UKWELI KUHUSU MELI KUBWA YA TITANIC NA CHANZO CHA KUZAMA KWAKE

(Soma Ni Muhimu Kujua Hili Litakusaidia)

Watu Wengi Mmesikia Kuhusu Meli Iitwayo TITANIC. Ambao Hamkuwa Mkiijua Sana Basi Mtakuwa Mliiona Ile Picha Ya Romeo Na Julieth.

Ile Ilitengenezwa Ikiwa Meli KUBWA Kuliko Zote, SALAMA Kwa Viwango Vya Kimataifa, Na Pia Ilikuwa Ya KIFAHARI Kuliko Zote Ambazo Umewahi Kuzijua.

Wakati Imemalizwa Kuundwa Na Kuingizwa Majini, Ikafanyiwa Majaribio, Kila Mtaalamu Wa Maswala Ya Uchukuzi Aliamini Ni Meli Bora, Imara, Kubwa Kuliko Zote, Salama Na Ya Kifahari Pia.

Hakuna Aliyewahi Kufikiri Au Kuwaza Kuwa Hii Meli Iliyoundwa Kwa UMAKINI, UBORA NA VIGEZO Vya Kimataifa Ingeweza Kuzama, Tena Katika Safari Yake Ya KWANZA. Lakini Ilitokea, Na Hiyo Meli ILIZAMA Katika Safari Yake Ya KWANZA Ikiwa Inatoka Mji Wa Southampton Uingereza Kwenda New York Marekani.

Zilipotolewa Habari Za KUZAMA Kwa Meli Hiyo, Na Majina Kutolewa, Kulikuwa Na Orodha Mbili Tu Ambazo Zilitupiwa Macho Na Ndugu Za Wasafiri Waliokuwa Ndani Ya Meli. Orodha Zilizotolewa Toka Kwenye Tukio Hilo Zilikuwa WALIOOKOLEWA Na WALIOPOTEA!

Lakini Kabla Ya Kuzama Kwa Meli Hiyo, Kulikuwa Na Orodha Nyingi Zaidi Ya Hizo Mbili. Kulikuwa Na Orodha Ya Waliokuwa DARAJA LA KWANZA; MATAJIRI, Waliokuwa DARAJA LA PILI; WATU WA KATI Na Watu Wa DARAJA LA TATU; WATU WA KIPATO CHA CHINI.
Na Katika Hiyo Meli, Kulikuwa Na Matabaka, Tofauti Za Kimaisha Na Heshima Kati Yao Kama Ilivyo Leo Kwenye Maisha Yetu. Tofauti Ya Hadhi, Heshima, Thamani Na Umuhimu Wetu Vinatofautiana Kwa Sababu Ya Hali Zetu Za Maisha.

Lakini Kuna Siku Ambayo Tutasimama Mbele Za Mungu. Mimi Na Wewe… Tajiri, Mtu Wa Kati Na Hata Masikini. Na Zitatolewa Orodha Mbili Tu. Na MAISHA YAKO YA MILELE Yatategemea Uko Kwenye Orodha Ipi.
Mbele Za Mungu Kutakuwa Na Orodha Ya WALIOOKOLEWA Na WALIOPOTEA!
Dunia Yetu Ni TITANIC Ya Sasa, Imebeba Watu Wa Aina Zote, Na Sasa Iko Katikati Ya TUFANI, Inazama Taratibu… Mungu Hataki TUZAME NA KUINGIA KWENYE ORODHA YA WALIOPOTEA…Ametoa BOTI YA WOKOVU Iitwayo YESU KRISTO, Mwanae Aliyekufa Msalabani Ili Awe FIDIA Ya Dhambi Na Maovu Yako. Yaani Mungu Alimtoa Yesu Mwanae Wa Pekee, Afe Msalabani Alipe DENI Ya Dhambi Zako, Ili Wewe Uhesabiwe Haki Bure, Na Upewe Haki Ya Kuokolewa Toka Kwenye DUNIA INAYOZAMA Na UINGIE Kwenye BOTI YA WOKOVU Ambayo Wote WALIOOKOLEWA Wanapanda Boti Hiyo!

Fanya UAMUZI WA BUSARA LEO; Usiseme Mimi Nina Dini Yangu Nzuri, Nina Imani Niliyokulia Tangu Nikiwa Mtoto. Hata Waliokuwa Kwenye TITANIC Hawangekuelewa Kuwa ITAZAMA Tena IKIWA NI SAFARI YAKE YA KWANZA… Usichezee Maisha Ya Milele. Mungu Hapendi UPOTEE MILELE JEHANAMU, Bali Anataka UOKOLEWE Na Kuishi Naye Rahani Milele… Mungu Anataka UOKOLEWE; Ndio Maana Ametoa BOTI YA WOKOVU Iitwayo YESU… Tafadhali Mpe Yesu Nafasi Akuokoe Na Kukuingiza Kwenye Orodha Ya WALIOOKOLEWA! Usichezee Nafasi Hii, Mimi Sikujui Lakini Mungu Anakujua. Amekupa Nafasi Ya Kusoma Ujumbe Huu Kwa Kuwa Anataka UOKOLEWE, Hapendi UPOTEE!

Kama Unajua Haujaokolewa, Yesu Si BWANA Na Mwokozi Wako, Lakini Hautaki KUZAMA Na Hii Dunia Inayozama Taratibu, Basi Fanya UAMUZI Bora Wa Kuyaokoa Maisha Yako Milele, MPE YESU MAISHA YAKO!

Kwa Ajili Ya KUOKOKA, Kujifunza Zaidi Kuhusu Wokovu Na Maisha Ya Utakatifu Na Jinsi Ya Kuishinda Dhambi, Wasiliana Nami Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila;
0753 466 675 Au 0655 466 675
Usikubali KUPOTEA MILELE JEHANAMU, AMUA LEO!
@April 2013, Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
3 comments on “UKWELI KUHUSU MELI KUBWA YA TITANIC NA CHANZO CHA KUZAMA KWAKE
  1. Naomba uniombee maana napenda kuishi maisha ya ukiristo lakini vikwazo huja mbele yangu 0783879834

  2. Godfrey mshaula says:

    una akili kweli ww?

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: