KWA WAOAJI NA WAOLEWAJI TU

kwa waoaji na waolewaji

Kosa Kubwa Wanalofanya Waoaji Na Waolewaji WENGI (KAMA SI WOTE) Ni Kuoa/ Kuolewa “KUTOKANA NA MAHITAJI YALIYOPO” Yaani “KUOA/KUOLEWA KUTOKANA NA HALI YA WAKATI HUO” Mfano:

-Mkaka Mweusi ANAOA Binti MWEUPE WA SURA Bila Kujali Kigezo Cha Ukweli Kwamba “KUNA KESHO MBELE YAO” Ambayo “HAIHITAJI WEUPE WA SURA BALI MAONO, NJOZI NA AKILI ZA KUONA YASIYOONEKANA YALIYOKO KESHO”… Ni Kweli Wataoana Lakini Baada Ya “MUDA KIDOGO” Tutawaona “WANACHECHEMEA” Maana “ALIOA SURA NA SI MKE”

-Dada ‘TOKA FAMILIA MASIKINI’ Kwa Kuchoshwa Na MSOTO ALIOPITIA, Anaamua ‘KUOLEWA NA MWENYE PESA’ Bila KUCHUNGUZA AU KUWA NA UHAKIKA Na “CHANZO CHA PESA” Kama “CHA HAKI” Au Kama “HUYO KIJANA ANA AKILI ZA KUTOSHA ZA ROHONI NA KIMAISHA KUWEZA KUTUNZA NA KUDUMU TAJIRI KATIKA KESHO YAO” Na Mwisho Wa Siku Ikitokea “DHORUBA NA UCHUMI UKAYUMBA AU KUFA” Basi Na “NDOA INAYUMBA AU KUFA”… Ni Kweli WAMEOANA, Lakini Ukweli Ni Kwamba, “AMEOLEWA NA MALI AU PESA NA SI MTU” Na Wakati Wowote UCHUMI USIPOELEWEKA NA NDOA IMEKWAMA!

TURUDI KWENYE BIBLIA:

-Yakobo ALIOA SURA NZURI YA RAHELI Na KUTOMTHAMINI “SURA MBAYA LEAH” Lakini “HAKUJUA KUWA RAHELI NI MWABUDU MIUNGU MINGINE” Hivyo “ALIOA SURA NZURI” Kutokana Na Mahitaji Yake Ya Wakati Huo Lakini “HAKUZINGATIA HALI YA KIROHO YA RAHELI WAKE” Na Mwisho Wa Siku “HAKUFIKA NAYE MBALI”

-Daudi ALIMWOA BINTI WA MFALME SAULI AITWAYE MIKALI (Alioa Kwa Kuangalia Kigezo Cha FAMILIA BORA) Kwa Vile “ALITOKA FAMILIA MASIKINI NA ALITAKA KUPANDISHA CV YAKE” Lakini Hakujua Kuwa ANAMUOA MWANAMKE Ambaye “ANAWAONEA WATU AIBU KULIKO MUNGU” Na Siku Daudi Alipocheza Na Kusifu Mbele Za Mungu Kwa Nguvu Mpaka Vazi Lake Likadondoka, “MKEWE MIKALI MPENDA SIFA ZA WANADAMU” Alimkemea Mmewe Daudi “KWAMBA AMEJISHUSHA HADHI NA KUJIDHARAULISHA MBELE ZA WATU” Yaani “HAKULINDA HADHI YAKE NA HESHIMA MBELE ZA WATU”… Ni Kweli Alioa Mke Toka Ndani Ya FAMILIA BORA, Lakini Hakuzingatia Kigezo Kwamba “ASIWE ANAYEWAHESHIMU WATU KULIKO MUNGU”

-Mfalme Suleiman, Mwana Wa Daudi; Huyu Alikuwa Na WAKE 300 Na Masuria (NYUMBA NDOGO) 700, Jumla 1000!
ALIOA KUTOKANA NA MAZINGIRA ALIYOKUWEMO WAKATI HUO BILA KUJALI “KESHO YAKE NA YA TAIFA LAKE”… Kutokana Na Kuzungukwa Na Nchi Nyingi Ambazo Zilikuwa Na UADUI KWAO, Suleiman Aliamua KUOA Mke Toka Kwenye Kila UFALME ULIOMZUNGUKA, Ikiwa Ni Njia Ya KUTENGENEZA URAFIKI NAO, ILI WASIJE WAKAINGIA NAO KWENYE VITA… Ni Kweli ALIOA WAKE, Lakini ALIOA TOKANA NA HALI ILIYOMZUNGUKA “KWA WAKATI HUO” Hivyo BADALA YA KUPATA SULUHU, MWISHO WA SIKU ALIHARIBIKIWA ZAIDI!

TUNACHOJIFUNZA HAPA:
-Usioe Au Kuolewa Kwa Sababu Ya Mazingira Au Changamoto UNAYOPITIA, Usioe Au Kuolewa Eti Kwa Vile umri umekwenda, Au Kwa Vile Wazazi Na Ndugu Zako Wanakupa Presha Kuhusu Hilo (Hawaoi/ Hawaolewi Wao Bali Wewe, Ndoa Ni Swala La Kwako Binafsi), Usiolewe Au Kuoa Kwa Kigezo Cha Mwenzi Mwenye Pesa, Familia Bora, Kiwango Cha Elimu Nakadhalika, HAYA YOTE YANAWEZA KUBADILIKA KESHO INGAWA LEO YANAONEKANA NI YA MUHIMU AU YA LAZIMA… Kumbuka Unaoa Na Kuolewa Na MTU NA SI HALI YAKE AU VITU VYAKE… Swala La Ndoa NI UTU ZAIDI (THAMANI YA MTU ALIVYO KIROHO, KITABIA, KIAKILI, KIMTAZAMO, KIMAONO, KIMIPANGO NK) Na Si Vile ALIVYO LEO!
KUMBUKA NENO LA MUNGU LINASEMA”
“TUSIVIANGALIE VINAVYOONEKANA BALI VISIVYOONEKANA; MAANA VUNAVYOONEKANA NI VYA MUDA TU, BALI VISIVYOONEKANA NI VYA MILELE [VYA KUDUMU]” (2Kor 4:18)!

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo, ndoa

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: