TABORA, WIKI LA PASAKA, 16-20 APRIL 2014!

Tabora

Nakusalimu Katika Jina Kuu La Yesu Kristo Wa Nazareti, Mwana Wa Mungu Aliye Hai, Ni Imani Yangu Kwamba Mungu Anakutunza Na Kukutendea Mema.
Kutokana Na Kichwa Hapo Juu, Tunatarajia Kuwa Na Huduma Ya Injili Mkoani Tabora, Wilaya Ya Tabora Mjini, Kwenye Kata Za KILOLENI, ISEVYA, IPURI NA MWINYI Kuanzia 17/04 Hadi Jumapili Ya Pasaka 20/04.

IDADI YA WATENDA KAZI WANAOTARAJIWA KWENDA HUKO

Tunatarajia Kuwa Na Timu Ya Walau [Minimum] Watenda Kazi 50 Ambao Wengi Wao Watakuwa WANAVYUO WALIOOKOKA TOKA FELLOWSHIP MBALIMBALI HAPA DAR ES SALAAM Pamoja Na WATUMISHI BINAFSI WANAOGUSWA NA INJILI TOKA HAPA DAR NA MIKOANI [AMBAO MNAGUSWA NA KAZI YA INJILI NA MNGEPENDA KUWA SEHEMU YA KAZI HII, NA MUDA WA KUWA NASI HUKO KATIKA KIPINDI HICHO]!
Kwa WALE MSIO WANAVYUO, LAKINI WENYE UTAYARI WA KUWA NASI KWENYE HUDUMA HIYO; TUTATOA NAFASI 10 HADI 15 KUTOKANA NA MAZINGIRA YATAKAVYOKUWA!

HUDUMA ZITAKAZOFANYIKA KWENYE HUDUMA HII

Tutakuwa Na Huduma Kadhaa Kwenye Huduma Hii Ya Siku 5 Huko Tabora Kama Ifuatavyo:
1)MAOMBI YA KUTEMBEA [WALKING PRAYER]
Haya Yatafanyika Kila Siku Ya Huduma Toka Alhamisi Hadi Jumapili [April 17-20] Na Yatakuwa Maalumu Kwa KUSHUGHULIKA NA KILA FALME NA MAMLAKA ZINAZOZUIA HALI YA KIROHO, UCHUMI, ELIMU Kwenye Eneo Husika Na Mkoa Mzima Wa Tabora.
Yatakuwa YAKIANZA SAA 10:00-12:00 ALFAJIRI

2)USHUHUDIAJI WA NYUMBA KWA NYUMBA [DOOR TO DOOR EVANGELISM]
Hii Itakuwa Ushuhudiaji Na Ufikishaji Habari Njema Za Msalaba NYUMBA KWA NYUMBA Kwenye Mitaa Kupitia Watenda Kazi Ambao Watakuwa Kwenye TIMU ZA WAWILI WAWILI AU WATATU WATATU.
Watafikisha Habari Njema, Watombea Wagonjwa Na Wenye Shida Mbalimbali, Watafikisha Taarifa Kwa Ajili Ya Mikutano Ya Injili YA JIONI, Wataandika Majina Ya Waliokata Shauri Kumpokea Yesu, Namba Zao Za Simu Na Mitaa Yao KWA AJILI YA UFUATILIAJI ZAIDI BAADA YA HUDUMA Kupitia WACHUNGAJI WENYEJI NA WATENDA KAZI WATAKAOBAKI.

3)SEMINA KWA AJILI YA WAONGOFU WAPYA [WALIOKATA SHAURI KUMPA YESU MAISHA- NEW CONVERTS]
Lengo La Semina Hizi Itakuwa Kuwajenga Na Kuwasaidia WAKRISTO WAPYA WALIOKATA SHAURI KUYATOA MAISHA KWA YESU Waweze KUELEWA THAMANI YA WOKOVU WALIUPOKEA, KUWAANDAA KUVIPIGA VITA VIZURI VYA IMANI Nakadhalika.
Watakuwepo WATENDA KAZI Ambao Ni WALIMU Watakaobaki KUIFANYA HIYO KAZI Wakati Wengine Wakiwa Kwenye USHUHUDIAJI WA NYUMBA KWA NYUMBA!

4)MIKUTANO YA NJE YA INJILI (CRUSAIDES)
Kuanzia Alhamisi Hadi Jumapili, April 17-20 Kutakuwa Na MIKUTANO YA NJE YA WAZI YA INJILI Ambayo INALENGA KUWAFIKIA WATU KWA HABARI NJEMA ZA UFALME WA MUNGU… Watakuwepo WATENDAKAZI WAINJILISTI Waliofundishwa A,B,C Za Injili Ambao WATAWASILISHA UJUMBE WA MSALABA KWA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU NA KUVUNA ROHO ZA WENGI KWA YESU!

5)HUDUMA YA SINEMA BAADA YA MKUTANO WA INJILI
Kila Baada Ya Mikutano Ya Injili Kutakuwa Na ONESHO LA SINEMA Ambalo Litaambatana Na MAELEZO YA KIINJILI NA WITO WA WOKOVU Kwa Watazamaji Ambao UTALETA WATU KWA YESU.
Tunajua Kwamba Kama Ilivyokuwa Kwa NIKODEMO, Kuna Watu WANAOGOPA KUJITOKEZA MCHANA KWEUPE ILA WANAWEZA KUWA “WANAFUNZI WA SIRI WA YESU” Mpaka Pale WATAKAPOKUA NA KUJISIMAMIA KIIMANI; HAO NAO TUNATAKA KUWAVUTA KWA YESU!

MAHITAJI YA HUDUMA HII ILI IFANIKIWE
1)Tunahitaji Watu Wenye Utayari WA KUJITOA WAO NA MUDA WAO Na Kuwa Tayari KUWA NASI HIYO TAREHE 16 HADI 20 APRIL; Ni Sadaka Yako Ya Upendo Kwa BWANA Na Pia Ni Darasa Lako La Utumishi, Na Utakuwa Umefanya Kitu Kwa Ufalme Wa Mungu… Kumbuka Ziko Nafasi KUMI NA TANO TU KWA WASIO WANAVYUO/ RAIA WA KAWAIDA.

2)TUNAHITAJI WALAU MILIONI 5 AU ZAIDI KUFANIKISHA HUDUMA HII, NAZO ZIKO KWENYE MGAWANYO UFUATAO:
-Usafiri Wa Timu Nzima Ya Watu 50, Kwenda Na Kurudi
-Usafirishaji Wa Vyombo Kwa Ajili Ya Mikutano Na Sinema [Vifaa Vya Mziki Na Vinginevyo]
-Chakula Cha WATENDAKAZI [Breakfast, Lunch, Dinner] Kuanzia Tarehe 16 Hadi 20 April
-Malazi [Matandiko, Mikeka, Mazuria, Maturubai Nakadhalika]

HUBIRI NA SISI KWA KILE KIDOGO MUNGU ALICHOKUPA
Leo Ni Januari 18, Na Huduma Ipo April 16 Hadi 20. Tumekushirikisha Hili Jambo Mapema Ili Upate MUDA WA KUTOSHA KUANDAA SADAKA YAKO NZURI KWA AJILI YA KAZI HII NJEMA YA MSALABA.
Tutaanza Kupokea Sadaka Yako Mara Tu Utakapomaliza KUUSOMA UJUMBE HUU Na KUUWEKA KWENYE MAOMBI Na KUPATA KIASI CHA KUTOA; MAANA MUNGU HUWAPENDA WALE WATOAO KWA MOYO WA KUPENDA, SI KWA KULAZIMISHWA WALA KUSUKUMWA.
Hivyo Basi, UNA MWEZI WOTE HUU WA JANUARI NA MWEZI WOTE WA FEBRUARI PIA; KAA NA KUTAFAKARI NA KUAMUA UNATUPELEKA KUHUDUMU KWA SADAK KIASI GANI [UNAVYOSUKUMWA MOYONI MWAKO]!
Mwisho Wa Kupokea Sadaka Itakuwa mwanzoni mwa Mwezi MACHI, Ili Tupate Fursa Ya Kuanza MAANDALIZI YA HUDUMA HIYO; KIMAFUNDISHO, MAOMBI NA KUKUTANIKA ILI TUFAHAMIANE NA KUPEANA MAJUKUMU.
Maandalizi Yatakuwa Walau Ya Mwezi Mmoja Mfululizo Tangu Machi, Maana Tunataka Kufanya Kazi Ya Uhakika, HATUTAKI KULIPUA AU KUZIMA MOTO!

MSISITIZO ZAIDI

Andaa Sadaka Yako Nzuri Na Uipeleke Injili Nasi; Nisingependa Kutaja Viwango [Roho Mtakatifu Aseme Nawe Kibinafsi] Ili Kuanzia Leo Hadi Mwisho Wa Februali UWE UMEFANYA KITU CHA KUELEWEKA KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU.
Ila Naomba, Ukishapata Amani Ya Kushiriki Kuipeleka Injili Kwa Sadaka yako, Tafadhali Nijulishe Ili KUWEKA AHADI YAKO [PLEDGE] KWA KAZI HII YA MUHIMU YA MUNGU; Hii Itakufanya Ufanye Bidii Kuiondoa, Maana Usipoji-commit Ni Rahisi Adui KUKUPA MAWAZO YA KUTOTOA TENA NA UKAISHIA KUTOKUWA SEHEMU YA BARAKA HII!
Pia Napokea Ushauri Na Mawazo Kama Yapo Kwa Simu Nitakazoweka Hapa.
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675 — with Godfrey Kamwaya and 19 others.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: