Kanuni ya Uchumi na Fedha

Uchumi na Fedha

Uchumi na Fedha

Yesu Alisema Katika Ule Mfano Wa WATUMWA NA TALANTA, Ya Kwamba Yule Aliyepewa TALANTA MOJA Aliichukua Ile TALANTA Na Kisha AKAIFUNGA KWENYE LESO AKAITUNZA [AKAIWEKA AKIBA] Lakini Wale Wengine Wawili, Yaani Aliyepewa TALANTA MBILI Na Aliyepewa TALANTA TANO, Wao “HAWAKUZIFUNGA KWENYE LESO NA KUZITUNZA” Bali “WALIZIINGIZA KWENYE MZUNGUKO WA PESA NA KUZIZALISHA” Na Baada Ya Muda Yule Aliyepewa TALANTA MBILI AKAWA NA TALANTA NNE [Akapata FAIDA YA TALANTA MBILI] Na Yule Aliyepewa TANO Baada Ya Muda AKAWA NA TALANTA KUMI [Akapata Faida Ya TALANTA TANO]!

TUNAJIFUNZA NINI HAPA:

Yule Mtumwa Aliyepewa TALANTA MOJA Yeye ALIIWEKA AKIBA Bila KUIZUNGUSHA NA KUIZALISHA Na AKAENDELEA KUWA NA KIASI HICHO HICHO…. Cha Kujifunza Kwenye UCHUMI NA FEDHA: KILA UNACHOKIWEKA AKIBA, BILA KUKIZUNGUSHA KITABAKI VILEVILE, NA BAADA YA MUDA THAMANI YAKE ITAKUWA IMESHUKA!
Yule TAJIRI Aliporudi Na Kuikuta TALANTA MOJA Bila Kuzalishwa HAKUMKASIRIKIA NA KUMWEKA KIFUNGONI YULE MTUMWA “KWA KUPOTEZA MALI YAKE” Hapana! ALIMWEKA KIFUNGONI KWA SABABU, “THAMANI YA TALANTA ILE MOJA KWA WAKATI ULE ILIKUWA IMESHUKA BAADA YA MUDA KUPITA BILA KUIZALISHA”
Umeawahi Kujiuliza Mtu Aliyeweka Akiba Ya Shilingi LAKI MOJA MWAKA 2000??? Ni Kweli Kwamba ATAKUWA NA LAKI YAKE MOJA, Lakini THAMANI YAKE YA WAKATI HUU NI TOFAUTI SANA NA YA MWAKA 2000.
Hiki Ndicho Kilichomfanya TAJIRI Amtupe Kifungoni Yule MTUMWA MBAYA NA MLEGEVU!

Wale Watumwa Wengine Wawili [WA TALANTA MBILI NA WA TALANTA TANO] Wao HAWAKUWEKA AKIBA Bali “WALIWEKEZA AKIBA” Yaani WALICHUKUA ZILE TALANTA ZAO NA KUZIZUNGUSHA SOKONI, ZIKAZAA NA KUONGEZA THAMANI KADRI MUDA ULIVYOKUWA UNASOGEA!

KWAKO WEWE:

Usipende Kuweka Pesa Akiba, Sio Jambo Jema Maana “THAMANI YA PESA INASHUKA KADRI MUDA UNAVYOSOGEA”
Ukipata Pesa IWEKEZE, Irudishe Sokoni Izunguke… Kama Huna Biashara Au Shughuli Ya Kuzalisha Pesa Husika Basi NUNUA KITU AMBACHO THAMANI YAKE INAPANDA KADRI MUDA UNAVYOKWENDA Mfano: ARDHI, MASHAMBA, MIGODI, MIFUGO, NYUMBA Nakadhalika Maana Baada Ya Muda Hivi VITU VINAPANDA BEI NA KUKUPA ZAIDI YA ULICHOWEKEZA!!!
Ukiona Hii Njia Huiwezi PELEKA KWA WATOA RIBA [VICCOBA, SACCOS Etc] Ambao WATAKUZUNGUSHIA PESA YAKO Kupitia Watu WATAKAOKUJA KUKOPA NA KUIZALISHA KWA RIBA!!!

Ukiwa Masikini Si Kwa Sababu Biblia Haijatoa Suluhisho, Bali Kwakuwa MACHO YAKO HAYAKUONA SIRI KWENYE MAANDIKO Na Hata Kama Yaliona, Basi HUKUYATENDEA KAZI Kwenye Maisha Yako Ya Kila Siku.

HII NI HEKIMA YA KUTUNZA PESA YAKO NA KUIONGEZA,
KAZI NI KWAKO,
“Kuzaliwa Familia Masikini Si Kosa Lako Ila Kufa Masikini Ni Kosa Lako”
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “Kanuni ya Uchumi na Fedha

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: