSA AMANI; ILE BARAKA YA MUNGU ILIKUWA IKIINUA MOYO WAKE NA IMANI YAKE KWA MUNGU.
HAUWEZI KUWA UMEPOKEA AU KUPEWA JAMBO LOLOTE NA MUNGU HALAFU LIKAWA CHANZO CHA KILIO, MAUMIVU NA MATESO MAISHANI MWAKO!
“KILA KUTOA KULIKO KWEMA NA KILA KITOLEWACHO KILICHO KAMILI HUTOKA JUU KWA BABA WA MIANGA AMBAYE KWAKE HAKUNA KIVULI CHA KUGEUKAGEUKA” (Yakobo 1:17).

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
0655 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: