Ushuhuda huu utageuza Maisha Yako:Usome ukusaidie

https://fbcdn-sphotos-d-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash3/527066_441892622566007_1409957347_n.jpgKaribu Miezi Miwili Iliyopita, Nilitembelea Group Mojawapo Hapa Facebook Na Kukutana Na Dada Gwantwa Wilson Akiwa “Ame-post” Ujumbe Juu Ya Matatizo Ya Kiafya Aliyonayo Hasa Tatizo La PUMU [ASTHMA] Ambalo Lilikuwa Likimsumbua.
Nilipoiona Ile Post Yake, “HURUMA YA KIMUNGU [Compassion]” Ilinishika, Nikacomment Kwenye Ile Post Na Kumwekea Namba Yangu Ya Simu Ili Anaitafute Kwa Ushauri Na Maombezi.
Ulipita Karibu Mwezi Mmoja Hivi Bila Kunitafuta, Lakini Siku Moja Nikiwa Kwenye Daladala Kwenda Ubungo Simu Iliita, Na Namba Mpya Ilikuwa Inapiga.
Niliipokea Ile Simu Na Kumsikiliza; Akajitambulisha Na Kunikumbusha, Nikawa Nimemkumbuka.
Nikamuulizia Aliko, Akanielekeza Kuwa Yuko Hospitali Ndogo [Zahanati] Iliyoko UKONGA; Nikamwambia Naelekea Ubungo, Nikimaliza Kilichonipeleka, MOJA KWA MOJA NAKUJA HUKO ULIKO, NA YESU ATAKUPONYA!
Nilipomaliza Mizunguko Yangu Huko Ubungo, Nikapanda Daladala Na Kwenda Huko Alikokuwa… Njiani Nilimwambia Mungu, “NAJUA HUPENDI WATU WAKO WATESWE NA MAGONJWA WALA DHAMBI AU LOLOTE LISILO JEMA; NAKUOMBA UNIPE NEEMA, UMPONYE HUYU BINTI KWA MIKONO YANGU”
Nilipofika Pale Alipokuwa, Nilimsubiri Amalize Taratibu Za Hospitali, Na Kisha Tukapata Muda Wa Kwenda Sehemu Kukaa Na Kuongea Kwa Kirefu.
Baada Ya Kuyasikiliza Maelezo Yake; Nami Nilimpa “MAELEZO SAHIHI” Yaani “KILE BIBLIA INASEMA KUHUSU AFYA YAKE” Na Kile “AMBACHO YESU AMESHAFANYA KWA AJILI YA AFYA YAKE PALE MSALABANI ZAIDI YA MIAKA 2000 ILIYOPITA”
Baada Ya Kunielewa Na IMANI YAKE KUINUKA; Niliweka Mikono Yangu Juu Yake “KWA MAMLAKA YA JINA LA YESU NA NENO LAKE” Kisha Nikaamuru “KILA UGONJWA NA UDHAIFU KWENYE ULE MWILI UMWACHIE NA UONDOKE”
Na Papo Kwa Hapo Aliponywa Na Akaanza Kupumua Vizuri Bila Shida Yoyote, Nguvu Zake Zikarudi, Akawa Mwepesi!
Tukaagana Akarudi Kwao Nami Nikarudi Kwetu!

Kesho Yake, Alinitumia Meseji Akisema, “MTUMISHI, UTUKUFU KWA YESU, TANGU JANA BAADA YA MAOMBEZI HADI LEO SIJAPATA MASHAMBULIZI YA ASTHMA TENA; MWANZONI NILIKUWA NIKISIKIA TU HARUFU YA MAFUTA AU PAFYUMU KIFUA KINABANA NA HALI YANGU INAKUWA MBAYA; LAKINI KWAKWELI, TANGU JANA SIPATI TENA TATIZO HATA NIKITUMIA MAFUTA NA PAFYUMU AU HATA NIKIPITA KWENYE VUMBI; HAKIKA YESU AMENIPONYA”

Hadi Sasa Ni Zaidi Ya Mwezi Umepita, Dada Huyu Ni Mzima, Ameponywa Kabisa, Anaendelea Mbele Na Yesu Na Hata Maisha Yake Ya Kiroho Yameimarika Sana.
Hii Ni Kututhibitishia Ukweli Wa Maneno Ya BWANA YESU;
“MWANA AKIKUWEKA HURU UNAKUWA HURU KWELIKWELI”

Wewe Unateswa Na Nini? Je Unadhani Hilo Tatizo Lako Ni Kubwa Kuliko Nguvu Ya Msalaba Wa Yesu? Je Ni Matatizo Ya Kiafya? Una Ugonjwa Ambao Hospitali HAWAUONI LAKINI UNAENDELEA KUTESEKA? Ama Una Ugonjwa Ambao Hospitali Hawana Dawa? Je Ni Biashara Yako? Je Ndoa Yako Haijakaa Sawa? Je Ni Familia, Watoto Wako Wanakusumbua? Nini Kinakunyima Raha?
YESU AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU; AMEJITWIKA HUZUNI ZETU (Isaya 53:4), Kwani Uendelee Kuteseka?

Yesu Yuko Tayari Kukusaidia, Anasubiri tu Uamuzi Wako;
Nitafute Kwa Msaada Wakati Wowote;
0655 466 675
dicoka@rocketmail.com
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in ushuhuda
2 comments on “Ushuhuda huu utageuza Maisha Yako:Usome ukusaidie
  1. Evodius yohana says:

    Hongera mtumish mungu kwa kuyatumia mamlaka ya jina la yesu cfa na utukufu apewe yeye nmebarkiwa na ushuhuda huu kwani imani bila matendo imekufa

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: